Waafrika waoshwa miguu na Wazungu

Waafrika waoshwa miguu na Wazungu

RAKI BIG

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2020
Posts
394
Reaction score
459
Katika hali isiyo ya kawaida Maofisa wa Police wa kizungu na raia wengine wa kizungu huko North Carolina nchini Marekani wamejitosa kupiga magoti na kuwaosha miguu watu weusi wenye asili ya Afrika ambao ni viongozi wa dini ili kuomba msamaha wa ubaguzi wa rangi kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Wazungu hao wakiwemo Maofisa wa Police wamesema wanaomba radhi kwa niaba ya mababu na mabibi zao (wahenga) ambao walipandikiza chuki za ubaguzi wa rangi na kuwajaza watu fikra potofu kuwa mtu mweupe ni bora kuliko mtu mwenye ngozi nyeusi kitu ambacho wasema sio sahihi Kwani binadamu wote ni sawa bila kujali rangi ya mtu.

Wamesema wanaomba radhi kwa biashara ya utumwa dhidi ya waafrika, pia wanaomba radhi kwa vitendo vyote Vya kinyama na kifedhuli walivyofanyiwa watu weusi na vizazi vyao vilivyopita ambavyo mbegu ya chuki waliyopandikiza wahenga wa kizungu ndio imesababisha yanayotokea sasa.

103476829_1959246960882005_8505372852033034414_n.jpg
 
... wazungu ni level nyingine kwa kweli!
 
Wengi wanataka kuona wazungu wakiosha MITAZAMO YAO, HISIA ZAO, MANENO YAO NA MATENDO YAO KUELEKEA WAAFRIKA.
Nyerere, Mandera, Nkurumah, Martin Jr njooni mtupe uzoefu kama ni kweli.
 
Hiyo ni ishara ya uungwana na kukiri makosa na kutubu, licha ya kwamba makosa walitenda mababu zao lakini kwa jambo hilo wamejitakasa kwa kutambua makosa na kwa hakika wanastahili msamaha na sisi Waafrika tuwe waungwana kuliko wao kwa kuwasamehe, -- kwa karne moja na ushee, leo Wazungu wamekiri makosa yao, hivyo wamejitakasa.

Mtu anayesamehe ni bora kuliko anayesamehewa. Ndiyo maana Mungu ni msahemevu.
 
Dah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

kuna watu watajiona wanapeeendwa hapa kina Sexer dudus na Root

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3]
 
Back
Top Bottom