WABADHIRIFU WA MIRADI WANALIANGAMIZA TAIFA

WABADHIRIFU WA MIRADI WANALIANGAMIZA TAIFA

Besta Mlagila

Senior Member
Joined
May 29, 2018
Posts
101
Reaction score
191
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Mbinga, John Ndimbo amewaonya wabadhirifu wa fedha za miradi ya umma, kuacha uovu huo, kwani unaliangamiza taifa na kuumiza wananchi wa maeneo zilikoelekezwa kutumika. Aidha, amemtaka kila mwananchi kutenda haki kwa upendo katika eneo lake, iwe kazini au nyumbani ili kuchochea amani na utulivu alivyodai haviwezi kuletwa na Rais au maaskofu peke yao.

Amekemea viongozi wanaotumia nafasi zao na kujifanya kama sawa na Mungu, huku wakiwanyanyasa watu kwa kuwanyima haki za msingi na kuwataka kuelewa kuwa wanatenda chukizo kwa Mungu hivyo wabadilike na kutenda haki. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, aliyasema hayo jana katika mahubiri aliyoyatoa katika Misa Takatifu ya Krismasi, iliyofanyika kitaifa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Kiliani mjini Mbinga mkoani Ruvuma.

Tunapotazama na kusikiliza vyombo vya habari, tukiangalia harakati za mawaziri wanapoenda kutembelea miradi mbalimbali, unasikia waziri analalamika watendaji kukosa kutunza fedha za miradi, wanafanya ubadhirifu wa fedha za miradi, tukifanya hivyo tunatengeneza shimo la matatizo makubwa kule zilikokusudiwa. Fedha za serikali zinapaswa kutumika vizuri. Hawa wanaokemewa kufanya ubadhirifu na ambao si waadilifu ndio tunasali nao pamoja, ndio maana nasema sisi tunapaswa kuwa mfano lakini baadhi yetu ndio hao tunaharibu miradi ya serikali. Hakuna imani itatetea ubadhirifu au kukosa uadilifu kwa mali za umma,” alisema Askofu Ndimbo.

Alisema viongozi wanapaswa kuishi kwa mfano wa maisha ya Yesu Kristo, yalioongozwa kutumikia zaidi ya kutumikiwa. Alisisitiza kuwa viongozi wa leo, wanapaswa kuishi hayo kwa utenzi usemao; “Kuongoza kwa kutumikia na kutumikia kwa kuongoza” ili kuwavuta wengine kwenye utulivu, imani, matumaini na usalama.
 
Back
Top Bottom