The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 613
- 1,775
Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na International Telecommunications Union (ITU) imeeleza kuwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ndiyo kwenye watu wengi zaidi walio ‘offline’.
- Afrika ina zaidi ya 71% ya watu waliopo 'offline' wakati Ulaya ikiwa na kiwango cha chini zaidi cha 17.5%.
- Eneo la Ulaya lina matumizi makubwa zaidi ya internet (82.5%), huku Afrika ikiwa na kiwango kidogo zaidi (28.2)
- Kuna takribani 87% ya watumiaji wa internet katika nchi za Ulaya.
- Shirika la ITU linabashiri kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu, 57% ya kaya duniani zitaweza kupata internet nyumbani.
- Inakadiriwa watu bilioni 4.1 wanatumia internet mwaka 2019, ikiwa ni ongezeko la 5.3% ikilinganishwa na mwaka 2018.
- Kati ya mwaka 2005 na 2019, idadi ya watumiaji wa internet imekuwa ikipanda kwa 10% kila mwaka.