mwambunnyara
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 518
- 208
Mimi nafikiri walimu wa science kila mara ni wenye kujiona duni na hawajivunii au kukubali career yao Na wamekuwa wakijihisi wakosaji mpaka wameingia ualimu kiukweli hili lina undermine elimu yetu kwani kila Teacher haswaa aliepiga Pcb , A level basi plan yake ni kuchomoka walau akasome clinical officer au Pharmacy yani mguu mmoja ndani mwingine hii sio nzuri eliminishaneni mbadilike
Ni kweli Mkuu,ndiyo maana baada ya kuona wengi wetu wamekata tamaa,hawafanyi kazi kwa moyo,nikafanya kautafiti kidogo ndani ya manispaa ya Morogoro nikagundua kuwa kuna baadhi ya mambo yakifanyiwa kazi watu watafanya kazi ya ualimu wakiwa kifua mbele,tutaendelea kuwekana sawa taratibu,Ahsante kwa mchango wako Mkuu.
mnaunda nn au science za ubaoni....acheni ubaguzi mwalimu ni mwalimu tu...mnataka kuona walimu wengine hawafai wakati wengine mlienda diploma mna E&S...mbona sijawahi kusikia umoja wa medical doctor..phamarcist or nurse.....infirioty coplex inawasumbua
mnaunda nn au science za ubaoni....acheni ubaguzi mwalimu ni mwalimu tu...mnataka kuona walimu wengine hawafai wakati wengine mlienda diploma mna E&S...mbona sijawahi kusikia umoja wa medical doctor..phamarcist or nurse.....infirioty coplex inawasumbua
Na Mheshimiwa rais ni mtu anaejua sayansi na umuhimu wa waalimu wa sayansi kwa hiyo hapo kuna kitu cha kuwapa moyo na kuimarisha umoja wenu. mie si mwalimu.
Siku chache zilizopita tumeona vikundi mbali mbali vikiunga na kuwa na sauti moja,inayitoa mwangwi mkubwa,mfano ni waendesha boda boda,madereva,wauza nyama,wafugaji wa sungura,etc.
Kwanini isiwe sisi???together we can,tusiishie kulalamika tu,tujiunge na kutafuta namna ya kutatua matatizo yetu,kwa umoja wetu!!
Haya ndiyo yanayofanya walimu tudharaulike eti "WALIMU WASAYANSI" ivi wewe Mwalimu wa sayansi peke yako mwanafunzi atafikisha GPA ya 1.6 kuwa na sifa za kujiunga kidato cha tano au kujiunga na health certificate?kikubwa tuungane Walimu wote na kujaribu kupaza sauti kwa pamoja na ukumbuke wanasheria wazuri ambao watakutetea wewe Mwalimu wa sayansi mahakaman unapodai haki zenu wamesomeshwa na walimu wa Sanaa Ubaguzi huu utaenda hadi kwa wanafunzi matokeo yake tutaigawa jamii kwa kila Kundi kujiona wao ni bora kuliko wenzao.
Mkuu,una haki ya kutoa maoni yako,lakini kama ungenielewa vizuri,hata usinge panic kiasi hicho,lengo langu sio kuwabagua baadhi ya walimu wenzetu,nimesema wazi kuwa,walimu wa masomo ya science wanafanya kazi ya utaalamu wa maabara bila kulipwa,na serikali yetu inatambua kuwa wataalamu wa maabara wanahitajika,ndiyo maana ikaajiri wataalamu hao mwezi May,mwaka huu, sasa kama waalimu wa sayansi tunapaswa kufanya mazungumzo na serikali yetu,kwa mambo yanayohusiana na hizo kazi zilizopaswa kufanywa na wataalamu wa maabara,kwa hiyo usinielewe vibaya Mkuu!!