Wakati Musa anaongea na Farao kuwa awape ruhusa waisrael waende katika nchi walioahidiwa Farao aliwacheka Sana...
Neno la Mungu huwa haliishii kwenye kumwonya mhalifu pekee, hata hao wanaodhani wamesimama, Wana wa Israel walipokataa kuongozwa na Musa wakakaza Sana kumnung'unikia, Biblia inasema, Watu hao walitengwa pande mbili, wale ambao hawakuwa miongoni mwa wasio nung'unika walikaa upande wa Musa, na waliokuwa wakimnung'unikia Musa, walitengwa kwenye kundi la Musa na kukaa Kwa kora aliyekuwa kiongozi wa wanung'unikaji, basi Aridhi ilipasuka na kuwameza wote waliokuwa waliokuwa upande wa Kora (wanung'unikaji)
Kwa hiyo niinyi nanyi ni mfano wa hao wanung'unikaji bila hata sababu ya Maana, ingawa binadamu hawezi kutoa hukumu juu yenu, lakini utajuaje kama adhabu yenu ndio Chama chenu kuisha tu Kwa mpigo kikakosa tu wabunge, kutoka wabunge 50 Hadi mmoja, utajuaje labda ndio laana yenu wanung'unikaji, najiuliza tu maswali kuwahusu ninyi, Maana hamishi kuwasema vibaya viongozi, mmejipa kazi ya kuwa wanung'unikaji kila uchwao, kama ni Adhabu, wacha mchapwe!!
Biblia inasema pia, Mawazo ya Mungu yako mbaaali kama mbingu na Aridhi vilivyo na umbali wake, je ni Nani awezaye kuyafahamu?
Cha ajabu, mmekuwa watoa hukumu juu ya Uongozi huu, utadhani ninyi nanyi ni sehemu ya mawazo ya Nyumba, mkikoti Mandiko na kuyatumia kinyume kabisa na matumizi yake,
Mungu amesema, ameandaa siku moja tu ya kuja kuwahukumu watu woote, waovu na wema watakusanyika siku hiyo!
Mwacheni Mungu awe hakimu katika Enzi yake