Wabunge hawa hawatarudi Bungeni 2015

Status
Not open for further replies.

Atubela

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2011
Posts
749
Reaction score
854
Kutokana na hali inavyoendelea sasa kuna bahadhi ya wabunge wa upinzani wanaonekana dhairi hawatarudi tena katika bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ukimuondoa Mzee Ndesamburo ambae hatarudi kulingana na afya yake, lakini jimbo lake tayari lishaonekana kurudi CCM, kutokana na mtu wanaetegemea kumsimamisha kuwa hauziki, au kutokana na dini yake... (si unajua chama chetu)

1. Ezekiel Wenje

2. Highness Kiwia Huyu na Wenje waliupata ubunge kutokana na vita baridi iliokuwepo kati ya Masha na

3 Godbless Lema huyu Arusha ndio hawataki hata kumsikia akigombea hata udiwani

4 Mchungaji Msigwa Huyu nae aende akachunge kondoo wa Iringa, ukichukulia Chaguo lao lilikuwa Mwakalebela.

5 Joseph Mbilinyi

6 Tundu Lissu Huyu ndio Kabisaaa

7 John Mnyika Hili jimbo la huyu jamaa, mwenyewe Nape Nnauye

Jimbo la Shibuda anarudi nalo CCM na Makamu mwenyekiti wao Arfi kwakua hatagombea, jimbo lake linarudi CCM

Kama kuna wengine waweke lakini hawa wakirudi nipigwe ban ya maisha JF


 
Katika kizazi hiki kilicho na mwamko wa hali ya juu sana kote nchini, ni wabunge 17 ndio watakaorejea bungeni kama wabunge wa zamani; wengine wote wale wateteao chama badala ya umma wa Tanzania wao ni kwenda nyumbani kimoja.
 
Tuwekee vigezo ulivyotumia ambavyo vimepelekea wewe kufikia hitimisho lako...
 
Jitaje na wewe basi jimbo lako litachukuliwa na nani naona una machungu sana huna lingine la kuwaza?
 
Anza kujadili kwanza tutaondoaje umasikini kwa hawa raia wetu wanao ishi kwa Tsh 650 kwa siku na ni kwanini serikali ambayo imeaminiwa miaka 50 imeshindwa kutoondolea hilo, ni yupi inatakiwa awe wa kwanza kuondolewa yule aliyepewa miaka hamsini akaishia kutengeneza watu kama wewe wanaofikiria kwa matumbo baadala akili kwasababu unaamini propoganda ndizo zinatatua matatizo.

Ni vizuri tukajitofautisha na kina Lusinde na mwigulu na wenzake kwa kuwambia nini hasa inatakiwa kifanyike kututoa hapa tulipo kuliko kuendelea kuwatumbukiza watu kwenye umasikini usio na kifani wakati wamekalia kila aina ya utajiri
 
Chadema inawasha kuliko pilipili manga na badoo.

Ulishawahi kusikia/kuona pigo kwa ccm 2015?..badooooooo.
 
Mkuu mimi naona ungekamilisha list kama ungemaliza na Mhe. Mbowe, huyu jamaa wananchi wa Hai walikuwa hawajui kama kala sifuri kidato cha sita (6), sasa wamejua na wamechachamaa kwelikweli, wamesema hata awape Bilicans bungeni awamrudishi.
 
Yaani mimi napafahamu Moshi ndugu yangu.
Pale ukizungumzia CCM limebaki jina tu na vitega uchumi vyake. Siongei kwa ushabiki kwa sababu sipo CCM wala Sipo Chadema. Akiondoka mzee Ndesa wale watu wa pale watachagua chama cha Chadema na sio mtu.
Na ni sababu Chadema ina nguvu sana kuliko chama chochote pale.
Na hata Cirily Chami naye sidhani kama ataweza kusurvive 2015 pale.
Na kwa Ubungo ninachojua ni kuwa Mnyika ana nguvu sana na Chadema ina nguvu sana.
TUZUNGUMZE KWA FACTS NA SIO KWA USHABIKI.
Ni kama Vunjo pale Mrema ana nguvu sana yeye kama yeye sidhani kama TLP ina nguvu yoyote
 
ni hisia na matakwa ya chama tawala kuwapigia debe heb jipange na ulete maada nyingine naona maruerue. Cjapata hoja ya msingi hata moja kwa rais wa mby unazo wasilisha maana uamuzi n wetu wapiga kura na maendeleo yaonekanayo mitaan na ci porojo majukwaani.
 
Nimejiwekea utaratibu, ili niisome coment nilazima niangalie chini ---- kuna mtu ame-'LIKE' lakini hapa thread nzima sioni 'LIKES'
 
tunashukuru, najua umepata buku 7 ya kula mchana, basi nenda kapumzike, maana ayo mawazo yako hayana uchambuzi wowote, wala vigezo, umeandika tu. ila najua hao ndio wanaowanyima usingizi ccm. na bado poleni sana.
 
Sio mbaya kupima upepo kwa vinyweleo japo sikushauri kuzoea tabia hyo
 
Uzi umejaa chuki binafsi kuliko vigezo na sababu za msingi!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…