Waacheni wazungu waendelee!

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
173
Bado najiuliza hivi ni lini Afika tutafikia kiwango cha kuwajibika cha kiasi hiki?. Leo asubuhi Bob Qick, aliyekuwa mkurugenzi wa polisi kitengo cha counter terrorisim nchini Uingereza amejiuzulu. Kosa lake ni kushika karatasi vibaya na kuwawezesha wapiga picha kuona kilichomo, hata kusababisha operasheni ifanyike mapema kuliko ilivyopangwa. Najiuliza kama ingekuwa Tanzania au hata Afrika angejiuzulu?. Sasa kwa nini wasiendelee!, mtu umekosea unawajibika. Unapisha wengine nao watoe mchango wao, sisi hata kama kosa litasababisha hasara wewe umo tu, likisababisha mauaji wewe umo tu.
 
Mtu kakutwa na vijisenti vya wizi na bado hajiuzulu ndio iwe kushika karatasi vibaya?

Mpaka siku utakapotokea uongozi ambao utasema sheria ni msumeno unakata bila kujali maskini au tajiri, kiongozi au raia, sisi tutaendelea kuwa wasindikizaji katika maendeleo ya dunia hii.

Ukichukua hata nusu ya standards za wenzetu, Tanzania utafukuza kazi zaidi ya asilimia 75 ya wafanyakazi serikalini.
 
Back
Top Bottom