asante kwa ushauri.
ivi, nikiamua kunyamaza itakuwaje? si anaweza kuelewa kuwa am not interested, au nyie mnaionaje hii. Je nimueleze mume wangu?
huyu baba ni mtu mzima kidogo, yani anapishana umri kidogo tu na baba yangu.
sasa Yassin mbona unanichanganya? mara unakubaliana kuwa nimueleze mume, mara nimueleze mume wa nini.
Sasa ushauri wako ni Upi?
hewala,kua makini binti.Hizo ndio technik zetu wanaume hivyo dont be stupid
we unafikiri kwanini anasema anasita kunipigia simu? na kama ni maswala mengine, sisi ni majirani na yupo free kunitembelea nyumbani kama ilivyo kawaida.
dalili ya mvua hiyo .. mjibu tu .. kumbe hii ni namba yako basi nashukuru kwani umempunguzia mume wangu kazi kwani jana tu alizungumzia kukufuata ili akuombe namba yako .. basi nitampatia hii message aisome kabisa .. ubarikiwe
acha kutuzuga wewe'hujambo xxx. ninayo simu yako mda mrefu lakini kila nikitaka kipiga nasita. mimi ni YYYY' hii message imetoka kwa mme wa jirani yangu ambaye familia yangu na yake zinaheshimiana sana na ni marafiki wakubwa. Sasa hii message aliyonitumia imenichanganya. najiuliza maswali mengi, je ana nia gani?? mimi bado sijaijibu lakini nawaza je inawezekana hana nia mbaya?
Wana JF naomba msaada wa mawazo.