Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,075
Ukitizama mauaji, hasa ya watoto huko Gaza inasikitisha sana. Ukitafakari ule ugaidi wa Hamas dhidi ya yeyote aliyekuwepo Israel, unapata hasira.
Tangu mwaka 1948, Taifa la Israel lilipotangazwa kuwa ni Taifa huru, katika vita zote za waarabu dhidi ya Israel, licha ya ukweli kuwa Israel ilipata hasara ya kupoteza watu wake, lakini ukweli ni kuwa waarabu ndio walipata hasara maradufu. Mpaka leo, kwa wastani, ni kuwa kwa kila muisrael mmoja aliyepoteza maisha, waarabu 10 - 15 walipoteza maisha.
Kwa upande wa diplomasia, baada ya Waarabu wa Palestina kukaribisha makundi ya kigaidi kuwapigania, kwa kiasi kikubwa waarabu wa Palestina wamekosa uungwaji mkono wa kimataifa, hata miongoni mwa mataifa ya kiarabu. Uwepo wa Hamas, Hizibollah na makundi mengine ya kigaidi yanayofadhiliwa na Iran, kumefanya baadhi ya mataifa ya ⁸kiarabu kuwa karibu zaidi na Israel kwa sababu ndiyo Taifa pekee linaloweza kuyadhibiti makundi haya.
Serikali nyingi za nchi za Kiarabu, ukiondoa Iran, zinayaona makundi haya ya kigaidi ni tishio kwa Serikali zao. Baadhi ya mataifa ya kiarabu, mengine kwa uwazi na mengine kwa usiri, miaka ya karibunj yameamua kuwa karibu na Israel kwa sababu ni Israel pekee ndiyo inaonekana ina uwezo wa kuyatikisa makundi haya ya kigaidi yanayofadhiliwa na Iran.
Hii ndiyo sababu, hutasikia Taifa lolote la kiarabu, zaidi ya Iran, linaweza kuwapa msaada Hamas au Hizbollah. Mataifa haya ya kiarabu yapo tayari kuwapa wapalestina chakula lakini siyo kuwapa silaha makundi haya ya kigaidi.
Hata jitihada za Qatar kutaka mashambulio yasimame kwa muda ili mateka waweze kuachiwa, zinaisaidia zaidi Israel kuliko Hamas:
1) Wakati mateka wa Israel na mataifa mengine wakiachiwa na Hamas kwa uwiano wa 1:3; israel imekuwa ikiwaachia wafungwa wapalestina na kisha kuwakamata wengine kwa uwiano wa 1:3. Yaani kwa kila mfungwa mmoja wa Palestina aliyeachiwa, watatu walikamatwa na kufanywa wafungwa. Yaani Israel imewaachia wafungwa 180 wapalestina, lakini katika kipindi hicho hicho amewakamata wapalestina wengine zaidi ya 600 na kuwaweka kwenye magereza yake. Yaani sahizi kuna wafungwa wengi zaidi wapalestina kwenye magereza ya Israel kuliko hata walivyokuwa kabla ya kuanza kuachiwa.
Wayahudi inaonekana hawafanyi kazi kwa hasara.
Mbaya zaidi katika kipindi wanaachiwa mateka, Israel imeutumia zaidi huo muda kuweza kufahamu mateka wanaoshikiliwa na Hamas wako wapi. Na kwa sababu imefahamika kuwa Hamas wamekuwa wakiwamisha hamisha mateka, sasa UK imepeleka ndege za doria zitakazofuatilia uhamishaji wa mateka wa Hamas.
Kwa upande wa wapalestina, wapalestina waliokufa mpaka sasa ni zaidi ya mara 10 ya waisrael, na bado wanaendelea kufa. Ukija kwenye upande wa mateka, Hamas imewaachilia mateka 60, na haina mateka wapya. Israel imewaachilia wafungwa 180, lakini amewachukua wafungwa wapya zaidi ya 600. Kwa uwiano huu, Wapalestina wanavuna nini? Lakini zaidi ya haya, jana tu wapalestina raia na magaidi wa Hamas, zaidi ya 700 wameuawa. Na kuna vifo vingi vya watoto vya kuleta simanzi kubwa.
Ina maana huko Uarabuni, hakuna watu wenye hekima wawashauri Wapalestina wayakane makundi haya ya kigaidi, ili kufanyike mazungumzo ya wenye hekima baina ya waisrael na waarabu wa Palestina kuokoa maisha ya wasio na hatia kwa pande zote? Toka siku nyingi, Israel ilionesha kuwa tayari kuifanya Palestina na Israel kuwa nchi moja yenye jamii tofauti tofauti, lakini tatizo kubwa lipo kwa Iran.
Nchi za kiarabu haziwezi kufanya chochote hata kama Israel ikiamua kuwamaliza waarabu wote wa Wapalestina, hivyo Wapalestina wanastahili kutegemea zaidi busala yao kuliko kuitegemea Iran na hayo makundi ya kigaidi.
Watoto wanaangamia Palestina, lakini bado kuna simanzi kubwa miongoni mwa familia za wayahudi. Chanzo kikubwa ni Haya Makundi ya Kigaidi ya Iran. Kwa nini makundi haya ya kigaidi yasipifwe marufuku kujihusisha na harakati za Wapalestina kutafuta wanachokiona ni haki yao? Siku zote, hata kama ukiwa na haki fulani, lakini huyo unayedhani kumekubania haki zako, ukamtumia jambazi, hakika hutasikilizwa. Kitakachotazamwa ni ule ujambazi wa lile jitu ulilolitumia. Kamwe makundi ya kigaidi hayataweza kuwaletea wapalestina Taifa.