Wabunge Chadema wamtikisa Pinda bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge Chadema wamtikisa Pinda bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mallaba, Feb 11, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Wabunge Chadema wamtikisa Pinda bungeni Send to a friend Friday, 11 February 2011 00:25 0diggsdigg

  Exuper Kachenje, Dodoma
  WABUNGE wa Chadema jana walimtikisa waziri mkuu, Mizengo Pinda katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo wakimtaka kueleza serikali ina tamko gani kuhusu mauaji yaliyotokea Januari 5 mkoani Arusha.Kadhalika kikao cha tatu cha mkutano wa pili wa Bunge la kumi, jana kilishuhudia mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa mbunge wa kwanza katika bunge la kumi kuwekwa kikaangoni baada ya kupewa siku tano na Spika wa Bunge, Anne Makinda athibitishe madai yake kwamba Waziri Mkuu Pinda aliudanganya umma wa Watanzania wakati akijibu swali kuhusu vurugu za Arusha.

  Hoja ya Mbowe
  Msumari wa kwanza kwa Pinda, ulipigiliwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, baada ya kuuliza serikali inatoa tamko gani rasmi kuhusu tukio la mauaji ya watu watatu katika vurugu na maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na wahusika akiwamo IGP Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu.

  Katika swali lake la nyongeza Mbowe alitaka kujua ni lini serikali itaunda tume ya kisheria kuchunguza tukio hilo kwa kupata maelezo kutoka pande zote husika tofauti na sasa ambapo taarifa zilizopo serikalini ni zile zinazotoka upande mmoja wa jeshi la polisi.

  Majibu ya Pinda
  Hata hivyo, akijibu kombora hilo, Pinda aliinyoshea kidole Chadema akisema kwa mujibu wa maelezo aliyopewa ilivunja makubaliano yake na polisi na kuandamana.

  Pinda aliweka bayana kwamba, baada ya hali hiyo kilichotokea ni polisi kujaribu kuzuia maandamano hayo ya wanachama wa Chadema ambao tayari walikuwa wamehamasishwa na viongozi wao kwenda “kuwakomboa” wenzao waliokuwa wameshilikiwa kituo cha polisi mjini Arusha.

  "Nakushukuru Mbowe kwa kuuliza swali hilo, serikali hii ni makini, ikiwa jambo limetokea usikimbilie kusema serikali,
  serikali..., ni vizuri kuulizaa aliyesababisha...,'' alisema Pinda na kuongeza:

  ''Mlikiuka makubaliano na polisi, matamshi ya kwenye mkutano
  hayakuwa ya chama chenye dhamira ya kujenga amani, mkawataka wafuasi waende kuwakomboa wenzao."

  Katika kuondoa wingu na kuweka hadharani kila kitu, Pinda alisema pamoja na juhudi za polisi kuzuia maandamano
  hayo, lakini yaliendelea hadi mita 50 kutoka kituo cha polisi,
  nao hawakuwa njia nyingine kwa kuwa hawakujua nini kingewakuta kama waandamanaji wangevamia kituo cha
  polisi.

  "Police were left with no option' (hawakuwa na njia nyingine), ndipo watu watatu wakapoteza maisha. Kama Mbowe na Chadema mngeamua
  kushirikiana na serikali haya yasingetokea," alisema Pinda.

  Kuhusu kuunda tume ya wanasheria kuchunguza tukio hilo na kutoa alichokiita Mbowe ni ukweli na
  kuchukua hatua, Pinda alisema uchunguzi unaweza kufanyika, lakini lazima serikali ijiridhishe kwanza ndipo hilo lifanyike.

  "Ni sawa uchunguzi unaweza kufanyika, lakini lazima serikali ijiridhishe. Rai yangu tushirikiane, lazima muda wote
  tujitahidi tujenge nchi ya amani na utulivu,'' alionya Pinda.

  Uchaguzi wa Meya Arusha

  Katika hatua nyingine, Pinda alisema taratibu zilizotumika kumpata Meya wa mji wa Arusha na Naibu wake ni sahihi.

  Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalum Manyara, Martha Umbulla aliyetaka kujua pamoja na mambo mengine, msimamo wa serikali kuhusu Meya na Naibu Meya wa Arusha.

  "Sasa niseme hivi, kwa hesabu za kawaida za mtoto wa darasa la kwanza, katika uchaguzi mwenzako ana madiwani
  16 wewe una 14 utashindaje, baada ya hayo wakasema wakutane wazungumze, watazungumza nini?

  Hili ni suala la kisheria; Mimi nilikuwa Tamisemi, utaratibu uliofuatwa katika
  uchaguzi ule ni sahihi, Meya sahihi, Naibu Meya sahihi," alitoa msimamo Pinda.

  Hata hivyo, alisema pamoja na kuwepo kwa taarifa za Naibu Meya huyo wa Arusha kujitoa, lakini serikali haijapata
  barua rasmi kuhusu uamuzi huo.

  Pinda pia alisema, wabunge waliotajwa kuwa chanzo cha mvutano, aliowataja kuwa ni Chatanda wa CCM na
  Rebecca Mngodo wa Chadema ni halali.

  Lema: Pinda amedanganya
  Baada ya Pinda kumaliza maelezo yake hayo mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema aliomba mwongozo wa Spika kwa kusema "Mwongozo wa spika," akitumia kifungu cha 68.

  Lema baada ya kuomba mwongozo wa spika na kuruhusiwa alihoji; "Hatua gani zinaweza kuchukuliwa kama waziri mkuu analidanganya Bunge na umma? Naona waziri mkuu amelidanganya taifa," alisema Lema bila ya kufafanua
  alichodai kuwa ni uongo.

  Hata hivyo, kauli hiyo ilimchefua spika Makinda ambaye aling'aka akisema; "Bunge letu lina adabu lazima hiyo ifuatwe, huwezi kusema hivyo ikaishia hivi hivi tu, kama unaona waziri mkuu amedanganya basi nenda kaandike alafu ulete, maelezo yako,".

  Spika akionyesha kuchukizwa na kauli hiyo ya Lema, wakati akihitimisha kipindi hicho alimpa mbunge huyo wa Arusha mjini siku tano za kuwasilisha maelezo yake bungeni kuthibisha uongo wa waziri mkuu.

  Makinda alisema iwapo mbunge huyo atashindwa kuwasilisha uthibitisho huo, atatakiwa kujirekebisha kwa kufuta kauli yake au kuomba radhi, adhabu atakayokabiliana nayo ni
  kusimamishwa kuhudhuria vikao visivyozidi vitano vya bunge.

  Alimtaka kuthibitisha madai hayo, lakini kwa wakati Spika akitangaza hayo Lema hakuwepo ndani ya ukumbi wa Bunge.

  Hata hivyo, akizungumza na wanahabari baadaye nje ya ukumbi wa Bunge, Lema alisema : "Leo siwezi kuwathibitishia nisiharibu ushahidi, lakini nipo tayari kuthibitisha uongo huo wa waziri mkuu."

  Alifafanua kwamba," Bunge limeniambia nithibitishe, nasema waziri mkuu amedanganya na nitathibitisha hilo
  Februari 14 asubuhi, pia nitaongea nanyi (waandishi wa habari) na nitawapa uthibitisho."

  Alipoulizwa haoni kwamba pengine waziri mkuu alipewa taarifa potofu na siyo kusema uongo, Lema alisema: "Sio kwamba amepewa taarifa potofu, hilo ni lake yeye kulisema, lakini nasema waziri mkuu ameudanganya umma na nitathibitisha Februari 14."

  Spika Makinda alitoa agizo hilo kwa Lema, baada ya waziri mkuu kumalizia kujibu swali la mwisho lililoulizwa
  na Hamad Rashid wa CUF, kuhusu hali ya chakula na tishio la kupanda bei ya mafuta nchini.

  Madiwani Chadema kama wabunge wao
  Mwandishi, Moses Mashalla anaripoti kuwa sakata la uchaguzi wa umeya mkoani Arusha limeendelea kukufukuta kufuatia madiwani wa Chadema kususia kikao cha kwanza cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Arusha kwa kutoka nje ya ukumbi, kwa madai kwamba hawamtambui meya wa manispaa ya hiyo, Gaudence Lyimo.

  Hatua ya madiwani hao imekuja saa 48 tangu wabunge wa Chadema watoke nje ya bunge ikiwa ni hatua ya kupinga hatua ya kufanyiwa tafsiri maneno ‘Kambi rasmi ya upinzani bungeni’, katika kanuni za bunge toleo la mwaka 2007.

  Hatua ya madiwani hao wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wakati kikao cha kwanza cha baraza la madiwani kikiendelea kilijitokeza jana majira ya saa 8:30 mchana wakati ajenda ya kuteua kamati za kudumu za manispaa ya Arusha ikitaka kuanza.

  Kabla ya madiwani hao kutoka nje kulikuwa na mvutano na malumbano ndani ya kikao hicho baina ya madiwani wa Chadema na CCM hali iliyomlazimisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Estomihi Chang’a kutoka nje ya ukumbi ili kupisha kikao kisicho rasmi cha muafaka baina ya pande hizo, huku mkuu wa wilaya ya Arusha akihudhuria kikao hicho.

  Madiwani hao wa Chadema wakiongozwa na kiongozi wao,ambaye ni diwani wa kata ya Elerai, John Bayo walitoka nje na kuwaacha madwiani wa CCM wakiwemo watumishi wakiendelea na kikao.

  Akizungumza mara baada ya kutoka nje, Bayo alisema walichukua hatua hiyo baada ya kufikia maafikiano na uongozi wa chama chao ngazi ya taifa ya kuwa hawamtambui meya wa manispaa ya Arusha.

  “Sisi hatumtambui meya wa Arusha kwasababu alipatikana kwa njia za zisizo halali, hivyo tumetoka nje ya ukumbi kwa maafikiano ya madiwani wetu na uongozi wa taifa kuwa hatuwezi kushiriki kikao cha utekelezaji na mtu ambaye hatumtabui,"alisema Bayo.

  Bayo alisema wao walipokea taarifa za kikao hicho cha madiwani ambapo ajenda walizoambiwa kuwa ni pamoja ana kufungua kikao, kuunda kamati za kudumu za manispaa ya Arusha na kuunda ratiba ya vikao vya manispaa kwa mwaka mzima.

  Alisema walipofika katika ukumbi huo waliomba watumishi wa manispaa hiyo watoke nje ili waweze kujadili muafaka wa masuala mbalimbali baina yao na madiwani wa CCM na ndipo walipokubaliana na kisha kuzungumzia masuala mbalimbali walioafikiana baina ya pande zote mbili.

  Alidai kuwa mojawapo ya masuala ambayo walikubaliana na madiwani wa CCM ni pamoja na kuitaka serikali izikutanishe pande mbili zinazopingana ili ziweze kujadili hali ya mvutano uliopo na kutafuta suluhu.

  Hatahivyo, alisitiza kuwa mara baada ya kikao hicho walikubaliana pia kutafuta muafaka wa suluhu la utata wa umeya wa Arusha lakini baadhi ya madiwani wa CCM walipinga na kudai kuwa waendelee na ajenda zilizopo na suala hilo litafuata baadaye kitendo ambacho hawakukiafiki.

  Bayo alisema mbali na kulalamikia uchaguzi wa umeya pia walikuwa na wasiwasi na baadhi ya uundwaji wa kamati za kudumu za manispaa hiyo, kufuatia majina ya madiwani wa Chadema kuwekwa katika orodha katika baadhi ya kamati ihali hawakuomba kamati hizo.

  Kwa upande wake Meya Lyimo alisema wanashangazwa na hatua ya madiwani wa Chadema kutoka nje ya kikao hicho kwa madai ya kutotambua nafasi yake.

  Lyimo, alidai kuwa pamoja na madiwani hao kususia kikao, wao waliendelea na uundaji wa kamati za kudumu za manispaa ya Arusha kama kawaida bila kuwashirikisha madiwani wa Chadema kwa kuwa hawakuwepo na wataendelea kuchapa kazi za kuwatumikia wananchi.

  “Sisi hatukuwafukuza kwenye kikao lakini tumechagua kamati bila wao kuwepo kwa sababu hawakuwepo pia lakini tulitaka hata wao waongoze baadhi ya kamati,” alisema Lyimo.
   
 2. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnh ngoma nzito..............
   
 3. doup

  doup JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Ningependa Kituo kimojawapo cha Habari(TV au Radio) waje wamualike huyu Makinda tumuulize kama anajua maana ya neno ADABU, mpinzani anapohoji "Hatua gani zinaweza kuchukuliwa kama waziri mkuu analidanganya Bunge na umma? Naona waziri mkuu amelidanganya taifa," anaonekana hana adabu, wakati yeye mwenyewe (alisikika kwa sauti yake) na wabunge wa chama chake anasahahu jinsi alipoligeuza bunge sehemu ya mipasho; kwa kutoa maneno machafu na kejeli kwa wabunge wa CDM huku taifa likushuhudia. Nani hana adabu hapa.
   
 4. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  moja wapo ya mambo ambayo waziri mkuu angayaweka sawa ni kuthibitisha kama kweli waliouwawa walikuwa wakielekea kituo cha polisi, maana taarifa ni kwamba waliouwawa walikukumbana na vifo vyao mbali kabisa na kituo cha polisi. Baadhi wala hawakuwa miongoni mwa waandamanaji. Inabidi athitishe kwamba waliuwawa kati ya mita hizo 50 kutoka kituo cha polisi kama anavyodai. Kama waliuwawa sehemu tofauti na hiyo atueleze ni vipi anadai polisi waliachwa bila option nyingine zaidi ya kuua.
   
 5. m

  makongorosi Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sifa ya kwanza ili kuwa mwana ccm lazima uwe muongo, pili uwe fisadi. pinda amefuzu uongo sasa anaelekea kwenye ufisadi.
   
 6. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Tusitarajie majibu mazuri kwa wauaji hata siku moja,pinda ni familia moja na ccm na utawala uliopo kwa hiyo haoni thamani yoyote ya waandamanaji wilouawa kupinga ccm na na utawala wake hata wangekufa mia kwake sawa tu.Tuache woga watanzani tudai haki yetu milee.
   
Loading...