Wabunge ahadi za nini kama jukumu la utekelezaji ni la serikali?

Hao wenye mipango mbona wameshindwa completely kuweka japo msingi wa office yao kwa miaka nenda rudi japo ruzuku ya kufanya hivyo wanapata kila mwaka utawatofautishaje na maçcm kama wataingia madarakani
 
Yaani wakakuambia watakujengea marekani nawewe ukakubali ukawachagua? Wakupima wewe zitakuwa haziko sawa
 
Ebu fikiria rationally bandugu: mbunge yeyote anasema hivyo kwa kuamini serikali itatimiza wajibu wake wa kukusanya kodi na kutumia mapato yapatikanayo kwa maendeleo ya walipa kodi. Sasa kwa uelewa wako unafikiri mbunge akisema atajenga barabara, alimaanisha atajenga kwa kutumia pesa zake? Alisema hivyo akiamini atakapokuwa anaisimamia serikali, serikali itatimiza wajibu wake!

Mbunge kazi yake ni kuishauri serikali namna ya kutumia mapato yatokanayo na kodi kutegemea na changamoto zilizopo kwenye eneo husika. Serikali yaweza kuwa haifahamu changamoto mahususi kutoka kwenye localities. Hivyo mbunge anavyowaahidi wapiga kura, anawaahidi kwa imani kwamba serikali itasikiliza na kuzitatua changamoto hizo.

Sasa sielewi hoja hapa ni nini haswa? Kwanini lawama ziende kwa mbunge na siyo serikali kwa kushindwa kutumiza wajibu wake?
Tena amesema wabunge wa upinzani! Kuna jambo lipo Nyumba ya hoja yake, lkn hajatumia kichwa chake vizuri
 
Aina ya siasa hizi za kilaghai ni vyema tukaziacha; inabidi tufike mahali mbungd awajibishwe kwa ahadi zake anazozitoa pindi anaomba kura.

Ilani ya chama ndio iwe muongozo wa nini serikali itawafanyia wananchi.
Ilani ya chama kipi?
 
Wabunge wetu hasa wale wa upinzani wakati wanakuja kutuomba kura huja kwa maneno matamu yaliyojaa ahadi kede kede ali mradi tuwape kura.

Huja na ahadi ambazo ukizipima unaona marekani hii hapa.

Wakati wakirudi tena kutumba kura tukiwauliza kwanini hawajatimiza wajibu wao hudai kua jukumu lao sio kuleta maendeleo bali ni kuisimamia serikali.

Sasa kama jukumu la kuleta maendeleo sio lao ? kwanini watoe ahadi zisizoweza kutekelezeka.

Hawaoni kwamba kutoa ahadi hewa ni kuipa serikali mizigo yao.

Hawaoni kwamba ahadi hizo ni sawa na hadaa na utapeli.

Kwanini wasitoe ahadi zilizo ndani ya uwezo wao kuziteekeleza?

Au ahadi ambazo ni rahisi kuisimamia serikali ili izitekeleze.

Ifike mahali sasa siasa za namna hii ziishe na wabunge waje na mikakati yao ya maendeleo isiyotegemea mbeleko ya serikali katika kuikamilisha.

Wananchi tumechoka ahadi za uongo uongo za wabunge wetu hasa wa upinzani.
Kijana nadhani umesoma lakini hujaelika. Ni hatari sana kwa watu wa namna yako kuendelea kushawishi umma kwa kuwa unaweza kuwasadikisha upumbavu.

Nitatoa somo dogo sana ili liweze kukuongoza katika views zako hapo baadaye. Kwanza unapotoa somo kwa wananchi usiegemee upande mmoja. Wabunge wote wanaomba kura,wa chama tawala na wa vyama vingine vya upinzani wote wanatoa ahadi.

Jukumu la kwanza la mbunge ni kutunga sheria, la pili kuisimamia serikali, na tatu kuhamasisha shughuli za maendeleo jimboni mwake, na hapa nimeweka chache. Ndiyo maana wananchi mnaombwa kumchagua kiongozi mwenye uwezo wa kuyafanya yote hayo bila woga.

Sasa nikujulishe kuhusu wapinzani unaowabeza. Wapinzani hao wameweza kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo kwenye majimbo yao kwa kuwa wamejitambua kuwa wanafanya kazi ndani ya serikali isiyojali usawa. MpinAni kwa serikali jii ni mtu hatari, na itafanya kila hila asipelekewe miradi. Karata inayochezwa na hao wapinzani ni kuwa na wabunge wenye shule ya kutosha, wenye connections, miradi mingine ni personal proposals wanazofanya na kuzipitishia kwenye serikali za majimbo yao na wanafanikiwa kama tu mtawala wa mahali pale anaona meriti ya miradi husika, vinginevyo tuwape hongera sana wabunge wa upinzani, they are doing great jobs amidst strong opposition from their own government.
 
Aina ya siasa hizi za kilaghai ni vyema tukaziacha; inabidi tufike mahali mbungd awajibishwe kwa ahadi zake anazozitoa pindi anaomba kura.

Ilani ya chama ndio iwe muongozo wa nini serikali itawafanyia wananchi.

Sipingi kabisa mtazamo wako lakini hoja yako iko kiupotoshaji, uelewa finyu na propaganda ndani yake. Hivi umewahi kuona serekali inaomba kura? Msingi wa mbunge kuahidi kujenga miundo mbinu ni kwamba pindi chama chake kikipewa nafasi ya kuongoza serekali basi atahakikisha anaibana serekali ya chama chake kutekeleza ahadi hizo.
 
Kimsingi wabunge wanabaki ni mic tu za kupaza matatizo ya wananchi. Na kama hivyo ndivyo basi walitakiwa kuwa wakweli kwamba kazi yao ni kuongea tu na kuiomba serikali ikiridhia maombi ya mahitaji ya wananchi kwasababu anayefanya haswa ni serikali. Serikali ndo yenye jukumu la kukusanya kodi, kupanga na kutekeleza. Katika haya mbunge hana kazi yoyote ila mwisho wa siku lile jambo likifanikiwa utaona anarudi kujisifia na likikwama lawama kwa serikali.

Ukitaka kujua angalia baadhi ya maeneo na miradi wanayopelekewa, mingine wala hata haijawahi kuwa maombi ya mbunge lakini serikali yenyewe kwa mipango yake inakwenda kufanya. Mfano mzuri ni mkoa wa pwani. Sidhani kama Koka aliomba Pwani ifanywe mkoa wa viwanda lakini sote leo tunaona Kibaha imekuwa ukanda maalumu wa viwanda. Lakini mfano wa pili naangazia jimbo la Bukoba mjini, hakuna miradi Kutoka serikalini iliyokwisha kuanza kutekelezwa tatizo kuna mbunge mpinzani.

Basi kama mbunge ndo wa kuleta hayo na apeleke miradi kule. Lakini angekuwa ni kutoka chama cha bwana mkubwa naamini hiyo miradi ingeshaachiwa. Hapa tunajifunza, mwisho wa siku anayepanga na kutekeleza ni serikali tu. Anao uwezo wa kukwambia bajeti ipo tutafanya na ama bajeti haipo kwa unayoyataka hata kama ukweli hiyo bajeti ipo. Waziri atakwambia vyanzo vyetu vimekwama lakini pembeni watapewa wengine. Na hasa katika zama hizi, majimbo ya wapinzani yalie tu. Ikitokea mpinzani akapewa 5km za lami basi ujue mwenzie CCM atapewa kumi alizoomba zote na ataongezewa nyingine tatu kwasababu tu anayepewa ni CCM, huu ndo ukweli.

Serikali ndo Alfa na serikali ndo omega katika suala la maendeleo na kuendeleza sehemu husika.
 
Aina ya siasa hizi za kilaghai ni vyema tukaziacha; inabidi tufike mahali mbungd awajibishwe kwa ahadi zake anazozitoa pindi anaomba kura.

Ilani ya chama ndio iwe muongozo wa nini serikali itawafanyia wananchi.

Sipingi kabisa mtazamo wako lakini hoja yako iko kiupotoshaji, uelewa finyu na propaganda ndani yake. Hivi umewahi kuona serekali inaomba kura? Msingi wa mbunge kuahidi kujenga miundo mbinu ni kwamba pindi chama chake kikipewa nafasi ya kuongoza serekali basi atahakikisha anaibana serekali ya chama chake kutekeleza ahadi hizo.
 
Aina ya siasa hizi za kilaghai ni vyema tukaziacha; inabidi tufike mahali mbungd awajibishwe kwa ahadi zake anazozitoa pindi anaomba kura.

Ilani ya chama ndio iwe muongozo wa nini serikali itawafanyia wananchi.

Sipingi kabisa mtazamo wako lakini hoja yako iko kiupotoshaji, uelewa finyu na propaganda ndani yake. Hivi umewahi kuona serekali inaomba kura? Msingi wa mbunge kuahidi kujenga miundo mbinu ni kwamba pindi chama chake kikipewa nafasi ya kuongoza serekali basi atahakikisha anaibana serekali ya chama chake kutekeleza ahadi hizo.
 
Aina ya siasa hizi za kilaghai ni vyema tukaziacha; inabidi tufike mahali mbungd awajibishwe kwa ahadi zake anazozitoa pindi anaomba kura.

Ilani ya chama ndio iwe muongozo wa nini serikali itawafanyia wananchi.

Sipingi kabisa mtazamo wako lakini hoja yako iko kiupotoshaji, uelewa finyu na propaganda ndani yake. Hivi umewahi kuona serekali inaomba kura? Msingi wa mbunge kuahidi kujenga miundo mbinu ni kwamba pindi chama chake kikipewa nafasi ya kuongoza serekali basi atahakikisha anaibana serekali ya chama chake kutekeleza ahadi hizo.
 
Sipingi kabisa mtazamo wako lakini hoja yako iko kiupotoshaji, uelewa finyu na propaganda ndani yake. Hivi umewahi kuona serekali inaomba kura? Msingi wa mbunge kuahidi kujenga miundo mbinu ni kwamba pindi chama chake kikipewa nafasi ya kuongoza serekali basi atahakikisha anaibana serekali ya chama chake kutekeleza ahadi hizo.
Na vipi chama chake kisipewe nafasi ya kushinda, ni nini hatma ya huyo mbunge na wananchi wake? Yaani chama kilichoshinda ni mshindani wake. Anao huo uwezo wa kukifanya kitu hicho hicho, utasema ndio. Je, anao uwezo wa kufanikiwa kuibana serikali katika kutimiza ahadi zake alizozitoa huko mwanzoni?
 
Ebu fikiria rationally bandugu: mbunge yeyote anasema hivyo kwa kuamini serikali itatimiza wajibu wake wa kukusanya kodi na kutumia mapato yapatikanayo kwa maendeleo ya walipa kodi. Sasa kwa uelewa wako unafikiri mbunge akisema atajenga barabara, alimaanisha atajenga kwa kutumia pesa zake? Alisema hivyo akiamini atakapokuwa anaisimamia serikali, serikali itatimiza wajibu wake!

Mbunge kazi yake ni kuishauri serikali namna ya kutumia mapato yatokanayo na kodi kutegemea na changamoto zilizopo kwenye eneo husika. Serikali yaweza kuwa haifahamu changamoto mahususi kutoka kwenye localities. Hivyo mbunge anavyowaahidi wapiga kura, anawaahidi kwa imani kwamba serikali itasikiliza na kuzitatua changamoto hizo.

Sasa sielewi hoja hapa ni nini haswa? Kwanini lawama ziende kwa mbunge na siyo serikali kwa kushindwa kutumiza wajibu wake?

Mzee acha kudanganya hapa. Unasema serikali inaweza isijue changamoto zilizo kwenye localities lakini mbunge akajua?? Hivi unajua muundo wa serikali ulivyo wewe?? Serikali sio Rais-->PM-->Baraza la mawaziri tu, bali inaundwa tokea ngazi za vijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, mpaka serikali kuu na huko kote kuna viongozi wanaotumikia wananchi na serikali kuu inapewa taarifa zote.
Mtoa hoja anayo mantiki kubwa sana ambayo hawa wabunge imefika wakati sasa waache kuwadanganya wananchi. Kazi yao ni kuisimamia serikali tu na wala sio waleta maendeleo.
Kwanini wasiseme ukweli tu kuwa wataisimamia serikali na kuikumbusha ifanye kazi yake ya kuleta maendeleo??
 
Na vipi chama chake kisipewe nafasi ya kushinda, ni nini hatma ya huyo mbunge na wananchi wake? Yaani chama kilichoshinda ni mshindani wake. Anao huo uwezo wa kukifanya kitu hicho hicho, utasema ndio. Je, anao uwezo wa kufanikiwa kuibana serikali katika kutimiza ahadi zake alizozitoa huko mwanzoni?

Uwezo wa kuibana serekali hata kama chama chake hakishika dola anao kwa mujibu wa katiba. Ila serekali kwenye utekelezaji ina vigezo vingi. Kwanza ni uwezo wa kibajeti, vipaombele vya serekali iliyoshinda, umuhimu wa miundo husika, wakati mwingine utashi wa kisiasa wa serekali ya chama kilichoshinda dola. Hivi ni baadhi tu ya vigezo.
 
Mzee acha kudanganya hapa. Unasema serikali inaweza isijue changamoto zilizo kwenye localities lakini mbunge akajua?? Hivi unajua muundo wa serikali ulivyo wewe?? Serikali sio Rais-->PM-->Baraza la mawaziri tu, bali inaundwa tokea ngazi za vijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, mpaka serikali kuu na huko kote kuna viongozi wanaotumikia wananchi na serikali kuu inapewa taarifa zote.

Nimesema serikali inaweza isijue changamoto zote kwenye localities. Kwa ulichokisema, unamaanisha una-question relevance ya mbunge au haufahamu maana ya mwakilishi wa wananchi. Mbunge ndiye mwenye kuwawakilisha wananchi kwenye kupanga na serikali namna ya kutumia kodi kwa manufaa ya walipa kodi.

Hao uliowataja ni wateuliwa wa serikali. Kwa mfumo wetu wa kiutendaji hao hawapo responsible/accountable kwa wananchi moja kwa moja. Mbunge na viongozi wengine wote wa kuchaguliwa, wapo accountable kwa wananchi. Hivyo, wananchi ndiyo uwatumia viongozi wa waliowachagua kuwasemea matatizo yao.

Vilevile hao wengine hata wakifahamu changamoto za kwenye localities, hawana uwezo wa kuisimamia serikali na kuilekeza namna ya kuzitatua changamoto hizo. Ni diwani na mbunge tu ndiye wenye uwezo huo: diwani katika ngazi ya serikali ya mtaa, na mbunge katika ngazi ya serikali kuu.

. Kazi yao ni kuisimamia serikali tu na wala sio waleta maendeleo.
Hapa umechinganya. Sasa huoni kama wanapoisimamia serikali, na serikali ikatimiza wajibu wake, ndiyo kuleta maendeleo kwenyewe?

Kwanini wasiseme ukweli tu kuwa wataisimamia serikali na kuikumbusha ifanye kazi yake ya kuleta maendeleo??
Unajichanganya tena! Sasa mbunge atasema anaisimamia serikali kwenye nini na kwanini? Yaani unataka mbunge aseme, "mkinichagua nitaisimamia serikali"? Wapiga kura wanaojielewa si watamwomba aelezee kwa undani ni kivipi itaisimamia serikali na ili nini kifanikiwe?
Mbunge akisema "nitaikumbusha serikali ifanye kazi yake ya kuketa maendeleo", mbunge huyu ataweza kushawishi wapiga kura kweli? Ataikumbusha ifanye kazi kuleta maendeleo yepi na kwenye sekta zipi?

Mbunge hawezi kuwa vague, abstract na generalistic kihivyo. Lazima awe very specific katika maelezo yake ya namna atakavyoisimamia na atakavyoikumbusha serikali katika kuleta maendeleo. Lazima awe na uelewa wa kutosha juu ya changamoto za kimaendeleo zinazowakabili wananchi kwenye eneo husika. Hapo ndipo kunapelekea yeye kutoa concrete promises: "nitaisimamia serikali katika kuhakikisha inatumia kodi kuweza sekta ya kilimo kwa ruzuku za pembejeo, mbolea n.k. Inatumia kodi kugharamia mafunzo ya mabwana na mabibi shamba. Inatumia kodi kufadhili tafiti endelevu za kilimo n.k." Mbunge kama huyu ndiye anaweza kushawishi mpiga kura anayejielewa, kama kilimo ndiyo changamoto ya eneo husika.
 
Back
Top Bottom