Waandishi wa habari kabla ya kupambana na Nape na Mwenzake Ndugai anzeni na hawa kwanza

Mar 17, 2016
193
188
Tunashuhudia msuguano mkali kati ya Serikali(Nape, Waziri mkuu na Magufuli) na Bunge(Ndugai) kwa upande mmoja dhidi ya Wanahabari kwa upande mwingine.

Kumekuwa na malalamiko ya vyombo vya habari kubinywa kwa mda mrefu hasa magazeti kupitia sheria ya magazeti ya mwaka 1976.

Kilio kilizidi zaidi mwaka uliopita pale ilipotungwa sheria ya mitandao.Lkn je, ni kweli waandishi wa habari wakipewa wanachotaka watakuwa wamekuwa huru? au je, kuna sehemu tunatakiwa kuanzia kabla ya kufika hapa?, je mazingira ya sasa ya tasnia ya habari yanaifanya serikali isione haja ya kuweka mazingira mazuri ya haki hii ya msingi kikatiba ya utaftaji na upashanaji habari ulio huru zaidi?.

Kwa maoni yangu nadhani kabla ya kufika huku tuanzie hapa kwanza.

Ukifuatilia kwa umakini vyombo vingi vya habari ni kuwa waandishi wa habari hawako huru na mapambano yanayoendelea sasa ni ya wamiliki wa vyombo vya habari kutaka vyombo vyao viwe huru na wala sio waandishi wa habari kuwa huru.
Kwa maoni yangu waandishi wakiwa huru hata vyombo vya habari vitakuwa huru ila tunaweza kuwa na vyombo vya habari huru vilivyo na waandishi wasio huru. Ukiangalia mapambano yanayoendelea yanaweza kutupelekea kuwa na vyombo vya habari huru visivyo na waandishi huru kitu ambacho ni hatari sana kwa taifa.

Naomba tujiulize hv ni kweli waandishi wa gazeti La Uhuru au Tanzania daima wanafanya kazi kwa utashi wao? hebu kesho kasomeni vichwa vya habari vya magazeti haya. Hv ni kweli IPP media wanafanya kazi kwa utashi wao? Mnakumbuka wkt wa bifu la Mzee machache na Mhongo hizi media zilivyotumika? Hv ni kweli Sahara Media Communication waandishi wake wanafanya kazi kwa utashi wao? mnakumbuka kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita mamna vyombo hv vilivyofanya kazi? mnamjua mmliki wa vyombo hv ni nani ndani ya CCM?
Huwa mnavisikiliza vituo vya Magic FM na Redio Five mida ya Asubuhi? Mnawajua wamiliki wake?.

Ni wazi waandishi wa habari wa vyombo vingi hawako huru, wanafanya kazi zao kwa matakwa ya wamiliki wa vyombo hivyo.
Ukiwa na waandishi wa aina hii na ukawa na sheria zinazoruhusu Uhuru wa kutosha, madhara yake ni makubwa mno kwa kuwa wenye vyombo hv wanaweza kuwatumia vibaya waandishi hawa kama tulivoona uchaguzi uliopita na hata wanavotumika sasa.

Mimi nakiona hiki kama ndo kisingizio kinachotumiwa na serikali kwa kiasi fulani kuminya haki hii mhimu hasa kwa ulimwengu wa sasa.

Ni kwa nukta hii mm nadhani kabla ya kufanya mapambano na Nape au Ndugai wanahabari waanze kwanza kudai Uhuru kutoka kwa vyombo vyao vya habari baada ya hapo ndo twende kwa hawa.

Nasema hv kwakuwa naamini tasnia ya habari yenye waandishi wa habari huru itakuwa na afya kuliko tasnia ya habari yenye vyombo huru vyenye waandishi wasio huru.
 
Uncle huu ni ukweli ulio wazi kabisa.
Wanahabari wetu wanaminywa na wamiliki kwa kiwango cha hali ya juu sana.
Na ni kweli uhuru unaotakiwa ni wa wamiliki wa vyombo hivyo na si Wanahabari wenyewe.
Lakini mara nyingi makala yenye kusema ukweli hubezwa na wadau
 
Back
Top Bottom