Ndugu zangu Watanzania Wenzangu, Vyombo vya habari ni muhimu sana katika maendeleo ya Taifa lolote.Aidha vyombo vya habari kuwa na msimamo wa kuunga mkono chama cha siasa sio jambo la ajabu dunia nzima ni kawaida kabisa. Hoja yangu leo inatokana na hoja kuwa kuna waandishi mnanunuliwa na watu binafsi kwa maslahi yao na mnaacha taaluma zenu.
Angalia gazeti la Tanzania daima na mwandishi anaitwa ASHA BANI , toka juzi namna anavyoripoti unaona wazi kabisa ana maslahi na hiyo Kampuni ya asante tours ( Naomba kusahihishwa kama sijaiandika vema , ila ni kampuni hiyo inayotetewa na Nyalandu).
Kampuni hailipi tozo za hifadhi na imeondolewa kwenye kutoa huduma ndani ya mlima kilimanjaro, lakini anagalia gazeti la leo la Tanzania daima wanajaribu kuiponda menejimenti na bodi ya TANAPA kwa maamuzi yao ya kulinda fedha za shirika,ASHA BANI alivyoripoti kuwa TAKUKURU wapokea faili la TANAPA, uhandishi wa kimaslahi kabisa, kwa taarifa za kiserikali nilizonazo na za uhakika ni kuwa serikali imeamuru kampuni hiyo ilipe madeni yake kwanza ili iendelee kutoa huduma, na nawahakikishia umma wa JF hakuna uchunguzi wowote wa TAKUKURU juu ya suala hilo sababu TANAPA wanalinda maslahi ya kampuni zote za utalii na fedha za shirika. Hapa inaonekana ASHA kishakula pesa ya hao jamaa wa asante tours na sasa anajaribu kwa kila namna kuonesha habari yao imetoka gazetini. Mhariri wa Tanzania daima kama yupom makini baada ya kuona maoni ya Mwenekiti wa kamati ya Bunge ya mali asili alitakiwa kuchunguza jambo hili kabla ya kuruhusu habari hii kuendelea kuchapishwa kwa mtazamo wa mwandishi wake.
Ushauri wangu kwa wahariri , waangalieni sana waandishi wenu na muwe mnathibitisha habari wanazowapa kabla ya kuzichapisha, vinginevyo taaluma ya habari Tanzania inakosa mwelekeo kwa waandishi wanaopokea pesa ili kuandika kile mwenye pesa alichokutuma.Tanzania daima mchunguzeni Bani kala rushwa..........
Mkuu Ph.D, Tanzania tuna tatizo la rushwa, hivyo Waandishi kama Watanzania wengine, pia nasi tatizo hili linatukumba. Ila kwa mujibu wa habari hii, sio lazima mwandishi awe amepokea rushwa!, mwandishi anaweza kupokea fedha za "uwezeshwaji"ambazo kwa jina letu maarufu huziita "bahasha".
Sasa zipo bahasha ambazo ni rushwa, na zipo bahasha ambazo sio rushwa!. Tafuta muda upitie makala yangu hii, Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa ndipo uendeleze hizi tuhuma zako ndidi ya mwandishi husika.
Pasco.
Bahasha za uwezeshaji zinagaiwa wazi wazi na mtu unasainishwa!. Kwa kumbukumbu kumbu yangu za bahasha nene nilizowahi kuvuta kama mwandishi, ni niliopokwenda kuripoti UN GA, it was six fugure by then kwa maisha ya bongo sii haba!.haya bwana, bahasha ina kima maalum kinachopashwa kuwekwa, au itategemea na ofisi husika kiuwezo, mwandishi atakuwa huru mara baada ya kupokea bahasha iliyonona, si atajitahidi kujenga urafiki, ili kila wakati aitwe, mh hii si ndiyo takrima, mh si ndiyo bahasha za uchaguzi kwa wajumbe Ni rushwa kwa waandishi ni bahasha,
Bahasha za uwezeshaji zinagaiwa wazi wazi na mtu unasainishwa!. Kwa kumbukumbu kumbu yangu za bahasha nene nilizowahi kuvuta kama mwandishi, ni niliopokwenda kuripoti UN GA, it was six fugure by then kwa maisha ya bongo sii haba!.
Bahasha za uwezeshaji ni unconditional, tunashikishwa bahasha nene kila semina, warsha, mikutano na makongamano na bado tunawalipua!. Waandishi wabeba mikoba wapo, walamba viatu pia wapo na walipuaji tupo!. Kama ni waandishi wa kujikomba komba, huwa wanajikomba tuu with or without bahasha!.
Mkuu Rich, hizo bahasha ni allowances, au kwa kiswahili ni marupurupu, au posho, siku zote hayakatwi kodi!. Kuna fedha za masuhuli, maduhuli, masurufu na posho . Zile pesa za masuhuli ndizo ambazo ndizo zinazilipia mishahara, hizi zinakatwa kodi. Maduhuli, masurufu na posho, hazikatwi kodi!.Mkuu Pasco heshima mbele.
Lakini hii naona kama unakuwa unapotosha umma. Itakuwaje ninyi waandishi muwe mnapewa bahasha mikononi tena zenye ujazo tofauti?
Je huoni kama hii ndio njia murua ya kustawisha mazingira ya rushwa na ufisadi?
Ni kwanini hao wanaotoa hizo bahasha wasiweke kwenye akaunti zenu za benki?
Pia inabidi uwaambie TRA kwamba unapata extra income ambayo hujai-declare, huwezsi ukawa unapata mpaka kiasi cha six figure na kisikatwe kodi.
Huoni kwamba haya mambo yanazidisha usanii kwenye uandishi wenu?
Si unakumbuka neno la chequebook journalism la mzee wetu John Malecela? Lilikuwa na maana sana na leo inaonekana.
Mkuu Rich, hizo bahasha ni allowances, au kwa kiswahili ni marupurupu, au posho, siku zote hayakatwi kodi!. Kuna fedha za masuhuli, maduhuli, masurufu na posho . Zile pesa za masuhuli ndizo ambazo ndizo zinazilipia mishahara, hizi zinakatwa kodi. Maduhuli, masurufu na posho, hazikatwi kodi!.
Fedha zozote za activity zinakuwa expended na zinalipwa kwa cash, hizi hazihesabiwi kama kipato, bahasha hizo za uwezeshaji kutuwezesha hata sisi kutimiza wajibu wetu!.
Hivi unayo taarifa kuwa per diem ya maofisa wa juu wa serikali ni 80,000 per day?. Hii ndio government rate, lakini wakisafiri, hiyo per diem wanakunja, everything is paid for na posho kibao!. Kama wengine wote wanalipwa, lunch, sitting, transport, etc, why not waandishi?.
Naombeni msinitie hasira nikawaeleza ma siri ya ma allowances manene kina fulani wanayoyavuta!.
P.