Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Raia wa Afrika wanaojaribu kuvuka na kuelekea barani Ulaya, wanauzwa na watekaji wao na kuuzwa katika "soko la utumwa" nchini Libya. Hayo yamesemwa na shirika la kuwahudumia wahamiaji duniani International Organization for Migration (IOM).
Wahasiriwa wameiambia IOM kuwa, baada ya kuzuiliwa na walanguzi wa biashara ya watu au makundi ya wapiganaji, wanapelekwa hadi kwenye viwanja vya mji au kwenye maeneo ya kuegeshea magari na kuuzwa.
Wahamiaji walio na ujuzi kama vile upakaji rangi au ukulima, wanauzwa kwa bei ya juu, kiongozi mkuu wa shirika hilo la IOM nchini Libya ameiambia BBC
Kwa mjibu wa IOM, maelfu ya wanaume chipukizi kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara wameuzwa katika masoko hayo ya utumwa wa binadamu.
Mhamiaji mmoja kutoka Senegal, ambaye jina lake limefichwa ili kumlinda, amesema kuwa amewahi kuuzwa katika masoko kama hayo katika mji wa Sabha kusini mwa Libya, kabla ya kuwekwa katika gereza moja bovu, ambapo zaidi ya wahamiaji 100 walikuwa wakizuiwa.
Amesema kwamba, wahamiaji wanaozuiliwa waliambiwa kuwapigia simu familia zao, ambao waliulizwa kutoa fedha ya kikombozi ili waachiwe huru, na baadhi yao wakapigwa wakiwa bado wanazungumza kwenye simu, ili kuwafanya jamaa zao wasikie wakiteswa ili watume haraka fedha hizo.
Ameelezea kuwa ni matendo ya "kutisha" ambapo wahamiaji walilazimishwa kuhimili kula kiwango kidogo mno cha chakula, lakini kwa wale wasioweza kulipia wanauwawa au wanaachwa ili wafe njaa, ripoti hiyo inaongeza.
Source: BBC