Wabunge akiwemo 'Ndesa pesa' na Madiwani wa Chadema Moshi wameweza Mikoa Mingine je..?

JIULIZE KWANZA

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
2,569
499
Wabunge akiwemo ndesa pesa na Madiwani wa Chadema wakiwa katika harakati za kuweka Mji wa Moshi safi...inapendeza kama zoezi hili lingekuwa endelevu na kwa mikoa yote.onyesheni mfano wa kushirikiana na wananchi ambao ndio mabosi wenu....na mikoa mingine igeni mifano hii Nawasilisha
 
Miji mingine isubiri mpaka 2015 watakapowatoa ccm, vinginevyo wataendelea kufunga ndoa na uchafu.
 
Ilianza kung'aa pale Ndesa pesa alipoanza kuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2000
Babu yuko makini na ndoto endelevu hata lami alitaka kuweka kwa hela yake mwaka 2003 serikali ika kataa na kudai ni kazi ya halmashauri na sio mbunge
 
Ndesa na mbowe ni vichwa hawana bias ndio wane fikisha cdm apo kilipo sasa niwapiganaji wa kweli na uzuri mmoja hawategei posho zakwao Zuma watosha....ndio maana hawamogopi mwana magamba yoyote ata jk anajua ilo...
 
I like this, ntafanya majumuisho ya hii thread jioni, endeleeni kuchangia
 
vilaza wa ccm, walifanikiwa kufika mosi,waliopita, wakaazi wa moshi, na wasiofungamana na vyama changieni kwa bidii.
 
jamaa alinunua vocha, akaweka kwenye simu. Kisha akatupa chini. Akaondoka.Hatua kumi nyingi akadakwa kistaarabu,na kuulizwa kama ni mgeni Moshi,akajibu kuwa ni mgeni,akapelekwa ofisini,kule akaambiwa kosa lake,na kikaratasi cha vocha akaonyeshwa kama ushahidi.. Akatajiwa faini ya 50,000/- hakuwa nazo. Baadaye wenyeji wake walikuja kumlipia,ndiyo akaachiwa!
 
Mayatima wote wanalipiwa ada za shule za govt kupitia mfuko wa manispaa ni mipango ya madiwani wa cdm toka mwaka jana wameanzisha

Mkuu, ada za shule za kata ni 1500 kwa mwaka! Kwani Moshi kuna mayatima wangapi?
 
ninachokijua juu ya moshi si kwamba wananchi ni wasafi kivile kama watu wanavyotaka tuamini. na kuna mmoja ameenda mbali eti akisema wameenda shule. hamna lolote na Hilo si kweli kabisa. Ila ukweli ni kwamba kuna sheria kali zinazotekelezwa. na watu kila siku wanapigwa fine 20000 na 50000 kwa kutupa taka au kutema mate.
 
Mkuu, ada za shule za kata ni 1500 kwa mwaka! Kwani Moshi kuna mayatima wangapi?

Kwa hiyo unataka kutuambia nini!? hata angekuwepo yatima mmoja tu katika Moshi nzima, hiyo ingetengeneza tofauti katika maisha yake kuliko kutokufanya kitu kabisa!
Au unataka ada iwe milioni ndo uone wamefanya la maana!? Kuna wanaokosa hiyo hiyo 1500 na shule wanafukuzwa! Acha mbwembwe mkuu! Palipo na jambo zuri kupongeza sio udhaifu.

 
Back
Top Bottom