Msulibasi
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 5,904
- 7,817
Miaka ya nyuma kipindi cha Mwinyi na Mkapa makundi haya yalisaidia sana kukikosoa chama na serekali. Alipoingia JK hadi mda huu wapo kimya ama wanashabikia kila jambo. Nini kimetokea?Ndio maana serekali ya Jk ikawa na mapungufu mengi. Kuna ushahidi hii ya Magufuli ikawa na madhaifu zaidi kama haya makundi yataendelea kujitoa ufahamu.Tazama dhuluma ktk chaguzi,bomoabomoa,zuio la mikutano, ujambazi na mauaji,rushwa,huduma mbovu lakini waliishabikia CCM..Uchafu na majipu yaliyotumbuliwa ni fedheha kubwa kwa haya makundi. Fedheha zaidi wanapoanza unafiki na pongezi kwa marundo.Kanisa katoliki lina dosari kubwa nahisi chama kina mfumo wake humo.Wahadhiri hawa wa leo na majukumu yao ya chama Serekali za wanafunzi na matawi yao.Vituo vya tv na makada wao.Kina Makwayawahenga .Watangazaji wanatetemeka kusoma habari hasi ya CCM au serekali huku wakikejeli hata kupotosha kuhusu umuhimu wa upinzani na demokrasia. CCM ikitumia nguvu hila ktk chaguzi haya makundi yannanywea na kuĵifanya ''amani kwanza, amani muhimu,,, lakini hawaikemei CCM.Nimepunguza heshimaa yangu kwa maaskofu,makardinali,Maprof ,ma doctor .Naziheshim baadhi ya NGOs