Waathirika wa anguko la RA, EL, et al

Waathirika wa anguko la RA, EL, et al

Kuna jambo linaniumiza kichwa. Wakati hawa jamaa wakiwa na nyadhifa zao serikali ilikuwa inashindwa kuwachunguza na kuwachukulia hatua. Je sasa serikali itawachunguza na kuwachukulia hatua? Je rais atamruhusu Edward Hossea sasa kufanya kazi yake dhidi ya tuhuma kwa hawa mafisadi?
 
Najua taarifa za wikileaks kuhusu Tanzania zinaweza kutoa mengi kama zitaendelea kutoka. Lakinin uchunguzi kwa hawa inabidi tuanze na faili la IPTL ndipo mtu awe na nguvu za kuchunguza mwingine. Magamba ya CCM yameanza siku nyingi na hawa bora yao yanaanza kuvulika hao ambao bado wamekumbatia yao ni hatari sana.
 
Yawezekana ama kweli wameanguka kisiasa au ni mchezo wa kuigiza. Vyovyote ilivyo, kuna mabadiliko katika maisha yao ya kisiasa na kiuchumi na uwezo wao wa kuwezesha mawakala wao wa kisiasa na kiuchumi.

Ni wazi, kuna wapambe wao wengi ndani ya chama tawala, upinzani na serikalini. Baadhi yao naamini walikuwa kipato chao pekee kinatokana na ukuwadi wao, uvuvuzela, kunusa taarifa na pengine kushulikia adui.

Baada ya mabadiliko yaliyofanywa ngazi ya juu ya ccm, naamini kwamba maisha na kipato cha hawa wapambe vitafifia. Baadhi wanaweza kuwa jobless (mfano, kuna watu tayari wameaga hapa janvini na wengine wanaonekana kubadili falsafa zao)

Je tunaweza kukisia ni watu wangapi wameathirika na mabadiliko haya na ni kwa kiwango gani? Je sasa nchi itatawalika?


Masikini Beno Malisa and the companny. Mtakua mnalia sasa RA katoswa:angry:
 
JK mwenyewe ni gamba. Yupo ktk first 11 ya Dr Slaa. Ajivue au avuliwe. Usanii mtupu.
 
Hebu tujaribu kutengeneza orodha za wanaohusika (papa, nyangumi, sangara, na dagaa) na haya yafuatayo;

EPA na matawi yake yote

IPTL

Richmond/Dowans

BoT twin tower

NSSF

Daraja la Kigamboni

General Tyre

PPF

Stendi ya Mwenge

Ubungo Bus terminal

Jengo la UVCCM morogoro road

Viwanja vya wazi

Uwindaji Loliondo

Mikataba ya ujenzi wa Barabara

MSD uagizaji na usambazaji wa dawa

Bandari ya DSM

Ufujaji wa fedha zetu kwa mujibu wa taarifa za CAG

.....
.....
.....
.....
 
Hawa mafisadi ilisemekana wanaweza kuiyumbisha nchi kama watakamatwa - Peasant's son!!! Sasa hizi nguvu za ghafla za hiki chama zimetoka wapi kama sio usanii???:help:
 
Hawa mafisadi ilisemekana wanaweza kuiyumbisha nchi kama watakamatwa - Peasant's son!!! Sasa hizi nguvu za ghafla za hiki chama zimetoka wapi kama sio usanii???:help:

Ukikuta serikali inayosalimu amri kwa mafisadi basi ujue ufisadi ndio serikali yenyewe. Kwamba ukiondoa ufisadi umeindoa serikali yenyewe madarakani! Na kwa kuwa serikali haiko tayari kutoka madarakani basi ufisadi utadumu
 
Ukumbuke lakini kwamba mtu kama EL alikuwa anahonga in anticipation of political office. Uwezekano wake kupata madaraka umefutika therefore motivation ya kuhonga imekufa
Naona kama tunaota ndoto za mchana. EL alishasema kuwa yeye na JK hawakukutana barabarani! Ni wazi basi hapa kuna usanii umefanyika na EL atasafishwa tu. Nimeanza kuona baadhi ya habari leo zinasema waliotoswa ni Chenge na Rostam, EL hatajwi!
Naweza kusema kwa asilimia 70 kuwa JK anapenda na atafanya kila juhudi ili EL awe mgombea urais kwa tiketi ya ccm mwaka 2015. Ebu chunguza majina aliyoyaweka kwenye cc, nani anaweza kugombea urais mwaka 2015? Hussein Mwinyi hawezi kwani wanajua fika kuwa wabara hawatakuwa tayari; kwa masuala ya kubadirishana muislamu then mkristo (japo si rasmi), ni wazi basi kuwa hakuna mwislamu atayewekwa kumrith JK. Hivyo ukiondoa waislamu wote walio kwenye cc then utaanza kumuona EL akijitokeza.
Kilichofanyika, ni kumtoa EL kwenye front line ambako alikuwa akipata mapigo ya moja kwa moja na kumrudisha nyuma ili asipate vichapo vya moja kwa moja na hatimae tusahau - take it from me!
 
Sijawahi kuamini matamko ya CCM, hiki wanachotangaza tangaza hovyo kuhusu kuchukuliwa hatua mafisadi hamna kitakachofanyika muda utapita hamna atakejitoa wala wao hawana ubavu wa kumtoa mtu, kama kawaida yao wanajua sisi wasahaulifu subirini in a month watakuja na agenda nyingine tusahau kila kitu, tudandie lile jipya litakalokuwepo!
 
kazi ya kusafisha mtandao wa mafisadi bado ni kubwa sanaa!!labda ajitokeze Dikteta moja wa kuovahaul systems nzima ya Tanzania mpk vijijini
 
Sijawahi kuamini matamko ya CCM, hiki wanachotangaza tangaza hovyo kuhusu kuchukuliwa hatua mafisadi hamna kitakachofanyika muda utapita hamna atakejitoa wala wao hawana ubavu wa kumtoa mtu, kama kawaida yao wanajua sisi wasahaulifu subirini in a month watakuja na agenda nyingine tusahau kila kitu, tudandie lile jipya litakalokuwepo!

Nimeipenda hii, inabidi tuwe makini kufuatilia kauli zao. Kama changa la macho si wanajua mambo ya maandamano?
 
ccm wanacheza na akili zetu, wamegeuza kibao watu wote kufanya wajadili walivojivua gamba agenda za chadema tunaanza kuzisahau, mara utasikia maandamano ya kuunga mkon huku na kule!
 
ccm wanacheza na akili zetu, wamegeuza kibao watu wote kufanya wajadili walivojivua gamba agenda za chadema tunaanza kuzisahau, mara utasikia maandamano ya kuunga mkon huku na kule!

hapana mkuu, kujadili walivyojivua magamba ndiyo agenda yenyewe. We need to understand the implication, if it is true
 
hakuna aliyenguka ni sawa na usemi wao wa kujivua Gamba.........ni wale wale tu ila Gamba jipya!
 
Ahaa, kijana mmoja uvccm Kilimanjaro amelianzisha. Subiri tuone watakavyoanza kutwangana ngumi. Watajionesha wenyewe tu
 
mapema mno kusema wameanguka

Hao wanaoitwa mafisadi hawajaanguka kisiasa kwani bado wana nyadhifa za nguvu tu za ubunge na ujumbe wa halmashauri kuu ya ccm!! Nguvu wanayo ndani ya chama chao na wanaogopwa na uongozi wa juu wa chama na ndio maana wanashindwa kuwafukuza na kubaki kuwaomba eti wao wenyewe wapime na wachukue uamuzi wa busara!! Ukweli ni kwamba hawa mafisadi hawawezi kuondoka wenyewe na watahakikisha wanapoondoka wanaondoka na wengine wengi tu kama vile kufa kisiasa, hawatakubali kufa peke yao bali lazima wawakokote na wengine!!
 
kauli ya professa mark mandosya kwa mwenyekiti kuwa anaomba wale wote wanotuhumiwa waziteuliwe

Hata huyu mtaja kauliten prof Mwandosywa naye yumo kwa mabo hawafai kuteuliwa. Asidhani tumesahu kuhsu uhusika wake kwenye TTCL. jinsi mwane alivyolipiwa sijui shule na mfunzo huko Afrika kusini. Lilikuwa ni rai lile original lilianidka uozo huu na details ya stakabadhi zote.

CCM kuna magamab mengi
 
hapo hakuna ki2...! CCM baada ya kuona wamepoteza their fame, kwa sasa wanatafuta umaarufu wa panya (kazi kujipitisha pitisha waonekane) their central idea ni kumake headlines kwenye media...!
 
Back
Top Bottom