Waasi waendelea kusalimisha silaha zao huko Syria

Waasi waendelea kusalimisha silaha zao huko Syria

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,355
Reaction score
16,408
Waasi wa Syria wasalimisha silaha zao kwa serikali
Waasi nchini Syria wanaendelea kwa siku ya pili leo kusalimisha silaha zao nzito nzito kwa serikali kufuatia makubaliano ya kuihama miji ya kati ya Syria. Wapiganaji wa upinzani wamekubaliana na vikosi vya serikali na washirika wao kuweka chini silaha katika miji ya jimbo la kati la Homs, Talbisseh, Rastan na Al-Houla. Shirika linalosimamia haki za binaadamu la Syria limesema katika taarifa yake kwamba waasi hao wanasalimisha silaha zao kwa vikosi vya Urusi na Syria. Mkuu wa shirika hilo lenye makao yake mjini London, Uingereza, Rami Abdulrahman, amesema mizinga na bundki za rashasha ni miongoni mwa silaha zilizosalimishwa. Zoezi la kusalimisha silaha likikamilika, waasi wanaotaka kuondoka watahamishwa pamoja na raia, ameongeza kusema Rami Abdulrahman. Makubaliano ya kuweka chini silaha katika miji hiyo mitatu yanafuatia makubaliano kama hayo yaliyofikiwa hivi karibuni katika sehemu nyingi za Syria, nyingi zaidi zikiwa zile zinazouzunguka mji mkuu Damascus.

DW UJERUMANI
 
Back
Top Bottom