Wabunge: Fedha za EPA ziende TANESCO

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Wabunge: Fedha za EPA ziende TANESCO

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

BAADHI ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wameitaka serikali kuligawia Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) fedha za akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) zinazorejeshwa na mafisadi waliochota fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Walisema ili waridhike na urejeshwaji huo ni vema TANESCO ikapewa fedha hizo, ili kuboresha miundombinu yake itakayoiwezesha kutoa umeme wa uhakika mpaka maeneo ya vijijini.

Walisema hayo kwenye semina ya majadiliano ya muswada wa sheria za umeme na biashara ya mafuta ya petroli inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni kwenye mkutano ujao wa 11 unaotarajiwa kuanza Aprili 8 mjini Dodoma.

Akizungumzia hilo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Benson Mpesya, alisema hivi sasa TANESCO imekuwa tegemezi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuhimili gharama za uzalishaji umeme na badala yake wamekuwa wanunuaji wakuu wa umeme kwa kampuni binafsi.

"Fedha za EPA zinazorejeshwa tunataka wapewe TANESCO, ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kupeleka umeme kwa watu wengi zaidi," alisema Mpesya huku akishangiliwa na wabunge wenzake.

Naye Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, alisema kinachopaswa kufanywa na serikali hivi sasa ni kuboresha shirika hilo na si kuleta mipango ya kuruhusu wawekezaji katika sekta ya umeme, ili kushindana na TANESCO.

Alisema tatizo la TANESCO linajulikana wazi kuwa ni mzigo mkubwa wa kuzilipa kampuni zinazozalisha umeme baada ya viongozi wa serikali kuingia mikataba mibovu kwa masilahi binafsi.

"Kama pesa ipo, wapewe TANESCO si kuanza kuja na mipango ambayo ni kiini macho na ina lengo la kuwapa ulaji zaidi hao wawekezaji na kuiumiza TANESCO," alisema Kimaro.

Aidha, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema tatizo lililopo nchini ni kuwa wanatafutwa wawekezaji walalahoi na kupewa zabuni kubwa ilimradi fedha za walipa kodi zitumike.

"Sasa ni wakati wa kuwapa fedha zetu TANESCO na wala si wawekezaji wa kigeni ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliotufikisha hapa tulipo," alisema Mwakyembe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Mbunge wa Njombe Kusini, Anne Makinda, alisema muswada wa sheria ya umeme na biashara ya mafuta ya petroli kwa kiasi kikubwa haukupata baraka za wadau, kwani una mapungufu mengi na haonyeshi kama una nia ya dhati ya kuilinda TANESCO.

"Huu muswada haujapitia kwenye taasisi zenu na wadau wengine, kwani una kasoro nyingi na nina wasiwasi kama mtaweza kuhimili vishindo vya wabunge," alisema Makinda ambaye pia ni Naibu Spika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shelukindo, alisema tatizo la serikali ni kukalia ushauri wa wabunge ambao huonya juu ya jambo na kuitaka serikali isilifanye.

Alisema matokeo ya kukalia ushauri wa wabunge, ni kulifanya taifa lijikute likiingia katika matatizo makubwa, hasa kiuchumi na hata kuingia mikataba mibovu.

"Sisi tunapotoa ushauri huwa hatutoi kwa chuki kwa mtu Fulani, bali tuna nia ya kulijenga taifa, lakini kwa wenzetu wa serikali inaonekana labda tumeutoa kwa sababu ya chuki," alisema Shelukindo.

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na naibu wake, Adamu Malima, waliwaahidi kuyafanyia kazi mawazo hayo kwa masilahi ya taifa.

Malima alisema hakuna sababu kwa wabunge kuogopa miswada hiyo, kwani haina kitu kipya, kwa sababu taratibu za kununua umeme kutoka mashirika binafsi unafanyika, ila si kwa sheria zilizowekwa wazi, hivyo ni vema kukawepo sheria hizo.

"Kuna taratibu zinazofanyika katika sekta ya umeme na tunachohitaji hivi sasa ni kuweka sheria, ili kuweza kubana maeneo yenye utata," alisema Malima.

Aidha, Ngeleja alisema serikali imetenga sh bilioni 79 kuhakikisha umeme unafika vijijini na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi.

"Tunajitahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kuboresha sekta ya nishati na hivi sasa tumeelekeza nguvu zetu kupeleka umeme vijijini," alisema Ngeleja.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, aliionya serikali isijaribu kuacha kuwa msimamizi mkuu wa kutoa umeme.

Alisema kama serikali itafanya hivyo kuna hatari baadhi ya mikoa nchini kukosa huduma za umeme, kwani wawekzaji hupenda kuangalia maeneo fulani na kwa lengo la kutengeneza faida.

"Tuseme ukweli, hivi ni mwekezaji gani ambaye atakwenda kuwekeza sehemu ambazo anajua hatapata faida, hasa katika mikoa ya kusini au ya pembezoni mwa nchi?" alihoji Dk. Rashid.

Alisema Watanzania wamekuwa wakifanya mambo kwa makosa, hasa kwenye nishati ya umeme, hivyo ni vema hivi sasa wakawa makini, ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari ya kutokea kwa mgawo wa umeme kutokana na uhaba wa maji mwaka huu.

Muswada wa Sheria ya umeme na biashara ya mafuta ya petroli, ambao una lengo la kutoa fursa kwa kampuni nyingine kuzalisha umeme na kusambaza kwa kiasi kikubwa, unaelekea kugonga mwamba kutokana na asilimia kubwa ya wabunge kutouunga mkono.

Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 21 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
hizi hela zipo kweli jamani au hilo ni changa tuu

na k - 20.03.08 @ 22:17 | #3104

hizo hela ni changa

na k - 20.03.08 @ 22:18 | #3105

NDUGU WABUNGE KAMWE MSIKUBALI HUO MUSWADA UPITE BUNGENI HUKO BUNGENI.. ILA MIMI NAPENDA KUWAAMBI UKWELI NANYI WABUNGE WETU MKIWA NJE MWAONGE VIZURI SANA NA KWA MASLAHI YA TAIFA KWELI ILA MKIINGIA HAPO BUNGENI MTATOA KASORO NA MAPUNGUFU YOTE YAMISWAADA NA HOJA MBALIMBALI THEN AT THE END UTASIKIA MBUNGE ANASEMA NAUNGA MKONO HOJA 100% SASA KWA NINI UUNGE MKONO MSWADA MBOVU? UKATAE ILI UKAFANYIWE MAREKEBISHO MLIOYASUGGEST THEN UKIKAMILIKA NDO MUUNGE MKONO,,,BUT NAWAPONGEZA SIKUHIZI KIDIGO MNABADILIKA NA KUACHANA NA UNAFIKI HUO NAWAOMBA MUACHANENAO KABISA UNAFIKIAHUO NA MLINDE NA KUYATETEA MASKAHI YA NCHI KIKWELI

na PEMBE, Italy, - 21.03.08 @ 02:20 | #3106

WABUNGE WA TANZANIA HONGERENI SANA. MWENYEZI MUNGU AWABARIKI SANA. MLIKUWA WAPI MIAKA YOTE HII?? HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA, WATU WAWE MAKINI KWA MASLAHI YA TAIFA. TUKATAE KUFANWA WAJINGA KILA WAKATI NA WATU WABINAFSI WACHACHE AMBAO HAWANA NIA KABISA YA KULETA MAENDELEO YA NCHI. you will make a good legacy if you will save this nation from collapse!!!

na Peter, US, - 21.03.08 @ 02:52 | #3107

HIVI SELIKALI YA CCM MNAMATATIZO GANI, YAANI NYIE KILA KUKICHA MWAPIGANIA TU KUYALETA MAKAMPUNI YA WAZUNGU HAPA NCHINI HIVI WAZUNGU WAMEWALISHA NINI ETI NYIE AU MMELISHWA LIMBWATA AU WAMEWACHEZEA AKILI THEN WANANCHI TWABAKI KUWALAUMU KUMBE MUWAGONJWA TAYARI,,,MWAJUA FIKA TANESCO HAPO ILIPO NI MATOKEO YA HIZOHIZO KAMPUNI ZA KIGENI THEN BADO MNATAKA KUZITUNGIA HADI SHERIA,,WHAT ARE U DOING U GUYS OF CCM..
OKAY SASA U NGELEJA NA WATAALAMU WAKO WOOTE YAANI MLIKAA NAKUANDAA HUO MUSWADA MKAUONA KABISA IS PROFFITABLE KWA TAIFA UA? YAANI MNAFANYA MAMBO KAMA VILE MNATEGESHA DILI ILI TUKIJICHANAGANYA TU BABA AKE TUMELIWA... MIMI NAWASIWASI SANA HATA HII MISWADA MTAKUA MNAANDALIWA NA HAO HAO WAZUNGU THEN NYIE MNAWASILISHA TU BUNGENI BILA KUJUA KILICHOPO HASA NDANI,,JUST IMAGINE MUSWADA UNASAHIHI YA MTU BAKI(karamagi)
NA SIO WAZIRI NGELEJA SASA HIVI TUKIKUITA NGELEJA NA HAO WENZAKO WENDAWAZIMU TUTAKUA TUNAKUONEA ,,HAHAHA THIS IS FUNNY,,,,MIMI NAOMBA WATZ WENZANGU TUFUATILIE HASAANAYEANDAA HII MISWADA, HAPA MIMI NIMESHTUKA SI WIZARA ZETU JAMANI,,,
MAONI YANGU..
1.NAOMBA MISWADA YOTE IWE INASAMBAZWA KWENYE MEDIA LIKE NEWSPAPPERS ILI WANANCHI TUIPITE NA KUTOA MAONI YETU KABLA HAIJA PELEKWA BUNGENI,,,MAANA NAONA TULIO WATRUST KULINDA MASLAHI YA TAIFA LETU NDO WAMEKUA MA-AGENT WA KUYAIBA.
2.SERA YA UBINAFSISHAJI NI NZURI BUT SIO KIWENDA WAZIMU KAMA CCM MNAVYOFANYA HATA HAO MABWANA ZENU WAZUNGU HAWABINAFSISHI HADI SEKTA NYETI ZA JAMII,,,MAANA NAONA SASA SIAJABU KESHO MKAPELEKA MUSWADA WA KUBINAFSISHA JWTZ...
3.TANESCO IMEIOMBA SERIKALI TRILLION 1.6,IT MEANS IMEPUNGUKIWA HELA ZAKUJIENDESHA SASA TUUZIENI HISA WANANCHI ZIZIDIZO 50% ILI TUONGEZE MTAJI KWA TANESCO YETU NA TUIENDESHE WENYEWE KULIKO KUKIMBILIA LETA MABWANA ZETU WAZUNGU HAPA NCHINI KWETU.
,,,,TANESCO IS NOT FOR COMMERCIAL BUT FOR PUBLIC SERVICE,,,

na PEMBE, Italy, - 21.03.08 @ 03:00 | #3109

Tatizo kubwa la nchi ni kukosa viongozi wenye uzalendo kwa maana viongozi wataoweka mbele maslahi ya taifa mbele na siyo maslahi ya mtu binafsi. kwa mfano ktk swala zima la uwekezaji tulichokuwa tunahtaji siyo mtaji isipokuwa ni utahalamu na vitendea kazi na siyo mtaji kama wanavyodai viongozi hawa uchwara. watanzania wenyewe wangeuziwa hisa asilimia 60% ili kampuni au shirika liwe bado mikononi mwa watanzania wenyewe na siyo serikali. WAtanZANIA wenyewe ndio wakae chini na wawekenzaji wa nje na kuangalia namna ya kuendesha kampuni. Wenye hisa kubwa ambao ni Wantanzania wenyewe wasingeweza kukubali upumbavu unaofanyika hivi sasa wa kuwaachia wageni wafaidike na wao kuambulia patupu. kama unahitaji milioi 500, uza shea millioni moja kila shea shillingi mia tano. ni asilimia kubwa ya watanzania wanao uwezo wa kununua na shea kwa shillingi mia tano. dhumuni likiwa kuwajengea watanzania nafasi ya kuweza kufaidika wao moja moja ili waweze kuboresha maisha yao na familia zao badala ya kuinufaisha serikali ambapo pesa zote zinaishia mikononi mwa wachache. Moja kati sharti la uwekezaji ni kuajiri watanznaia na kama hakuna mtanznaia mwenye utaalamu huo basi mwekezaji atawajibika kutumia mtaalam kutoka nje na wakati huo huo mwekezaji atatakiwa kupewa muda maalum wa kutumia mtaalamu wa nje ili kutoa nafasi kwa mtanzania kuwatrained ili kuchukua nafasi ya mtaalam wa nje mara muda wake utakapokwisha. Watanzania tukitaka maendeleo ya kweli ni lazima tuweke mbele utaifa wetu kwa kuweka mbele kwanza Watanzania na raia wageni kufuata baadaye kwani tusijidangaye watanzania ukienda kwa watu weupe kazi uwapa watu wao kwanza na siyo kuwaacha raia wao na kuwapa wageni hakuna upumbavu kama huo nchi nyingi zilizoendelea. lakini rushwa imeturudisha nyuma sana inawafanya Viongozi wengi kuwa kama vipofu wasioona na kukubali masharti yanayotolewa na mgeni badala ya mwenye nyumba kuwa sauti mgeni ndio anakupangia masharti hii aiwezekani kabisa watanzania. watanzania tumekosa viongozi wenye uchungu na nchi mfano waziri mkuu Lowassa alitusaliti watanzania wenzake kwa kutulaza gizani miezi kadhaa kwa uroho wake wa fedha hii inatia uchungu sana.

na nick, Tanzania, - 21.03.08 @ 04:54 | #3110

Mimi nadhani there is something wrong somewhere in our minds/brain!! Why katika kutafuta suluhisho ya mambo yanayotushinda kuendesha (kutokana na uzembe/ubinafsi wetu) basi the simple and quick solution ni KUBINAFSISHA, tena kwa STRANGERS, WHHY? Hivi ni kweli kwamba WE CAN'T THINK OF SOME OTHER BETTER SOLUTIONS zaidi ya huo ubinafsishaji?? Inakera sana, hao waliopo madarakani ndo waamuzi wa maisha ya waTZ woooote sisi hata na ya vizazi vijavyo? Manake hapo utackia mikataba hiyo ni kuanzia 10-15yrs!! Sijui, ila it has to reach a point now na sisi tuanze kuwa na our own ways of solving our own problems, hizi sera za ubinafsishaji ni mbinu za wenzetu kujipatia ajira kwenye nchi za wengine/wajinga kwani kwao ajira hamna, so ni ubunifu wao katika kusaka ajira za watu na makampuni yao. Ipo siku utasikia kuwa eti, SERIKALI YA TZ IMESHINDWA KUJIENDESHA,suluhisho ni AJE MWEKEZAJI(tena wa nje) KUIENDESHA! mi cjui, huenda ikatokea kutokana na style iliopo TZ! Ahsanteni.

na Farry, Tanzania, - 21.03.08 @ 08:20 | #3113

na Farry, Tanzania, - 21.03.08 @ 08:21 | #3114

na Farry, Tanzania, - 21.03.08 @ 08:29 | #3115

na Farry, Tanzania, - 21.03.08 @ 08:34 | #3116

Kwa kweli wabunge mkiendelea hivyo bila shaka Tanzania ya asali na maziwa inawezekana. Hongera zangu kwenu kwa muda

na Quara, Mwanza, - 21.03.08 @ 09:11 | #3118

TANESCO WANA MIUNDOMBINU YA KUTOSHA KINACHOWAKWAZA NI MZIGO WA MADENI AMBAYO YAMETOKANA NA MIKATABA MIBOVU ILIYOKWISHA ONEKANA KWAMBA INAWEZA KUVUNJWA BILA MADHARA YEYOTE KWANINI HAIJAVUNJWA MPAKA SASA?HIZO PESA ZA EPA ZIJENGWE DARAJA LA KIGAMBONI WATANZANIA TUACHANE NA SQUARTERS NA UVUNJAJI HUKO MBELENI TUANZE KUPUNGUZA CONGESTION YA MAGARI HUKU TUKIKUZA UTALII.TUKIBINAFSISHA SEKTA HII NYETI WATANZANIA TUTAENDELEA KUPIKIA KUNI KWANI HATA GESI LICHA YA KUONDOLEWA KODI INAPANDA KILA KUKICHA TOKA 17000 MTUNGI WA KG 12 ORYX MWAKA JANA HADI 24000.GUNIA LA MKAA DEC 2005 LILIKUWA 6000 HAPA DAR MARA TU KAMPENI YA KUZUIA KUNI(mazingira) MKAA UKAPANDA HADI 25000 HUKU MKOMBOZI GESI AKIPATA NAFASI YA KUPAA BILA UDHIBITI MISHAHARA YETU TUNAIJUA VIPATO VYETU TUNAVIJUA MAISHA BORA HAYAWEZEKANIKI KWA MWENDO HUU NI UJIMA MPAKA KIAMA

na Kibati, Dar TZ, - 21.03.08 @ 09:42 | #3123

tatizo ni sisa kwenye fani za watu na ubabe wa majukwaani.
tanesco wanauwezo wa kujiendesha kama taaluma ya watu itaheshimiwa pasipo na SIASA ndani yake. ............Wewe injinia mzima kutolewa maazimio na watu hawajui hata OHMS' LAW inasemaje?????????????
Haifai cha msing tanesco wapewe nafasi yao kama professionals na utaona umeme utakua hata chini ya hapo zaidi ya tunavyojua.
Meku-Mbege
Arusha

na meku, Arusha, - 21.03.08 @ 10:40 | #3128

Sawa hizo pesa za epa ziende tanesco ili wananchi tusizidi kuumizwa kupandishiwa bili 200%. Na je hizo fedha zilizoibiwa kwenye mikataba ya TANESCO nani anarudisha? kama mikataba ilikuwa ni ya uwongo na pesa zimeliwa waliosaini hiyo mikataba ya tanesco na kukataa isivunjwe mbele ya mheshimiwa Rich,PAMOJA NA RICH mwenyewe walipe pesa zetu...

na william, mbeya, - 21.03.08 @ 09:19 | #3133

Ni kweli kama alivyosema ndugu yangu Pembe hapo juu, Wabunge wa CCM ni lazima sasa waache unafiki. Hii tabia ya wabunge kuwa wakosoaji wazuri nje ya bunge halafu bungeni ataukosoa muswada kidogo na kuunga mkono muswada kwa asilimia 100%. kwanza hizi asilimia 100% zinatoka wapi tena kama muswada unadosali. Huu ni unafiki, wakati umefika sasa wabunge wa CCM watambue kwamba CCM haina hatimiliki ya nchi hii, na hivyo hamuwezi kufanya mnavyotaka lazima msikilize Watanzania tunataka nini Watanzania hatutashiba `slogans' zenu pamoja na uzuri wake.

na amani makolo, tanzania, - 21.03.08 @ 10:26 | #3139

WaTz tufahamu kuwa hatuna serikali bali tuna kundi la wahuni, na waita hivyo kwa jinsi wanavyotuburuza,baada ya Richmond kustukiwa sasa wanabuni mbino nyingine. Kuleta makampuni binafsi ya umeme tukae tukijua huu ni mradi wao wenyewe,cha msingi ni kuiwezesha TANESCO kifedha na uwezo hupo.Isipokuwa hawa wahuni wanafanya hila tu za kifisadi,kwahiyo nawasihi Wabunge wote endeleeni kukaza uzi kuwabana hawa majangiri wanaolimaliza Taifa letu. Mungu Ibariki Tz.

na Chacha Kyara., Maputo Moz., - 21.03.08 @ 10:42 | #3141

yaani shida zote hizi tunazopata ni kwasababu ya mwanasheria mkuu aliyepita ANDREW CHENGE,ameliingiza taifa kwenye mikataba mibovu huku yeye akijinufaisha na familia yake,huyu jamaa ananyumba si chini ya 7 hapa dar na marekani anazo 2,mm naishi karibu na watoto wake yaani maisha wanayoishi huku ni kumkufuru mungu kabisa,huyu anatakiwa afungwe kabisa

na denis,h, albany.NY, - 21.03.08 @ 10:50 | #3143

Tatizo hasa ni nini kwetu sisi watanzania ?
Inabidi tuamke sasa (WAKATI UMEFIKA WA KILA MTAANZANIA POPOTE ALIPO MWENYE TAALUMA YA KILE KINACHOAMULIWA KINACHOHUSU MASLAHI YA TAIFA NA AMBACHO ANA UTAALAMU WAKE,ATOHE MAONE YAKE KWA KINA NA KWA UTAALAMU WAKE WA HALI YA JUU KATIKA MADA HUSIKA)
Vinginevyo tutaishia kutolewa maamuzi na watu ambao hata hawana taaluma ya wanacho kitoleamaamuzi
Mifano tunayo Mingi e:g( Wewe ni mtaalamu wa umeme kitaaluma unaenda kukubali maamuzi ya mtu ambaye hata hajui kutumia Volt meter ? si unaweza ukaunguza nyumba jamani ?, Wewe ni Daktari kitaaluma umemaliza Degree yako hapo Muhimbili hospital
Unaenda kufanyiwa usairi na mtu ambaye hajui hata sindano inachomwa vipi ili unze kazi,
kisa tu yuko kwenye siasa .
Haiwezekani maamuzi mazito yanayo husu maslahi ya taifa yakaachwa kufanya na watu wachechate tena ndani yake unaweza kukuta mtu hana utaalamu kabisa wa anacho kitolea maamizi kwa maslahi ya taifa,Pia naomba wabunge msikubali kila linaloletwa kwenu bila kukifanyia tathmini ya kina

Mzee John

na Mzee John, UK, - 21.03.08 @ 11:28 | #3145

Walaaniwe wote wanotaka kuiua TANESCO YETU. Tanesco tunakupenda sana, maoni yoyote yale against you yakwe ni ya viongozi au wapambe nuksi ni ya mafisadi, the majority tupo nanyi. Asanteni wabunge, teteeni kuifufua Tanesco. Akina Richmonduli wenye kampuni za mifukoni wamewezeshwa na viongozi wetu, kwa nini leo na utajiri tuliobarikiwa nao TANESCO yetu isiwezeshwe???????

na gwamaka - 21.03.08 @ 12:51 | #3153

Ni upuuzi kuleta mswada ambao waziri hajausoma kinaganaga. Hivi c mlisoma kwa kodi za watanzania? Hiyo ndo dhamana tuliyowapa. Nashauri km kuna kiongozi anajiona ni **** c aachie ngazi?! MNAMTESA RAIS NYINYI.aaa haya bwn. Msipojipanga hii mi5 mmelamba galasa na kesho tu ni uchaguzi mwingine. JK, uko baharini na dhoruba ndo hiyo,magunia yaso msaada yatupe uokoe chombo na watu wako. Noti za E PA tafadhal

na kulata, tz, - 21.03.08 @ 14:36 | #3156

nilishangaa sana wabunge walivyosema muda haujafika wa kusuruhu seria ya makampuni binafsi katika sekta yaumeme,cha muhimu waheshimiwa walitakiwa walalamikie mapungufu yaliyoko kwenye sheria na yarekebishwe,sio kusema taneso iwezeshe then ibakie peke yake kuhudimia watanzania,tanesco kuna matatizo mengi,sidhani kama wakipewa hizo pesa ndo itakuwa mwisho wa matatizo ya umeme tanzaia,pengine hizo hela zikaishia kwa mafisadi vile vile,nadhani cha muhimu ni kuiwezesha tanesco na kuruhusu masirika binafsi wawekeze sekta ya umeme,ili kuipa changamoto tanesco,kuna watanzania tangu uhuru hawajawahi kutumia umeme,tukiwaachie tanesco peke yako mambo yatakuwa yakuputa taarifa tu kuwa mwaka huu imeongezeka5 ya wanaopata umeme,na tatizo libakaki aple pale,alafu nimeanza kuwa na wasi wasi na wabunge wengi,maana saa hivi kila atakacho pinga dr sla na wao wanafata tu,au ndo mnataka kuonesha wananchi kuwa nyie ndo mnafanya kazi kuliko wapinzani,nadhani kwa sasa tuangalie elimu za waheshimiwa kabla hawajaingia buneni,maana mwanzo walikuwa wao kila inachosema ccm ndio sawa,baada ya kufunguliwa macho na kasheshe la balali wamekuwa kila kitu wanapinga,dr slaa anajua nini anasema,anpinda kwa hoja na ushaidi,mama kilango make sure unakijua unachokiongea kabla ya kukuiruka kusema.n hayo tu

na john tz - 21.03.08 @ 17:46 | #3174
 
Wabunge: Fedha za EPA ziende TANESCO

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

BAADHI ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wameitaka serikali kuligawia Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) fedha za akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) zinazorejeshwa na mafisadi waliochota fedha hizo kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Walisema ili waridhike na urejeshwaji huo ni vema TANESCO ikapewa fedha hizo, ili kuboresha miundombinu yake itakayoiwezesha kutoa umeme wa uhakika mpaka maeneo ya vijijini.

Walisema hayo kwenye semina ya majadiliano ya muswada wa sheria za umeme na biashara ya mafuta ya petroli inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni kwenye mkutano ujao wa 11 unaotarajiwa kuanza Aprili 8 mjini Dodoma.

Akizungumzia hilo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Benson Mpesya, alisema hivi sasa TANESCO imekuwa tegemezi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuhimili gharama za uzalishaji umeme na badala yake wamekuwa wanunuaji wakuu wa umeme kwa kampuni binafsi.

“Fedha za EPA zinazorejeshwa tunataka wapewe TANESCO, ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa lengo la kupeleka umeme kwa watu wengi zaidi,” alisema Mpesya huku akishangiliwa na wabunge wenzake.

Naye Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, alisema kinachopaswa kufanywa na serikali hivi sasa ni kuboresha shirika hilo na si kuleta mipango ya kuruhusu wawekezaji katika sekta ya umeme, ili kushindana na TANESCO.

Alisema tatizo la TANESCO linajulikana wazi kuwa ni mzigo mkubwa wa kuzilipa kampuni zinazozalisha umeme baada ya viongozi wa serikali kuingia mikataba mibovu kwa masilahi binafsi.

“Kama pesa ipo, wapewe TANESCO si kuanza kuja na mipango ambayo ni kiini macho na ina lengo la kuwapa ulaji zaidi hao wawekezaji na kuiumiza TANESCO,” alisema Kimaro.

Aidha, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema tatizo lililopo nchini ni kuwa wanatafutwa wawekezaji walalahoi na kupewa zabuni kubwa ilimradi fedha za walipa kodi zitumike.

“Sasa ni wakati wa kuwapa fedha zetu TANESCO na wala si wawekezaji wa kigeni ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliotufikisha hapa tulipo,” alisema Mwakyembe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Mbunge wa Njombe Kusini, Anne Makinda, alisema muswada wa sheria ya umeme na biashara ya mafuta ya petroli kwa kiasi kikubwa haukupata baraka za wadau, kwani una mapungufu mengi na haonyeshi kama una nia ya dhati ya kuilinda TANESCO.

“Huu muswada haujapitia kwenye taasisi zenu na wadau wengine, kwani una kasoro nyingi na nina wasiwasi kama mtaweza kuhimili vishindo vya wabunge,” alisema Makinda ambaye pia ni Naibu Spika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shelukindo, alisema tatizo la serikali ni kukalia ushauri wa wabunge ambao huonya juu ya jambo na kuitaka serikali isilifanye.

Alisema matokeo ya kukalia ushauri wa wabunge, ni kulifanya taifa lijikute likiingia katika matatizo makubwa, hasa kiuchumi na hata kuingia mikataba mibovu.

“Sisi tunapotoa ushauri huwa hatutoi kwa chuki kwa mtu Fulani, bali tuna nia ya kulijenga taifa, lakini kwa wenzetu wa serikali inaonekana labda tumeutoa kwa sababu ya chuki,” alisema Shelukindo.

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na naibu wake, Adamu Malima, waliwaahidi kuyafanyia kazi mawazo hayo kwa masilahi ya taifa.

Malima alisema hakuna sababu kwa wabunge kuogopa miswada hiyo, kwani haina kitu kipya, kwa sababu taratibu za kununua umeme kutoka mashirika binafsi unafanyika, ila si kwa sheria zilizowekwa wazi, hivyo ni vema kukawepo sheria hizo.

“Kuna taratibu zinazofanyika katika sekta ya umeme na tunachohitaji hivi sasa ni kuweka sheria, ili kuweza kubana maeneo yenye utata,” alisema Malima.

Aidha, Ngeleja alisema serikali imetenga sh bilioni 79 kuhakikisha umeme unafika vijijini na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi.

“Tunajitahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kuboresha sekta ya nishati na hivi sasa tumeelekeza nguvu zetu kupeleka umeme vijijini,” alisema Ngeleja.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, aliionya serikali isijaribu kuacha kuwa msimamizi mkuu wa kutoa umeme.

Alisema kama serikali itafanya hivyo kuna hatari baadhi ya mikoa nchini kukosa huduma za umeme, kwani wawekzaji hupenda kuangalia maeneo fulani na kwa lengo la kutengeneza faida.

“Tuseme ukweli, hivi ni mwekezaji gani ambaye atakwenda kuwekeza sehemu ambazo anajua hatapata faida, hasa katika mikoa ya kusini au ya pembezoni mwa nchi?” alihoji Dk. Rashid.

Alisema Watanzania wamekuwa wakifanya mambo kwa makosa, hasa kwenye nishati ya umeme, hivyo ni vema hivi sasa wakawa makini, ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari ya kutokea kwa mgawo wa umeme kutokana na uhaba wa maji mwaka huu.

Muswada wa Sheria ya umeme na biashara ya mafuta ya petroli, ambao una lengo la kutoa fursa kwa kampuni nyingine kuzalisha umeme na kusambaza kwa kiasi kikubwa, unaelekea kugonga mwamba kutokana na asilimia kubwa ya wabunge kutouunga mkono.

Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 21 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
hizi hela zipo kweli jamani au hilo ni changa tuu

na k - 20.03.08 @ 22:17 | #3104

hizo hela ni changa

na k - 20.03.08 @ 22:18 | #3105

NDUGU WABUNGE KAMWE MSIKUBALI HUO MUSWADA UPITE BUNGENI HUKO BUNGENI.. ILA MIMI NAPENDA KUWAAMBI UKWELI NANYI WABUNGE WETU MKIWA NJE MWAONGE VIZURI SANA NA KWA MASLAHI YA TAIFA KWELI ILA MKIINGIA HAPO BUNGENI MTATOA KASORO NA MAPUNGUFU YOTE YAMISWAADA NA HOJA MBALIMBALI THEN AT THE END UTASIKIA MBUNGE ANASEMA NAUNGA MKONO HOJA 100% SASA KWA NINI UUNGE MKONO MSWADA MBOVU? UKATAE ILI UKAFANYIWE MAREKEBISHO MLIOYASUGGEST THEN UKIKAMILIKA NDO MUUNGE MKONO,,,BUT NAWAPONGEZA SIKUHIZI KIDIGO MNABADILIKA NA KUACHANA NA UNAFIKI HUO NAWAOMBA MUACHANENAO KABISA UNAFIKIAHUO NA MLINDE NA KUYATETEA MASKAHI YA NCHI KIKWELI

na PEMBE, Italy, - 21.03.08 @ 02:20 | #3106

WABUNGE WA TANZANIA HONGERENI SANA. MWENYEZI MUNGU AWABARIKI SANA. MLIKUWA WAPI MIAKA YOTE HII?? HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA, WATU WAWE MAKINI KWA MASLAHI YA TAIFA. TUKATAE KUFANWA WAJINGA KILA WAKATI NA WATU WABINAFSI WACHACHE AMBAO HAWANA NIA KABISA YA KULETA MAENDELEO YA NCHI. you will make a good legacy if you will save this nation from collapse!!!

na Peter, US, - 21.03.08 @ 02:52 | #3107

HIVI SELIKALI YA CCM MNAMATATIZO GANI, YAANI NYIE KILA KUKICHA MWAPIGANIA TU KUYALETA MAKAMPUNI YA WAZUNGU HAPA NCHINI HIVI WAZUNGU WAMEWALISHA NINI ETI NYIE AU MMELISHWA LIMBWATA AU WAMEWACHEZEA AKILI THEN WANANCHI TWABAKI KUWALAUMU KUMBE MUWAGONJWA TAYARI,,,MWAJUA FIKA TANESCO HAPO ILIPO NI MATOKEO YA HIZOHIZO KAMPUNI ZA KIGENI THEN BADO MNATAKA KUZITUNGIA HADI SHERIA,,WHAT ARE U DOING U GUYS OF CCM..
OKAY SASA U NGELEJA NA WATAALAMU WAKO WOOTE YAANI MLIKAA NAKUANDAA HUO MUSWADA MKAUONA KABISA IS PROFFITABLE KWA TAIFA UA? YAANI MNAFANYA MAMBO KAMA VILE MNATEGESHA DILI ILI TUKIJICHANAGANYA TU BABA AKE TUMELIWA... MIMI NAWASIWASI SANA HATA HII MISWADA MTAKUA MNAANDALIWA NA HAO HAO WAZUNGU THEN NYIE MNAWASILISHA TU BUNGENI BILA KUJUA KILICHOPO HASA NDANI,,JUST IMAGINE MUSWADA UNASAHIHI YA MTU BAKI(karamagi)
NA SIO WAZIRI NGELEJA SASA HIVI TUKIKUITA NGELEJA NA HAO WENZAKO WENDAWAZIMU TUTAKUA TUNAKUONEA ,,HAHAHA THIS IS FUNNY,,,,MIMI NAOMBA WATZ WENZANGU TUFUATILIE HASAANAYEANDAA HII MISWADA, HAPA MIMI NIMESHTUKA SI WIZARA ZETU JAMANI,,,
MAONI YANGU..
1.NAOMBA MISWADA YOTE IWE INASAMBAZWA KWENYE MEDIA LIKE NEWSPAPPERS ILI WANANCHI TUIPITE NA KUTOA MAONI YETU KABLA HAIJA PELEKWA BUNGENI,,,MAANA NAONA TULIO WATRUST KULINDA MASLAHI YA TAIFA LETU NDO WAMEKUA MA-AGENT WA KUYAIBA.
2.SERA YA UBINAFSISHAJI NI NZURI BUT SIO KIWENDA WAZIMU KAMA CCM MNAVYOFANYA HATA HAO MABWANA ZENU WAZUNGU HAWABINAFSISHI HADI SEKTA NYETI ZA JAMII,,,MAANA NAONA SASA SIAJABU KESHO MKAPELEKA MUSWADA WA KUBINAFSISHA JWTZ...
3.TANESCO IMEIOMBA SERIKALI TRILLION 1.6,IT MEANS IMEPUNGUKIWA HELA ZAKUJIENDESHA SASA TUUZIENI HISA WANANCHI ZIZIDIZO 50% ILI TUONGEZE MTAJI KWA TANESCO YETU NA TUIENDESHE WENYEWE KULIKO KUKIMBILIA LETA MABWANA ZETU WAZUNGU HAPA NCHINI KWETU.
,,,,TANESCO IS NOT FOR COMMERCIAL BUT FOR PUBLIC SERVICE,,,

na PEMBE, Italy, - 21.03.08 @ 03:00 | #3109

Tatizo kubwa la nchi ni kukosa viongozi wenye uzalendo kwa maana viongozi wataoweka mbele maslahi ya taifa mbele na siyo maslahi ya mtu binafsi. kwa mfano ktk swala zima la uwekezaji tulichokuwa tunahtaji siyo mtaji isipokuwa ni utahalamu na vitendea kazi na siyo mtaji kama wanavyodai viongozi hawa uchwara. watanzania wenyewe wangeuziwa hisa asilimia 60% ili kampuni au shirika liwe bado mikononi mwa watanzania wenyewe na siyo serikali. WAtanZANIA wenyewe ndio wakae chini na wawekenzaji wa nje na kuangalia namna ya kuendesha kampuni. Wenye hisa kubwa ambao ni Wantanzania wenyewe wasingeweza kukubali upumbavu unaofanyika hivi sasa wa kuwaachia wageni wafaidike na wao kuambulia patupu. kama unahitaji milioi 500, uza shea millioni moja kila shea shillingi mia tano. ni asilimia kubwa ya watanzania wanao uwezo wa kununua na shea kwa shillingi mia tano. dhumuni likiwa kuwajengea watanzania nafasi ya kuweza kufaidika wao moja moja ili waweze kuboresha maisha yao na familia zao badala ya kuinufaisha serikali ambapo pesa zote zinaishia mikononi mwa wachache. Moja kati sharti la uwekezaji ni kuajiri watanznaia na kama hakuna mtanznaia mwenye utaalamu huo basi mwekezaji atawajibika kutumia mtaalam kutoka nje na wakati huo huo mwekezaji atatakiwa kupewa muda maalum wa kutumia mtaalamu wa nje ili kutoa nafasi kwa mtanzania kuwatrained ili kuchukua nafasi ya mtaalam wa nje mara muda wake utakapokwisha. Watanzania tukitaka maendeleo ya kweli ni lazima tuweke mbele utaifa wetu kwa kuweka mbele kwanza Watanzania na raia wageni kufuata baadaye kwani tusijidangaye watanzania ukienda kwa watu weupe kazi uwapa watu wao kwanza na siyo kuwaacha raia wao na kuwapa wageni hakuna upumbavu kama huo nchi nyingi zilizoendelea. lakini rushwa imeturudisha nyuma sana inawafanya Viongozi wengi kuwa kama vipofu wasioona na kukubali masharti yanayotolewa na mgeni badala ya mwenye nyumba kuwa sauti mgeni ndio anakupangia masharti hii aiwezekani kabisa watanzania. watanzania tumekosa viongozi wenye uchungu na nchi mfano waziri mkuu Lowassa alitusaliti watanzania wenzake kwa kutulaza gizani miezi kadhaa kwa uroho wake wa fedha hii inatia uchungu sana.

na nick, Tanzania, - 21.03.08 @ 04:54 | #3110

Mimi nadhani there is something wrong somewhere in our minds/brain!! Why katika kutafuta suluhisho ya mambo yanayotushinda kuendesha (kutokana na uzembe/ubinafsi wetu) basi the simple and quick solution ni KUBINAFSISHA, tena kwa STRANGERS, WHHY? Hivi ni kweli kwamba WE CAN'T THINK OF SOME OTHER BETTER SOLUTIONS zaidi ya huo ubinafsishaji?? Inakera sana, hao waliopo madarakani ndo waamuzi wa maisha ya waTZ woooote sisi hata na ya vizazi vijavyo? Manake hapo utackia mikataba hiyo ni kuanzia 10-15yrs!! Sijui, ila it has to reach a point now na sisi tuanze kuwa na our own ways of solving our own problems, hizi sera za ubinafsishaji ni mbinu za wenzetu kujipatia ajira kwenye nchi za wengine/wajinga kwani kwao ajira hamna, so ni ubunifu wao katika kusaka ajira za watu na makampuni yao. Ipo siku utasikia kuwa eti, SERIKALI YA TZ IMESHINDWA KUJIENDESHA,suluhisho ni AJE MWEKEZAJI(tena wa nje) KUIENDESHA! mi cjui, huenda ikatokea kutokana na style iliopo TZ! Ahsanteni.

na Farry, Tanzania, - 21.03.08 @ 08:20 | #3113

Mimi nadhani there is something wrong somewhere in our minds/brain!! Why katika kutafuta suluhisho ya mambo yanayotushinda kuendesha (kutokana na uzembe/ubinafsi wetu) basi the simple and quick solution ni KUBINAFSISHA, tena kwa STRANGERS, WHHY? Hivi ni kweli kwamba WE CAN'T THINK OF SOME OTHER BETTER SOLUTIONS zaidi ya huo ubinafsishaji?? Inakera sana, hao waliopo madarakani ndo waamuzi wa maisha ya waTZ woooote sisi hata na ya vizazi vijavyo? Manake hapo utackia mikataba hiyo ni kuanzia 10-15yrs!! Sijui, ila it has to reach a point now na sisi tuanze kuwa na our own ways of solving our own problems, hizi sera za ubinafsishaji ni mbinu za wenzetu kujipatia ajira kwenye nchi za wengine/wajinga kwani kwao ajira hamna, so ni ubunifu wao katika kusaka ajira za watu na makampuni yao. Ipo siku utasikia kuwa eti, SERIKALI YA TZ IMESHINDWA KUJIENDESHA,suluhisho ni AJE MWEKEZAJI(tena wa nje) KUIENDESHA! mi cjui, huenda ikatokea kutokana na style iliopo TZ! Ahsanteni.

na Farry, Tanzania, - 21.03.08 @ 08:21 | #3114

Mimi nadhani there is something wrong somewhere in our minds/brain!! Why katika kutafuta suluhisho ya mambo yanayotushinda kuendesha (kutokana na uzembe/ubinafsi wetu) basi the simple and quick solution ni KUBINAFSISHA, tena kwa STRANGERS, WHHY? Hivi ni kweli kwamba WE CAN'T THINK OF SOME OTHER BETTER SOLUTIONS zaidi ya huo ubinafsishaji?? Inakera sana, hao waliopo madarakani ndo waamuzi wa maisha ya waTZ woooote sisi hata na ya vizazi vijavyo? Manake hapo utackia mikataba hiyo ni kuanzia 10-15yrs!! Sijui, ila it has to reach a point now na sisi tuanze kuwa na our own ways of solving our own problems, hizi sera za ubinafsishaji ni mbinu za wenzetu kujipatia ajira kwenye nchi za wengine/wajinga kwani kwao ajira hamna, so ni ubunifu wao katika kusaka ajira za watu na makampuni yao. Ipo siku utasikia kuwa eti, SERIKALI YA TZ IMESHINDWA KUJIENDESHA,suluhisho ni AJE MWEKEZAJI(tena wa nje) KUIENDESHA! mi cjui, huenda ikatokea kutokana na style iliopo TZ! Ahsanteni.

na Farry, Tanzania, - 21.03.08 @ 08:29 | #3115

Mimi nadhani there is something wrong somewhere in our minds/brain!! Why katika kutafuta suluhisho ya mambo yanayotushinda kuendesha (kutokana na uzembe/ubinafsi wetu) basi the simple and quick solution ni KUBINAFSISHA, tena kwa STRANGERS, WHHY? Hivi ni kweli kwamba WE CAN'T THINK OF SOME OTHER BETTER SOLUTIONS zaidi ya huo ubinafsishaji?? Inakera sana, hao waliopo madarakani ndo waamuzi wa maisha ya waTZ woooote sisi hata na ya vizazi vijavyo? Manake hapo utackia mikataba hiyo ni kuanzia 10-15yrs!! Sijui, ila it has to reach a point now na sisi tuanze kuwa na our own ways of solving our own problems, hizi sera za ubinafsishaji ni mbinu za wenzetu kujipatia ajira kwenye nchi za wengine/wajinga kwani kwao ajira hamna, so ni ubunifu wao katika kusaka ajira za watu na makampuni yao. Ipo siku utasikia kuwa eti, SERIKALI YA TZ IMESHINDWA KUJIENDESHA,suluhisho ni AJE MWEKEZAJI(tena wa nje) KUIENDESHA! mi cjui, huenda ikatokea kutokana na style iliopo TZ! Ahsanteni.

na Farry, Tanzania, - 21.03.08 @ 08:34 | #3116

Kwa kweli wabunge mkiendelea hivyo bila shaka Tanzania ya asali na maziwa inawezekana. Hongera zangu kwenu kwa muda

na Quara, Mwanza, - 21.03.08 @ 09:11 | #3118

TANESCO WANA MIUNDOMBINU YA KUTOSHA KINACHOWAKWAZA NI MZIGO WA MADENI AMBAYO YAMETOKANA NA MIKATABA MIBOVU ILIYOKWISHA ONEKANA KWAMBA INAWEZA KUVUNJWA BILA MADHARA YEYOTE KWANINI HAIJAVUNJWA MPAKA SASA?HIZO PESA ZA EPA ZIJENGWE DARAJA LA KIGAMBONI WATANZANIA TUACHANE NA SQUARTERS NA UVUNJAJI HUKO MBELENI TUANZE KUPUNGUZA CONGESTION YA MAGARI HUKU TUKIKUZA UTALII.TUKIBINAFSISHA SEKTA HII NYETI WATANZANIA TUTAENDELEA KUPIKIA KUNI KWANI HATA GESI LICHA YA KUONDOLEWA KODI INAPANDA KILA KUKICHA TOKA 17000 MTUNGI WA KG 12 ORYX MWAKA JANA HADI 24000.GUNIA LA MKAA DEC 2005 LILIKUWA 6000 HAPA DAR MARA TU KAMPENI YA KUZUIA KUNI(mazingira) MKAA UKAPANDA HADI 25000 HUKU MKOMBOZI GESI AKIPATA NAFASI YA KUPAA BILA UDHIBITI MISHAHARA YETU TUNAIJUA VIPATO VYETU TUNAVIJUA MAISHA BORA HAYAWEZEKANIKI KWA MWENDO HUU NI UJIMA MPAKA KIAMA

na Kibati, Dar TZ, - 21.03.08 @ 09:42 | #3123

tatizo ni sisa kwenye fani za watu na ubabe wa majukwaani.
tanesco wanauwezo wa kujiendesha kama taaluma ya watu itaheshimiwa pasipo na SIASA ndani yake. ............Wewe injinia mzima kutolewa maazimio na watu hawajui hata OHMS' LAW inasemaje?????????????
Haifai cha msing tanesco wapewe nafasi yao kama professionals na utaona umeme utakua hata chini ya hapo zaidi ya tunavyojua.
Meku-Mbege
Arusha

na meku, Arusha, - 21.03.08 @ 10:40 | #3128

Sawa hizo pesa za epa ziende tanesco ili wananchi tusizidi kuumizwa kupandishiwa bili 200%. Na je hizo fedha zilizoibiwa kwenye mikataba ya TANESCO nani anarudisha? kama mikataba ilikuwa ni ya uwongo na pesa zimeliwa waliosaini hiyo mikataba ya tanesco na kukataa isivunjwe mbele ya mheshimiwa Rich,PAMOJA NA RICH mwenyewe walipe pesa zetu...

na william, mbeya, - 21.03.08 @ 09:19 | #3133

Ni kweli kama alivyosema ndugu yangu Pembe hapo juu, Wabunge wa CCM ni lazima sasa waache unafiki. Hii tabia ya wabunge kuwa wakosoaji wazuri nje ya bunge halafu bungeni ataukosoa muswada kidogo na kuunga mkono muswada kwa asilimia 100%. kwanza hizi asilimia 100% zinatoka wapi tena kama muswada unadosali. Huu ni unafiki, wakati umefika sasa wabunge wa CCM watambue kwamba CCM haina hatimiliki ya nchi hii, na hivyo hamuwezi kufanya mnavyotaka lazima msikilize Watanzania tunataka nini Watanzania hatutashiba `slogans' zenu pamoja na uzuri wake.

na amani makolo, tanzania, - 21.03.08 @ 10:26 | #3139

WaTz tufahamu kuwa hatuna serikali bali tuna kundi la wahuni, na waita hivyo kwa jinsi wanavyotuburuza,baada ya Richmond kustukiwa sasa wanabuni mbino nyingine. Kuleta makampuni binafsi ya umeme tukae tukijua huu ni mradi wao wenyewe,cha msingi ni kuiwezesha TANESCO kifedha na uwezo hupo.Isipokuwa hawa wahuni wanafanya hila tu za kifisadi,kwahiyo nawasihi Wabunge wote endeleeni kukaza uzi kuwabana hawa majangiri wanaolimaliza Taifa letu. Mungu Ibariki Tz.

na Chacha Kyara., Maputo Moz., - 21.03.08 @ 10:42 | #3141

yaani shida zote hizi tunazopata ni kwasababu ya mwanasheria mkuu aliyepita ANDREW CHENGE,ameliingiza taifa kwenye mikataba mibovu huku yeye akijinufaisha na familia yake,huyu jamaa ananyumba si chini ya 7 hapa dar na marekani anazo 2,mm naishi karibu na watoto wake yaani maisha wanayoishi huku ni kumkufuru mungu kabisa,huyu anatakiwa afungwe kabisa

na denis,h, albany.NY, - 21.03.08 @ 10:50 | #3143

Tatizo hasa ni nini kwetu sisi watanzania ?
Inabidi tuamke sasa (WAKATI UMEFIKA WA KILA MTAANZANIA POPOTE ALIPO MWENYE TAALUMA YA KILE KINACHOAMULIWA KINACHOHUSU MASLAHI YA TAIFA NA AMBACHO ANA UTAALAMU WAKE,ATOHE MAONE YAKE KWA KINA NA KWA UTAALAMU WAKE WA HALI YA JUU KATIKA MADA HUSIKA)
Vinginevyo tutaishia kutolewa maamuzi na watu ambao hata hawana taaluma ya wanacho kitoleamaamuzi
Mifano tunayo Mingi e:g( Wewe ni mtaalamu wa umeme kitaaluma unaenda kukubali maamuzi ya mtu ambaye hata hajui kutumia Volt meter ? si unaweza ukaunguza nyumba jamani ?, Wewe ni Daktari kitaaluma umemaliza Degree yako hapo Muhimbili hospital
Unaenda kufanyiwa usairi na mtu ambaye hajui hata sindano inachomwa vipi ili unze kazi,
kisa tu yuko kwenye siasa .
Haiwezekani maamuzi mazito yanayo husu maslahi ya taifa yakaachwa kufanya na watu wachechate tena ndani yake unaweza kukuta mtu hana utaalamu kabisa wa anacho kitolea maamizi kwa maslahi ya taifa,Pia naomba wabunge msikubali kila linaloletwa kwenu bila kukifanyia tathmini ya kina

Mzee John

na Mzee John, UK, - 21.03.08 @ 11:28 | #3145

Walaaniwe wote wanotaka kuiua TANESCO YETU. Tanesco tunakupenda sana, maoni yoyote yale against you yakwe ni ya viongozi au wapambe nuksi ni ya mafisadi, the majority tupo nanyi. Asanteni wabunge, teteeni kuifufua Tanesco. Akina Richmonduli wenye kampuni za mifukoni wamewezeshwa na viongozi wetu, kwa nini leo na utajiri tuliobarikiwa nao TANESCO yetu isiwezeshwe???????

na gwamaka - 21.03.08 @ 12:51 | #3153

Ni upuuzi kuleta mswada ambao waziri hajausoma kinaganaga. Hivi c mlisoma kwa kodi za watanzania? Hiyo ndo dhamana tuliyowapa. Nashauri km kuna kiongozi anajiona ni **** c aachie ngazi?! MNAMTESA RAIS NYINYI.aaa haya bwn. Msipojipanga hii mi5 mmelamba galasa na kesho tu ni uchaguzi mwingine. JK, uko baharini na dhoruba ndo hiyo,magunia yaso msaada yatupe uokoe chombo na watu wako. Noti za E PA tafadhal

na kulata, tz, - 21.03.08 @ 14:36 | #3156

nilishangaa sana wabunge walivyosema muda haujafika wa kusuruhu seria ya makampuni binafsi katika sekta yaumeme,cha muhimu waheshimiwa walitakiwa walalamikie mapungufu yaliyoko kwenye sheria na yarekebishwe,sio kusema taneso iwezeshe then ibakie peke yake kuhudimia watanzania,tanesco kuna matatizo mengi,sidhani kama wakipewa hizo pesa ndo itakuwa mwisho wa matatizo ya umeme tanzaia,pengine hizo hela zikaishia kwa mafisadi vile vile,nadhani cha muhimu ni kuiwezesha tanesco na kuruhusu masirika binafsi wawekeze sekta ya umeme,ili kuipa changamoto tanesco,kuna watanzania tangu uhuru hawajawahi kutumia umeme,tukiwaachie tanesco peke yako mambo yatakuwa yakuputa taarifa tu kuwa mwaka huu imeongezeka5 ya wanaopata umeme,na tatizo libakaki aple pale,alafu nimeanza kuwa na wasi wasi na wabunge wengi,maana saa hivi kila atakacho pinga dr sla na wao wanafata tu,au ndo mnataka kuonesha wananchi kuwa nyie ndo mnafanya kazi kuliko wapinzani,nadhani kwa sasa tuangalie elimu za waheshimiwa kabla hawajaingia buneni,maana mwanzo walikuwa wao kila inachosema ccm ndio sawa,baada ya kufunguliwa macho na kasheshe la balali wamekuwa kila kitu wanapinga,dr slaa anajua nini anasema,anpinda kwa hoja na ushaidi,mama kilango make sure unakijua unachokiongea kabla ya kukuiruka kusema.n hayo tu

na john tz - 21.03.08 @ 17:46 | #3174

Halafu walipwe Dowans au????
 
Back
Top Bottom