Wabunge CHADEMA kuanza ziara

Wabunge CHADEMA kuanza ziara

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Ziwa Mashariki, wanatarajiwa kuanza ziara katika mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga, kwa ajili ya kuimarisha chama na kuwaeleza wananchi sababu za kutokea vurugu bungeni.

Akizungumza juzi na Tanzania Daima, mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, alisema kuwa ziara hiyo itakuwa na ajenda nne muhimu.

Alizitaja ajenda za ziara ya operesheni hiyo kuwa ni kuwaeleza wananchi sababu ya vurugu zilizotokea hivi karibuni bungeni, mambo ya Katiba mpya, kujenga na kuimarisha chama na kuzungumzia kilimo cha pamba.

Alisema katika ziara hiyo itakayoanzia Musoma mkoani mkoani Mara na baadaye kwenye majimbo mengine ya mikoa hiyo, pia watazungumzia hali ya maendeleo, umaskini na changamoto zilizopo tangu uhuru mwaka 1961.

"Tunakwenda kuwaambia wananchi kuhusu kilimo cha pamba na changamoto zake, kujenga na kuimarisha chama chetu. Kwa hiyo naomba sana wajitokeze kwa wingi watuunge mkono katika harakati zetu," alisema Nyerere.

Alisema kuwa wabunge wengine watakaokuwa kwenye oparesheni hiyo ni Meshack Opulukwa (Meatu), Silvester Kasulumbayi (Maswa Mashariki), Ester Matiku (Viti Maalum Mara) na John Shibuda (Maswa Magharibi).

Nyerere alisema kivumbi cha ziara hiyo kitaanza hivi karibuni mara baada ya taratibu za kichama kukamilika na kuwaomba wanachama wote wa CHADEMA wenye nia ya kugombea nafasi yoyote kupitia chama hicho nao kujitokeze kwa wingi.
 
Naipenda hiyo , ifikapo 2015 wananchi watajua kuchambua mbivu na mbichi, siku hizi sisikii kabisa ule wimbo wa ccm No. 1,
 
Itabidi KINANA na NAPE warudie tena ziara yao,hii ya sasa imekua kazi bure
 
Watasuthubutu kuimbia nambari wani ni ccm ,wajaribu waone kitu watanzania watawafanya 2015 mbali sana tunawaonesha 2014 kwenye chaguzi za serikali za mitaa
 
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Ziwa Mashariki, wanatarajiwa kuanza ziara katika mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga, kwa ajili ya kuimarisha chama na kuwaeleza wananchi sababu za kutokea vurugu bungeni.

Akizungumza juzi na Tanzania Daima, mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, alisema kuwa ziara hiyo itakuwa na ajenda nne muhimu.

Alizitaja ajenda za ziara ya operesheni hiyo kuwa ni kuwaeleza wananchi sababu ya vurugu zilizotokea hivi karibuni bungeni, mambo ya Katiba mpya, kujenga na kuimarisha chama na kuzungumzia kilimo cha pamba.

Alisema katika ziara hiyo itakayoanzia Musoma mkoani mkoani Mara na baadaye kwenye majimbo mengine ya mikoa hiyo, pia watazungumzia hali ya maendeleo, umaskini na changamoto zilizopo tangu uhuru mwaka 1961.

"Tunakwenda kuwaambia wananchi kuhusu kilimo cha pamba na changamoto zake, kujenga na kuimarisha chama chetu. Kwa hiyo naomba sana wajitokeze kwa wingi watuunge mkono katika harakati zetu," alisema Nyerere.

Alisema kuwa wabunge wengine watakaokuwa kwenye oparesheni hiyo ni Meshack Opulukwa (Meatu), Silvester Kasulumbayi (Maswa Mashariki), Ester Matiku (Viti Maalum Mara) na John Shibuda (Maswa Magharibi).

Nyerere alisema kivumbi cha ziara hiyo kitaanza hivi karibuni mara baada ya taratibu za kichama kukamilika na kuwaomba wanachama wote wa CHADEMA wenye nia ya kugombea nafasi yoyote kupitia chama hicho nao kujitokeze kwa wingi.
Nakumbuka Wabunge wote wa CHADEMA akiwepo na Babu Slaa walizunguka nchi nzima kudai serikali za majimbo,naona wameeacha hiyo sasa wana dai serikali tatu na sasa wanazunguka nchi nzima kutetea hoja kuwa SUGU alikua sahihi kumpiga yule Polisi....baada ya hili sijui kutakua na mzunguko wa kupinga matokeo ya Urais 2015! Wazee wa kuzunguka Nchi nzimaaaaa!
 
Ni wazo zuri na naunga mkono ziara hiyo kwani inafanyika wakati muafaka kwani itakuwa counter attack nzuri kwa Nape na Mwenzie Kinana na hivyo kuzima kabisa propaganda zao kwani watanzania wa sasa wanachotaka ni kuambiwa ukweli na sio propaganda kama za ...oooh ...'Dr. slaa kamnyan'ganya mtu mwanamke' halafu mnaingia mitini - kipindi hiki . Ila ninamwomba mratibu wa ziara hiyo kumwondoa kabisa Shibuda maana sio mwenzetu huyo. kuwepo kwake ni dosari kubwa na anaweza sababisha baadhi ya wananchi kususia kuhudhuria mikutano hiyo....futa kabisa jina lake.
 
Nakumbuka Wabunge wote wa CHADEMA akiwepo na Babu Slaa walizunguka nchi nzima kudai serikali za majimbo,naona wameeacha hiyo sasa wana dai serikali tatu na sasa wanazunguka nchi nzima kutetea hoja kuwa SUGU alikua sahihi kumpiga yule Polisi....baada ya hili sijui kutakua na mzunguko wa kupinga matokeo ya Urais 2015! Wazee wa kuzunguka Nchi nzimaaaaa!

Acha mawazo ya kizamani kama Kingnge. Kila chama kina utaratibu wake wa kufanya kazi
 
futa ccm kabisa kanda ziwa,nawatakia kazi njema ya ukombozi kanda ya ziwa.
 
Nakumbuka Wabunge
wote wa CHADEMA akiwepo na Babu Slaa walizunguka nchi nzima kudai
serikali za majimbo,naona wameeacha hiyo sasa wana dai serikali tatu na
sasa wanazunguka nchi nzima kutetea hoja kuwa SUGU alikua sahihi kumpiga
yule Polisi....baada ya hili sijui kutakua na mzunguko wa kupinga
matokeo ya Urais 2015! Wazee wa kuzunguka Nchi nzimaaaaa!

SErikali ya majimbo itakuja tukiipata tanganyika na wanazunguka kueleza chazo cha vurugu siyo matokeo ya vurugu
 
Ni vizuri kuwa karibu na wananchi lakini
1. Kati yao nani mtaalamu wa kilimo cha pamba??!!Halafu wakulima ndio wanajua zaidi changamoto wanazoziishi sio hao wabunge so wakasikilize matatizo na waone jinsi ya kutatua sio wao kuenda top- down.

2. Kuhusu vurugu za bungeni wanaenda kuwaeleza nini wananchi wasio na dawa na madawati????!!!Limeonekana kwenye Tv na magazeti na kadhalika kwa hiyo wananchi wanahitaji may be kuuliza maswali na wao wajibu hayo maswali sio kulezwa sababu,say unaulizwa nani kasema wanahitaji kujua sababu???!!!

Ugonjwa ule ule wa kudhani kundi fulani linajua sana shida na mahitaji ya wananchi kuliko wananchi wenyewe!!!!!
 
Hii ni hatua nzuri katika kujenga na kuimarisha chama, lazima wadau muendelee kutoa elimu, taarifa na ufafanuzi pale inapohitajika. Biashara asubuhi jioni mavuno.
 
Back
Top Bottom