Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 255
By Mutakyahwa Kijoka
Umasikini katika bara LA Africa (hasa kwa nchi yangu ya Tanzania) umejengwa katika vipindi muhimu: utumwa na biashara ya utumwa, Ukoloni kabla ya Uhuru wa bendera na baada ya Uhuru wa bendera.
Nitaongelea kidogo utumwa na biashara ya utumwa pamoja na Ukoloni kabla ya uhuru. Nasema kidogo kwasabu hiyo ni historia na changamoto kuelekea maendeleo wala sio kikwazo cha maendeleo endelevu ya sasa hivi. Utumwa na biashara za kuuza watu leo hii mifumo hii haina mguvu, miaka mingi imeshapita na bado hali ni ileile kwa maana ya kulinganisha na hali za waliokuwa wauzaji na watumikishaji wa watumwa.
Ukoloni kabla ya uhuru wa bendera vile vile ni hoja dhaifu kuitumia kama sababu ya kikwazo kwa cha maendeleo yetu kwa sasa. Miaka nayo imepita!
*Uhuru wa bendera* ndio hasa wenye vikwazo vingi kwa nchi za kiafrica. Changamoto zenyewe zimejikita ktk WATAWALA, IMANI ZA KIDINI na UNAFIKI WA WATAWALIWA.
~WATAWALA~ ndilo tabaka muhimu la kuangalia. Nchi zetu ziliwekwa chini ya mbwa mwitu, mafisi, waroho, wapuuzi na wanyonyaji. Kwa bahati mbaya kabisa walioshika madaraka mpaka leo hii wamekuwa ni watu waliojimilikisha raslimali zote chini yao kwa kutumia makampuni hewa, ndugu zao, familia zao au marafiki zao nje na ndani ya nchi.
Hawa watawala wamemiliki vyeo, uchumi, ... kila kitu hadi uhai wa raia zao. Hawa wamekuwa miungu watu. Wanaishi peponi. Masikio yao wameziba na hawajui shida, njaa, ukame, magonjwa, umasikini na kila kitu wanachoteseka nacho watawaliwa. Kifupi wamelewa madaraka na wanaishi maisha ghali sana kuliko ata wakoloni wa awali. Hawa ndio *wakoloni weusi*. Ni wabaya sana kuliko majini.
Ukilinganisha watawala wa sasa ni zaidi wakoloni waliotawala Africa kwa mabavu. Wengi hawawezi kuelewa kwakuwa tumefundishwa na kukuzwa hivyo wakoloni wazungu walikuwa wabaya. Huo ni upuuzi na kwenye fikra Mpya wafaa kupuuzwa. Unajua kuwa at a wao kwao waliwaliwaliana pia? Ata USA ya sasa ilitawaliwa. Maandishi yetu na waandishi wa Africa wanaotupa mzigo kwa wakoloni hawayaongelei haya.
Angalia kwamfano, ni migodi mingapi madini yetu yanachukuliwa tena kwa wingi zaidi kuliko wakati wa Ukoloni na uangalie maisha ya wenyeji karibu na migodi hiyo? Kufikiria kuwa wakoloni waliiba madini yetu ndio maana kwamfano tuko masikini ni ujuha uliopitiliza mipaka yake. Sikuwahi kuona wakoloni wakichimba madini kwa mitambo ya kisasa na kutengeneza milima ya udongo unaotokana na miamba huko chini ya ardhi mf Kahama au Buzwagi.
Ata vile, walijenga reli ambazo zishakufa wakati wakoloni weusi wanaruhusu viwanja ndani ya machimbo ndege zinabeba na kutuachi mashimo! Ata Yale yapitayo bandarini uziacha barabara zetu mbovu zimelalia upande kwa uzito wa madini na mchanga!
Nimetoa mfano wa madini tu ila kuna raslimali zetu nyingi zina bebwa na wahuni hawa kwa vigezo vya wawekezaji ambao ndio wao wenyewe.
Kwakifupi, Africa ilipata mkosi mwingine Mpya, naamini nchi ambazo zingeendelea kuwa chini ya wakoloni walee, Ingekuwa bora zaidi ya hizi zetu. Watawala wetu wana njaa kama majini. Wanataka ardhi yotee, wanataka madini, wanataka bahari, wanataka majumba, wanataka maziwa, wanataka kila kitu,
Wanataka hadi choo cha kulipia mjini...... Hawashibi. Waafrica no katili kwenye uchumi. Ni zaidi ya majitu yenye njaa kali ya kumeza kokoto, misumali, moto, kila kitu kipitacho mbele yao.
Watawala wa kiafrica, nadhani wamemelaaniwa, wanasahau sana. Hawajui shida,
hawajui kuumwa,
Hawajui njaa,
Hawajui ukame,
Hawajui maumivu...
Hawajui kabisa, ngoja niwape mfano, mnamo karne ya 18 nchini ufaransa, mfalme wa wakati huo King Luis 16 alioa mwanamke Mrembo sana kwa jina Marie Antoinette, mama huyu alikuwa katokea Austria Hungary. Alilewa raha za kifalme, mfalme alilipisha kodi za kutisha kumfurahisha mke wake, kodi ya nyumba, kichwa, wanaume, ardhi, mifugo... kodi ya kila kitu kidogo waguse ata pumzi. Yote tisa, hali ilikuwa ngumu sana kama ilivyo Africa ya leo.
Njaa aliongezeka na maisha yalikuwa magumu sana. Mkate uliisha mtaani. Mkate ndio kilikuwa chakula kikuu wakati huo. Sasa siku ya mapinduzi, walikuja waandamanaji wanadai mkate. Kwenye kasiri la mfalme alitoka yule mama na kuwasihi kuwa wangekula keki kwa siku ile! . Mrembo hakujua kuwa watu wana njaa. Yaani alidhani wanapenda sana mkate kuliko keki!. Sio kosa lake. Alikuwa na laana ya kisahau kama watawala wa Africa.
Ata hivyo mfalme na mke wake waliangamizwa siku ya mapinduzi. Ndugu na washirika wao pia waliuliwa ikiwemo familia yake ya watoto 3. Waliopelekwa jela uhamishoni.
Watawala wa kiafrica wanadhani wako salama na ndg na magenge yao. Kwa umasikini unavyoongezeka, dunia inafunguka, kuna siku watu hawatalala njaa. Watachukua hapohapo chakula au Mali zilipo.
Watawala wamejiwekea sheria na misingi ya kisheria inayowanufaisha na vizazi vyao milele na milele Amin.
~Dini na Imani za kidini~ hili nalo ni genge na mkosi mwingine baada ya Uhuru. Kuna vikundi vya matapeli, majizi, wajanja, wahuni, wadhurumaji wengi kupitia dini takribani zote. Wanaubiri miujiza ya kuponya, kutajirisha, nyota....! Hawa matapeli wapya waliolelewa na mifumo ya utawala kutengeneza wajinga wengi kina "Mungu atatenda" wamewafanya waafrica kupoteza uwezo wa akili. Kifupi, hii haimaanishi professor, au mkulima, yeyeto mpenda kuombewa ameshaanguka kwenye ujinga huu na sasa ni mwendo wa kuzamisha kizazi hadi kizazi.
Mnakumbuka Tanzania issue ya babu wa Loliondo? Ule upuuzi wa uponyaji ulivyogharimu maisha ya watu? Kifupi issue ilikuwa well planned na watawala kupotosha umma.
Viongozi wa dini zote kubwa ni matajiri sana. Wanamiliki kila kitu na wako karibu na utawala. Wanamailiki Banks, vitegauchumi vya kutosha na kutisha lkn kila siku wanalia njaa za ujenzi, viwanja, sadaka,.... toka kwa masikini. Banks hazizalishi faida? Vitauchumi navyoje?
Ukweli, dini kwa sasa ni chaka LA wahuni. Wakusanyaji, walafi na wenye uchu wa kuendelea kumasikinisha watu wao. Wanahubiri miujiza na kupanda mbegu badara ya kuwapa waumini akili za uzalishaji na ujasiliamali. Ata walioenda shule uzugwa na kupoteza uwezo wa kielimu. Kifupi dini zinatengeneza misukule wengi kuliko wale wanaotengenezwa na shetani.
Dini nyingi zinaendeleza mahubiri ya kikoloni ' heri ngamia kupita kwenye tundu LA sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu, shinda na kesheni mkiomba,...." Hii Ni mifano tu, lkn umewahi kujiuliza tajiri ni mtu wa namna gani? Umewahi kuhoji kwa kiongozi wa dini atoe ufafanuzi wa nan tajiri...
Kifupi, dini na watawala kwa taarifa yako ni kitu kimoja. Wote hawa wazugaji. Wanakaa pamoja, wanakula pamoja, wanaongoza pamoja, wanapeleleza maisha ya waumini pamoja, wanatawala pamoja, wanafanya kila kitu pamoja..,.
Na kwa taarifa yako tafiti kuhusu viongozi wa kidini barani Africa zinaonesha ni aidha wale wanoongoza makanisa, misikiti, na imani nyingine ni ndugu, marafiki au watu wa karibu wa watawala. So watawala wana viongozi wa dini wamejiweka pamoja kwa namna ambavyo ukiwa na akili ndogo ya kuchunguza mambo hutaona. Ebu fikiria kanisani kwako au msikitini kwako....., viongozi wakoje?
Inaendelea.....