Waandishi kama hamkumuuliza Dr.Mpango swali hili,basi wote mnapaswa kurudi vyuoni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,860
Katika kikao cha jana cha Waandishi wa habari na Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi, nilitaraji waandishi wangemuuliza waziri ni kwanini TRA hawajatangaza makusanyo ya mwezi November kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa miezi kadhaa iliyotangulia.

Nikisoma taarifa za kikao hicho cha waziri na waandishi katika baadhi ya magazeti, nashawishika kuamini kuwa swali hilo halikuulizwa maana kama kuna mwandishi angeuliza juu ya swala hilo,basi bila shaka majibu ya swali hili yangekuwa ni moja ya habari kubwa ya kuripotiwa kutoka katiks kikao hicho kutokana na umuhimu wa jambo lenyewe.

Kwa mtazamo wangu nasema kama waandishi walishindwa au hawakuona umuhimu wa kuuliza swali hiloz,basi waandishi wote waliohudhuria mkutano huo wanapaswa kurudi chuoni kupigwa msasa na baada ya hapo ndio warudi tena maofisini/mitaani kuendelee na kazi ya uandishi.
 
Hebu fafanua umuhimu wa swali hilo!
Linajenga kitu gani hasa!
Labda wewe una siri Fulani na it is not necessary kila mtu akawa nayo!
kwa taarifa za pesa za mwezi November unaweza kuzipata muda wowote ule, na hata baada ya kuuliza wangeweza jibiwa kuwa zitatangazwa soon, bado kungekuwa na haja ya kuendeleza mjadala ktk hilo!
unless kuna preliminary reports ambazo wangejengea hoja, au kama kuna "umbea" rasmi ktk mitandao au vyanzo vingine ndio kungekuwa na substances za kutosha kumbana waziri! otherwise majibu ya mchakato unaendelea yangetosha, sababu za muingiliano wa likizo na sikukuu vingetosha kuwa majibu mepesi ya hoja husika!

Labda swali la kuvunjwa BODI ya TRA huku wale walioingia by default wakaendelea kutumikia vyeo vyao, wao wanatengeneza Zaidi ya 70% ya board members na uwepo wao ktk nafasi zao unaelezea tu kuwa watarejea tena ktk bodi hiyohiyo iliyovunjwa kwa ajili yao!
vipi swali hilo liliulizwa? kwangu ningependa sana liwe sehemu ya mjadala, lkn kama halikuulizwa pia, siwezi kuhukumu weledi wa waandishi! inawezekana lilishajibiwa ktk platform nyingine, au mimi pia na swali langu ndio sijui kitu!
 
Huwezi sitisha utaratibu ghafla na bila maelezo alafu watu wenye akili wasihoji.
 
Huwezi sitisha utaratibu ghafla na bila maelezo alafu watu wenye akili wasihoji.
Kila walipotangaza ulipinga na ulikuwa mpiga ramli kuwa watakwama...tulia tu utapata ripoti ya robo ya pili ya mwaka.

Hata hivyo alitoa ripoti ya makusanyo kwa miezi mitano kuanzia july,2016 soma ripoti hiyo vema iliwekwa humu au nenda mpekuzi na si kulalama bila hoja.
 
1483175108102.jpg

Nimesoma hiyo ripoti ya juma tu.
 
Labda wanaogopa kuulimbokiwa maana wanaweza kunyang'anywa pen haraka sana.
 
Huwezi sitisha utaratibu ghafla na bila maelezo alafu watu wenye akili wasihoji.
unachanganya, kutohoji hakuwafanyi waandishi warudi chuoni!
lkn wewe unajuaje kama hawajahoji? maana sio lazima waandishi wenyewe ndio wahoji! lkn je, kwa muda walioutumia ktk mahojiano hayo waliyokuwa wakiulizia hayakuwa relevant?
je, mkutano ulihusu moja kwa moja suala hili la mapato ya kila mwezi ya serikali?
kuna wakati mahudhui ya mjadala yanaweza kuziondoa topic Fulani zisiwe na nafasi. mfano kama leo TFF wangekuwa wanajadili kuinua soka la vijana na waandishi wanadakika 30 za kuuliza maswali, bado ungewalaumu kama wasingeuliza swali la kwanini msemaji wa yanga amefungiwa? hata kama ulikuwa na uhakika alifungiwa kimakosa! hiyo topic ni muhimu kuwa na mjadala lkn kwa mjadala huu wa soka la vijana haikuwa sehemu yake!
anyway mimi sijasikiliza hayo mahojiano na sijui ulikuwa unahusu nini, ila concern yangu ni kwa wewe kuhukumu waandishi kwa kukosa kuuliza swali moja!
 
Back
Top Bottom