Wabongo bana sijui tukoje!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabongo bana sijui tukoje!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quemu, Oct 9, 2009.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Wabongo bana sijui tukoje!!!!!!!! Inakuwaje hatuwi wakweli ikija kwenye masuala ya kushirikiana kikazi/kibiashara? Kwa nini tunapenda kupeana matumaini yasiyo na matumani? Nimekuja kwako kuongea nawe kuhusu uwezekano wa kampuni yako kushirikiana na kijikampuni changu kiofisi. Sasa wewe badala ya kunipa ukweli halisi ya kuwa uwezekano upo au haupo, unanipa vijimatumaini vya kuungaunga. Isitoshe kila nikija ofisini kwako kuulizia maendeleo, unaniambia unamsubiri unayeshirikiana nae arudi kutoka safarini wiki ijayo. Ni mwezi wa 3 sasa huyo bwa'mkubwa hajarudi kutoka safarini tu? Halafu kila nikija kisingizio ni hicho hicho (bila ya shaka huwa unasahau kuwa ulikitoa wiki za nyuma). Haya sasa na simu zangu umeanza kuzichuja...

  Unat#@$& na nyoka anayetema funza.

  [​IMG]
   
 2. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 790
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 80
  If u ask me, i'll tell u hivyo ndivyo tulivyo, hii ina-reflect hata mikataba ya kipuuzi tunayoingia kama taifa kisa hatuwezi kusema hapana au ukweli wa tunavyojisikia. Pole mzee tafuta kampuni yenye credibility nzuri ufanyenayo kazi.
   
 3. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Unajua nini Nwaigwe.....tatizo linazidi kukithiri kwa sababu watu wanaleta umwinyi makazini. Yaani watu hawatenganishi kabisa kati ya kujadiliana usimba na uyanga vijiweni na kujadiliana masuala siriazi ya kushirikiana kikazi maofisini. Kwao wao hizi ishu mbili zinastahili uzito sawa.

  Ningetaka kujadiliana kuhusu mipasho ya kwenye khanga anazovaa mkeo, bila ya shaka ningemfuata yeye nyumbani kwako (wakati wewe huko kazini).
   
 4. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 790
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 80
  Lakini mbali na udhaifu wote huo wapo watu serious kazini bwana. Siku hizi kuna kampuni zinazoongozwa na vijana kama wewe ambao wana exposure yakutosha toka nje, ebu usi-conclude endelea kutafuta kampuni nyingine.I can imagine u-mwinyi upo hasa kwenye mashirika ya umma ambayo yameshikiriwa na wazee wasiotaka kupisha vijana, but still kama nilivyosema exceptional zipo be informed utazijua.
   
 5. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hivi unaweza kuamini nikikuambia kuwa asilimia kubwa ya hao vijana ambao wanapaswa kutumia expesure yao kuleta mabadiliko makazini, ndio wanaojisahau haraka na kujikita kwenye umwinyi. Amini usiamni, huyu jamaa ninayemshupalia hapa amemeza exposure ya karibu decade mbili mamtoni. Yaani hata miaka 3 hajamaliza toka arudi bongo. Lakini ndo hivyo tena karudi kule kule.
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  "Miafrika ndivyo ilivyo"... kwani unafikiri ile mijamaa iliyo sign mikataba ya Radar, Richmond, ATC, TRC, NBC, IPTL, n.k. haikuishi majuu?!

  Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi

  Pole sana ndugu yangu, Waafrika ubinafsi na umwinyi umetuzidi.
   
 7. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 790
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 80
  Sasa tuseme tumeumbwa wapumbavu? Huyo jamaa ebu mpe za usoni, mpe ukweli wa maneno yake, au vipi tafuta mshindani wake ufanye naye dili.Vipi umesharudi bongo?
   
 8. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 790
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 80
  Kwa dizain hii hatuwezi kufika mbali, tutabaki hapa hapa.
   
 9. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa Steve. Unakuta unaipeleka biashara kampuni. Biashara ambayo unajua na yenyewe inajua itaingiza kipato, lakini bado wawakilishi wake wanadengua kana kwamba unaomba msaada. Sijui tukoje!!!!
   
 10. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Sawa kabisa...hivyo ndivyo inavyotakiwa. Dawa ni kumpa laivu tu. Kwanza makaratasi yenyewe niliyochukua kwake ngoja niyachane tu.

  Mimi niko bongo mwezi wa 3 sasa. Na siondoki hapa mpaka kieleweke. Vipi wewe si umesema unakuja wiki chache zijazo...au sio? Ukifika wewe nicheki ili tukutane pale pa siku zote. Namba yangu ni ile ile ya miaka yote.
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  eehe heee heeh nani huyo anayekuzuga na matumaini feki

  try again later
   
 12. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,408
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Mimi nakubaliana nawewe kabisa yakwamba wabongo bwana sijui mkoje,yaani unaona kabisa kuwa hapa unapotezewa muda lakini bado unaendelea kufuatilia,mi ninachojua ni kwamba moja ya desturi ya wabongo ni kupoteza muda,sasa miezi mitatu yote hiyo huuonei huruma muda?
   
Loading...