Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,797
- 165,543
Tangu Raisi Magufuli aingie madarakani takribani miezi 9 sasa, kuna mambo mengi yamefanyika au kutokea chini ya utawala wake zikiwemo na kauli zake mbalimbali zilizozua mijadala mingi mitandaoni na kwenye maeneo mengine.
Hivyo basi,waandishi jaribuni kuomba muda wa kufanya mahojiano na Raisi Magufuli na mkipata nafasi muulize maswalu ya msingi kama vile;
Ni kwanini anazuia mikutano ya kisiasa kinyume na katiba?
Je,ni kweli hapendi kukosokewa?
Anazungumziaje swala la mfumuko wa bei?
Kwanini mpaka sasa bei ya sukari bado ipo juu tofauti na ahadi ya serikali?Je,wao kama serikali, swala hili sasa wanakiri limewashinda?
Kwanini mara kwa mara anawakilishwa na wasaidizi wake katika mikutano ya nje ya nchi na anadhani yuko sahihi kutohudhuria kabisa?
Je,anadhani ilikuwa ni sahihi kuwaondoa wanafunzi wa UDOM kwa kuwafukuza kwa style ile?
Kulikuwa na ulazima gani kwa serikali yake kuvunja nyumba za watu kwa haraka namna ile miezi michache tu baada ya yeye kuingia madarakani?
Je,ni kweli yeye ni dikteta kama wapinzani wanavyomuita?
Anadhani ni kwanini neno dikteta limeibuka katika utawala wake na si katika awamu zilizopita?
Kwanini aliwahi tamka anajuta kugombea uraisi wa nchi hii?
Je,anaona serikali yake iko sahihi kuzuia mijadala ya Bunge kurushwa live?
Je,anadhani nadharia ya kutumbua majipu bila kuweka mifumo mahususi ya uthibiti itasaidia kumaliza tatizo la ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka?
Ana mpango gani kuhusu swala zima la Katiba mpya?
Serikali yake imekuwa na mipango mingi kwa wakati mmoja.Je kipaumbele chake kwa sasa ni kipi?
Anadhani serikali yake iko sahihi kuanzisha mchakato wa kuhamia Dodoma pasipo kulihusisha Bunge ambalo ndilo lenye mamlaka ya kutenga fedha za kuendeshea shughuli mbalimbali za serikali?
Anaamini Tanzania ya viwanda itawezekana?
Maswali ni mengi mengine mtaongeza wenyewe
Mwalikeni studio au akutane na waandishi kwa mahojiano.
Tumechoka na press release na live event tunataka ajibu na maswali ya watanzania sasa.