Waalimu wastaafu wa masomo ya sayansi kurudishwa makazini

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,819
26,180
Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu wa Wizara ya TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema kuwa pamoja na utaratibu huo lakini pia wataandaa programu maalum ya kuwawezesha mbinuza kiufundishaji wahitimu wa elimu wa masomo ya sayansi ili kuwapa ajira.

Mhe. Jaffo amesema kwa sera ya ujenzi wa maabara kwa kila shule imeongeza changamoto ya hutaji wa walimu wa Sayansi hivyo kwa kufanya hivyo serikali itaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi.

Aidha Mhe. Jaffo ameongeza kuwa serikali imetoa miongozo katika halmashauri zote nchini kuhusu suala la uchangiaji wa ada katika mashule huku ikisisitiza kutoa kipaumbele kwa walimu wa sayansi wanaotafuta ajira.


Chanzo : EATV

uploadfromtaptalk1465222604893.jpg
 
Kizeee kikongwee kitawezaje kishika chaki tenaa
Umri wa kustaafu ni miaka 55 kwa hiari na 60 kwa mujibu wa sheria. Mzee wa miaka 60-65 akipewa mkataba hawezi kushindwa kufundisha. Hata mchakato wa Rais ulioisha uliona wagombea wengi walikuwa above 60. Tuache propaganda.
 
Back
Top Bottom