Wabunge 20 CCM wamtega Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge 20 CCM wamtega Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]
  Mwangwi wa uvuaji gamba


  Mwandishi Wetu


  [​IMG]  Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Mrisho Kikwete


  Wajiandaa kujiuzulu, kutimkia upinzani


  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) sasa kipo hatarini kukimbiwa na kundi la wabunge zaidi ya 20, wanaoweza kujiunga na chama kimojawapo cha upinzani na kisha kushiriki tena katika uchaguzi mdogo utakaoitishwa baada ya tukio hilo, uchunguzi wa Raia Mwema umebaini.


  Hata hivyo, imebainika kuwa njia pekee ya kunusuru CCM dhidi ya hatari hiyo ni utekelezaji wa dhati wa mpango mpya wa chama hicho kujivua gamba, unaohusisha kuwaengua katika nyadhifa za uongozi ndani ya chama, vigogo wenye kasoro za kimaadili, ikiwa ni pamoja na waliopata kujiuzulu serikalini.

  Katika orodha hiyo mbali na Rostam Aziz aliyekwishakujiuzulu na hivyo kujiepusha na shinikizo la kumtaka afanye hivyo, wengine ambao mara kadhaa wamewahi kutajwa katika orodha hiyo ni pamoja na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge.


  Kwa upande mwingine, kundi la watuhumiwa wa ufisadi limeelezwa kuendelea na mikakati ya kujisafisha huku nao wakijiandaa kujitoa CCM kumuunga mkono mmoja wao kuwania nafasi ya urais 2015 kupitia upinzani ikiwa watazuiwa kuwania ndani ya CCM.


  Tayari Lowassa amejitokeza hivi karibuni kukataa kuzungumzia kuhusu kuwania urais huku akitishia waandishi wa habari watakaoendelea kumhusisha na kashfa mbalimbali ambazo hata hivyo alikataa kuzitolea majibu alipoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari aliokutana nao Monduli, hivi karibuni.


  Lowassa anatoa vitisho hivyo dhidi ya waandishi wa habari ikiwa ni takriban miaka mitatu sasa tangu alipoelezwa na iliyokuwa Kamati Teule ya Bunge, apime uzito wa kashfa iliyokuwa ikimuelemea kuhusu Kampuni ya kufua umeme ya Richmond na achukue uamuzi wa kujiuzulu.


  Kwa utashi wake alijiuzulu huku kukijitokeza mazingira yanayotafsirika kuwa yeye ni kati ya viongozi waliokuwa katika safu ya kushinikiza Richmond ipewe zabuni ya kufua umeme, bila kuhakiki uwezo wa kampuni hiyo.


  Kujipanga kwa wabunge hao kunazidi kukiweka katika wakati mgumu chama hicho na hasa vikao vyake, kikiwamo cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambacho ndicho kilichoridhia mpango wa kujivua gamba ambao kimsingi unatafsirika kama ni mageuzi ndani ya chama hicho.


  Mpango wa kujivua gamba kwa mara ya kwanza ulitambulishwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Februari mwaka huu, mjini Dodoma na kuridhiwa rasmi kwenye NEC-CCM, ambamo utekelezaji wake ulianza kwa kuvunjwa kwa iliyokuwa Kamati Kuu ya chama hicho, pamoja na iliyokuwa sekretariati, ikiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.


  Hata hivyo, uamuzi wa kuwaondoa viongozi wenye maadili yanayotiliwa shaka utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua huku kila mara ikielezwa kuwa kama wahusika watashindwa kujiuzulu wenyewe, basi watashinikizwa na chama hicho kupitia vikao vyake rasmi na wenyewe wakipambana kujiokoa.


  Kutokana na chelewa chelewa hiyo na kuahirishwa mara kwa mara kwa uamuzi huo, mambo kadhaa yamekuwa yakijitokeza ambayo moja kwa moja yanahusishwa na kundi la viongozi wanaopaswa kuvuliwa nafasi zao za uongozi.


  Mambo hayo ni pamoja na migogoro ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), mgogoro ambao unafukuta zaidi mkoani Arusha, kwa kumhusisha Makamu Mwenyekiti wa umoja huo ngazi ya taifa, Benno Malisa.

  Vijana wanaotajwa kuhusika kwenye mgogoro huo ambao ni pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM, Arusha, James ole Millya na wenzake wamekuwa wakitajwa kuwa ‘vijana’ watiifu kwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ambaye ni kati ya viongozi wanaotajwa kutakiwa kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama hicho, na hasa nafasi zinazowashirikisha kwenye vikao vya uamuzi kuhusu mustakabali wa chama hicho.

  Haiba ya Lowassa mbele ya jamii ilizidi kuchafuka kwa kasi baada ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia barua yake ya kutaka kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu, kutokana na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond.


  “Kama mkakati huu wa kufanya mageuzi ndani ya chama ikiwa ni pamoja na kuwaondoa ambao uadilifu wao ni wa kutiliwa shaka mbele ya jamii, hautafanyika, basi gharama itakayolipwa na CCM ni kubwa kiasi cha kuhatarisha zaidi uhai wake,”

  “Wengine tupo tayari kujivua uanachama kuliko kuendelea kubaki humu ambamo jamii haiwezi kutuelewa kuwa tunasimamia misingi ya uadilifu au maslahi yetu binafsi. Tutaachia madaraka yote na uamuzi huo usichukuliwe kuwa ndiyo mwisho wetu wa kushiriki siasa, tutaondoka na kujiunga upande mwingine wowote na hata kugombea tena ubunge.


  “Lengo ni kuhakikisha tunaitumikia jamii na kutokukubaliana kwetu na mfumo wowote unaokusudia kulinda mafisadi na ufisadi. Hadi sasa, hali halisi inathibitisha kuwa jamii inazidi kupoteza imani kwa CCM njia pekee ya kurejesha imani hii ni kufanya mageuzi ya ndani kwa kujitenga na wasio waadilifu,” alieleza mmoja wa wabunge aliyezungumzia mpango huo.


  Hata hivyo, mbunge huyo kama ilivyo kwa wenzake sita ambao wamezungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kuthibitisha suala hili na kueleza kuwa wao wako zaidi ya 20 na wote kwa pamoja hawakuwa tayari majina yao kuandikwa gazeti kwa sasa.


  Lakini mbali na wabunge hao, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mtandao utakaoridhia uamuzi huo ni mkubwa ndani ya CCM, ukihusisha safu ya viongozi ambao hawajapoteza imani yao ya uadilifu mbele ya umma.


  Endapo wabunge hao wataondoka, CCM itaweza kuathirika zaidi katika baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini na nyanda za juu kusini.


  Hali hiyo inajitokeza wakati kikao kijacho cha NEC-CCM kikitarajiwa kufanyika mjini Dodoma mwanzoni mwa mwezi ujao, ambapo hatima ya kuwang’oa au kuwakumbatia wasio na maadili itajulikana humo, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa wale wanaotarajiwa kung’olewa kwa kukosa maadili wamekuwa wakishawishi wajumbe wa kikao hicho ili kuwatetea wasing’oke, ushawishi ambao umekuwa ukifanywa kwa kutumia nguvu ya fedha.


  Kikao hicho kijacho hata hivyo kinatanguliwa na kauli mbalimbali za wana-CCM waliodhamiria chama chao kinatimiza mkakati wake wa mageuzi ya ndani. Viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere.


  Makongoro amenukuliwa na gazeti moja la kila wiki akisema kwamba ni lazima uamuzi wa kuwang’oa akina Lowassa na wenzake ufanyike kwa sababu kufanya hivyo ni kutekeleza uamuzi wa vikao halali vya chama na si utashi wa mtu yeyote binafsi.


  Makongoro aliweka bayana kwamba hata kama Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wanafungamana na Lowassa kwa namna yoyote ile, iwe kwa urafiki au makubaliano fulani, maelewano yao hayo hayawezi kuachwa kuharibu chama hicho, kinapaswa kuendelea kuishi kwa mujibu wa misingi yake na si urafiki wa viongozi fulani.


  Makongoro alifikia hatua ya kutoa kauli kali dhidi ya Kikwete akirejea kauli zinazomuweka karibu na Lowassa akisema makubaliano baina ya wanasiasa hao wanaoelezwa kuwa marafiki hayakihusu chama.


  Akinukuliwa na gazeti hilo, Makongoro ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere, alisema jambo la msingi kwa CCM ni kutekeleza jambo la msingi na kwamba hakuna sababu ya kusikia habari za kuteteana.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Strategically speaking, kundi lolote litakalokua na uthubutu wa kujiengua CCM na kufanikiwa kukiridhisha CHADEMA kwamba wao ni wasafi na kwamba wako tayari kufanya kazi kwa pamoja, ni kundi hilo katika makundi hasimu kibao ndani ya CCM kitakachoibuka kidedea juu ya wpinzani wake ndani ya chama hicho ambacho hivi sasa kasi yake ya kuelekea kaburini ni kubwa zaidi leo kuliko hapo jana.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,141
  Trophy Points: 280
  Sijui kama ni ya kweli haya. Tulisikia kitu kama hiki miaka michache iliyopita na kile chama cha CCJ lakini hakuna lililotokea. Tusubiri.
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Ccm inanuka rushwa kuanzia kikwete na vionozi waote,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,chini ya kikwete nchi imaharibuka hakuna matumaini
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  HTML:
  Makongoro amenukuliwa na gazeti moja la kila wiki akisema kwamba ni lazima uamuzi wa kuwang’oa akina Lowassa na wenzake ufanyike kwa sababu kufanya hivyo ni kutekeleza uamuzi wa vikao halali vya chama na si utashi wa mtu yeyote binafsi.
  Nani mwenye guts hizo sasa?
  Lugha nyingine hapa ni sawa na kusema "Heri chama kife kuliko kuweka dosari kati ya Kikwete na Lowassa!....huh!
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Pamoja na bomu zito hilo linalokaribia kulipuka wakati wowote ndani ya CCM na makundi hasimu, migomo kila kona ya nchi, shingi yetu kushuka thamani kutoka Tsh 850 ya Mkapa hadi Tsh 1,870 ya leo kwa dola moja, ajabu ni kwamba rais wetu akiendelea KUTWIT huko Perth Australia, eti anaamini kwamba mambo (hapo chini kwenye RED) yanaimarika sana nchini.

  Jakaya Kikwete

  @jmkikwete Tanzania, East Africa

  The 4th President of The United Republic of Tanzania (Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

  National Website of the United Republic of Tanzania

  Text follow jmkikwete to your carrier's shortcode
  [​IMG]

  jmkikwete Jakaya Kikwete
  Tanzania supports Kenya's military offensive against Somalia militia Al-Shabaab.We back Kenya's decision to invoke... fb.me/Rwh6TS06
  2 hours ago

  [​IMG]

  jmkikwete Jakaya Kikwete @
  @Benjamin_Masige @Semkae We have The Planning Commission;bit.ly/rR3dhr
  3 hours ago

  [​IMG]

  jmkikwete Jakaya Kikwete @
  @sikika1 Thank you for the link.A well coordinated survey and representative sample.The situation is improving.(experts,facilities & ratios) 29 Oct

  [​IMG]

  jmkikwete Jakaya Kikwete
  Medicines and Medical Supplies Availability Report (a case of 71 districts and 30 health facilities).http://bit.ly/uuZ7KQ via @sikika1

   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni kwanini kulikuwa na Makubaliana kati ya Kikwete na Lowassa? Kwahiyo inadhihirisha kuwa bila Lowassa Kikwete asingekuwa Rais wa Jamhuri?
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Wana macho hawaoni wanamasikio haya sikii na wana akili isiyofikiria...still holding my prophesy there is no way this people are going to survive...Mninukuu I saw it three years a go nimewatahadharisha mara kadhaa hawakuelewa let them face the music and dance to the tune! Hii inabidi itoke ili wengine tushike nafasi zetu tulizoahidiwa na King of Kings.....Kila uamuzi utakaochukuliwa uta act on our favour!
   
 9. A

  Akiri JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Lisemwalo lipo kiongozi kama halipo linakuja
   
 10. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kila kukicha habari ni hii tu lowasa gamba, kujivua, uraisi eeeh!!! hakuna mtu anayefikiria kuipa nguvu shilingi ya Ki bongo wala kuimarisha uchumi, ni siasa tu ahaaaaa!! Haya mtoa hoja baada ya kuelezea ya lowasa na magamba yake tuelezee pia uzuri na usafi wa mfalme kikwete na prince riz1. Haya ndo madhara ya kumpa uraisi mswahili kila kitu nimajungu tu na umbeya, serkali haiwezi kuendesha kwa style hii ya umbeya na majungu na kujuana na umwinyi
   
 11. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  That's the paradox of the century.

  Makongoro (au Mako kwa wale tuliokuwa naye) wakati CCM ikiwa chini ya Baba yake na kuwa na misingi bora kuliko ya sasa, alisema si chama chenye mwelekeo wala kutetea wanyonge. Akaingia NCCR na 'kupewa' ubunge Arusha bila misukosuko kama waliyoipata akina Lamwai na Kaborou.

  Alipopoteza ubunge na kubaki kubangaiza, 'makubaliano' na baada ya kuombewa na Mama kwa Mkapa yakamrudisha CCM, dada yake Anna akapewa ubunge viti maalum, na hatimaye kwa hisani ya Kikwete akapewa Uenyekiti CCM Mara.

  Sote tunajua CCM ya Nyerere/Mwinyi si CCM ya Mkapa wala Kikwete.

  Ni lipi leo katika CCM ya Kikwete ambalo ni bora kuliko CCM ya Nyerere kiasi kwamba Makongoro analivalia njuga kuwa lisiharibu chama? Kama CCM ya Nyerere haikuwa na misingi bora ya kumfaa Makongoro, je nini kimebadilika hadi CCM ya Kikwete ikawa piganio la Makongoro?

  Kuna bwana mmoja alinidokeza kuwa CCM ya leo ni NCCR ya miaka ya 90 imeingia kwa mlango wa nyuma, akatoa mifano ya Wassira, Makongoro, Bagenda, Akwilombe. Nadhani sasa naanza kupata hiyo picha.
   
 12. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Upinzani wa kweli ndani ya Tanzania utatoka ndani ya chama tawala (CCM). Kujitenga kwa hao wabunge zaidi ya 20 itakuwa ndiyo mwanzo halisi wa vyama vingi vya siasa ndani ya Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.
   
 13. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM is a walking coffin!
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  political trash.. Kila siku new drama... Fanyeni basi kama mnaweza
   
 15. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sidhani!!!!! nawaona wote wamekaa ki uchumia tumbo sana a single promise to certain lucrative gvt post itawafanya wasikimbie chama. Lowassa mwenyewe kapigiwa simu asiongee fully aliyotaka kuyaongea kwenye press na kweli kanywea akaishia kubit around the bush, itakuwa hao wa kuhama chama?
   
 16. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  natamani kuwajua hao wabunge wanaotaka eti kujiondoa sisiem na kujivua ubunge, daaaah!
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wachumba tu hao... kesho akija mwingine wanaperepete tena, keshokutwa wakiwa na JK kwenye mbio za mwenge wanayumba tena

  BINAFSI NAWAONA WANASIASA WA TYPE HIYO WOTE WACHUMBA TU!!! a true patriot hafanyii kazi zake gazetini
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Na wewe unaamini RAI??? si njaa tayari ishapiga hodi na wao wako kwenye mkumbo sawa na IJUMAA au UWAZI??

  uandishi gani huo wanaoleta
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,141
  Trophy Points: 280

  Nakubaliana na wewe Mkuu na ndio maana pamoja na kuwa Sitta si msafi namuunga mkono sana juhudi zake za kuipinga Serikali ya CCM akiwa ndani ya magamba, kwa mfano katika hii issue ya malipo fisadi kwa dowans ya shilingi 113 bilioni ambayo yalikuwa yalipwe tangu January 2011 lakini kutokana na Watanzania kuyapinga malipo hayo hadii hii leo hayajalipwa. Sitta ndiye Waziri pekee hadi sasa ambaye amesimama hadharani na kuyapinga malipo hayo fisadi. Sijamsikia Pinda (huyu alishayafagilia malipo hayo), Mkullo, Ngeleja (huyu naye alishayafagilia malipo hayo) , Membe na Mawaziri wengine watoe kauli zao kama wako bega kwa bega na Watanzania au wako bega na bega na mafisadi wa Dowans.
   
 20. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hao wabunge 20 wanaosema wanataka kujitoa kama hao mafisadi hawataondolewa ni wasanii tu!! Wabunge wote wa ccm ni wachumia tumboni hivyo basi watachuuzana kuwa waondoke, wawili watatu wanaweza fanya hivyo halafu hao wengine watawachuuza wenzao na kubaki ndani ya ccm: halafu hao walioondoka wataanza kalalama kuwa walikubaliana kuwa waondoke wenzao wamebadili nia!! Mambo kama haya sio mageni kwani Mpendazoe alitoka CCM kwenda CCJ akitegemea wenzie watamfuata hatima yake ikawa wakina Mwakyembe na Sitta ndio hao wameukwaa uwaziri na yeye amebaki kulialia. Wabunge wa ccm hawana ubavu wa kuweza kutoka humo watabakia kuchezeshwa kiduku na mkweree full time.
   
Loading...