Waafrika ni kama herbivores | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waafrika ni kama herbivores

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sijali, Aug 30, 2011.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,053
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  Nijuavyo, ni wanyama wa 'lower level' ndiyo wasiojali wale wa jinsi yao, waoga sana na hawana ushirikiano. Wanyama kama mbuzi, nyumbu, nguruwe na kadhalika ndio wamo kwenye kundi hili.

  Wengi ni wala majani. Hawa hawana intelligence, akili au ujanja. Wakishambuliwa hata na simba mmoja na wao wako elfu, watakimbia. Mmoja wao akishikwa hawaendi kumsaidia na watamtazama analiwa mbele ya macho yao! Wanyama hawa kwa Kiingereza huitwa herbivores 'wala majani, mimea tu'

  Ukifikiria sana utakuta Waafirika tumo katika kundi hili. Waafrika hawajali wenzao kabisa.

  Nasema hivyo nikitaka kutoa mifano miwili tu ya hivi karibuni. Tangu waasi wa Libya walipoingia 'kuikomboa' Libya, wamekuwa wakitenda matendo ya kinyama kwa watu weusi- Waafrika. Wengi wameuawa na wanaendelea kuuawa eti kwa tuhuma za kuwa mamluki. Tuhuma hii nimeichunguza sana na kuona hata kama wako kweli mamluki ni kidogo sana.

  Waafrika wengi walioko Libya wamekwenda kutarazaki na kujipatia vibarua. Kinachonishangaza hakuna nchi yeyote ya Afrika imenyanyua sauti angalau ya kukashifu tu mauaji ya kinyama wanayofanyiwa hawa ndugu zetu na watu hawa wabaguzi wa rangi hata kuliko makaburu. Kila nchi ya Kiafrika haioni hilo ni tatizo lake.

  Mfano wa pili ni Misri. Kwa makusudi kabisa, nchi hiyo huwapiga risasi Waafrika wanaotaka kuvuka kwenda Israeli kujitafutia riziki. Mamia, au maelfu wameuawa katika njia hii.Kwa mara nyingine , hakuna hata nchi moja ya Kiafrika inayonyanyua sauti.

  Fananisha hali hiyo na kama mzungu mmoja tu aliuawa kwa makusudi katika matukio hayo mawili, kitu gani kingetokea?
  Mimi sisemi mataifa ya Kiafrika yakamie kwa majeshi nchi hizo mbili. Basi hata kulaani, kukanusha, kupinga au kuelezea kutokubali vitendo hivyo.....hatuwezi?

  Tabia hii ya kutojali 'wa aina yetu' imeyafanya mataifa mengi duniani, kwa jumla au kama watu binafsi, wasione kipingamizi au ugumu wowote wa kumnyanyasa, kumkandamiza, kumdharau na kumwonea mwafrika. Wanajua wazi 'wenzao watakimbia tu' na kutazama!
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Sijali, kama siyo woga uliopitiliza ni upumbavu mpevu tulio nao. Linalosikitisha zaidi ni jinsi Waafrika tunavyochezeshwa kama wanasesere (puppets) bila kutambua kuwa kuna mtu nyuma ameshika kamba na sisi tunaruka ngoma tusiyoijua.

  Viongozi wetu ni mabubu kwa sababu ya hofu kuwa mabomu ya NATO yanaweza kuwanyeshea na wao siku moja wakionekana wanakwaza matakwa ya wakubwa wa dunia hii. Umoja wa Mataifa, hasa Baraza la Usalama (Security Council), umekuwa chombo cha ukandamizaji badala ya kuwa cha kutetea wanyonge.

  Wakiishapitisha maamuzi yao wanasema "international community" imepitisha. Ukweli ni kwamba hiyo international community ni USA, UK, France and a few other western nations. Kwenye miaka ya 1960 na 70 tulikuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mambo haya na tulikuwa tunaingia mitaani kuyapinga. Siku hizi vijana wako busy na kutafuta utajiri, kwa haki au vinginevyo, hawana muda wa kufikiria kuhusu ubeberu na ukoloni mamboleo.

  Vijana ndiyo kichocheo cha mawazo mapya na mabadiliko, kama tulivyoona Tunisia, Misri na kwa kiasi fulani Libya. Bila vijana wa Kiafrika (sub-sahara) kuwa na muamko mpya haishangazi kuwa tunakuwa na tabia za ki-hervorous, kila mtu na lwake.

  Ukweli mwingine ni kuwa Waafrika wa Kaisikazini (Waarabu) hawajioni kuwa wao ni Waafrika. Kwao kuwa katika bara la Afrika ni ajali ya kihistoria. Kwa wale mlio ughaibuni au mmewahi kuishi ughaibuni mtakuwa mashuhuda wa hili.

  Hawa watu huwa hawajitambulishi kama Waafrika na hawapendi kuchanganyika na Waafrika. Kwa hiyo ubaguzi wao kwa watu weusi na unyama dhidi yao nchini Libya siyo jambo la kushangaza. Lakini nyuma yake ni 'divide and rule' tactics za nchi za magharibi. Vijana amkeni. Tunahitaji ukombozi mpya.
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tumuachie Mungu tu yeye ndiye muweza wa yote. Hao wazungu na waarabu wana kitu cha kujibu siku ya hukumu kwa mabaya yote waliyowafanyia weusi.
   
 4. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tatizo linalotusumbua waafrika sio uoga, bali ni kukosa ushirikiano baina yetu, kuanzia ngazi ya familia na kuendelea.
   
Loading...