Wa-Tz tunaangamia, tunauliwa soon

Wa-Tz tunaangamia, tunauliwa soon

Uko sawa mkuu, tumepoteza uelekeo. Nani wa kuturudisha kwenye mstari?

Dr. Slaa na wazalendo wengi waliozibwa midomo yao kwakutishiwa na serikali pamoja na viongozi walioko madarakani
 
Japo uchungu umejitokeza sana lakini kwa bahati mbaya sana, pengine bila hata ya wewe mwenyewe (MajiyaMtungi) kulitambua hadi hapa, ujumbe wenyewe uliokusudiwa utangulie mbele ya uchungu wote huo mwenyewe umerudi nao tumboni.

Sana sana hapo juu watu tunaoja tu ka-kasha la maneno matupu tu yasiobeba maji hata tone. Mkuu hebu teremka tena uwanjani ukasaidia kuoanisha uchungu wote huo ili upate kuendana bega kwa bega na ujumbe mama basi.

Nimejaribu kusoma post yako kwa makini sana ila sijakuelewa kabisa unachotaka kumaanisha
 
Tofauti na jf, uchungu wk umewahi kuutoa hadharani wakakusikia? Namaanisha majukwaa kibao yanatoa nafasi watu kutoa kilio chao, humu ni sawa na kilio cha samaki,

Ndo mwanzo na ataendelea
 
Mimi mpaka kuna wakati huwa nawatamani wa-CHINA na siasa zao za kijamaa!Huwezi mkuta mwananchi anapoteza muda na siasa kila mtu yupo busy kujitafutia riziki,na mambo kwao tambarare kabisaa!!

kumbuka walikuwa na dikteta wao aliyekuwa akitaka maendeo na ndo kawafikisha hapo walipo na sisi tunabaki kulia na democrasia tu
 
Ngoshash
Hujajua Kama jf ndo hadhara yetu wanyonge, hali zetu dhalili, mageziti yamejaa tambo za wakubwa, walohongwa wakazimishwa, jf bado iko huru, ikiharibika tunaipotezea, mloshiba mwatamba, kuugua, njaa, dhiki,adha za kila siku hamzioni, ATI Mpaka tuwaambie ktk hadhara?ipi Zaidi ya kuniona nikihamisha maiti ya ndugu yangu alokufa kwa kukosa huduma? Hiyo bado c hadhara jaman? Au ya king napolen na mkewe ndo Haya?
 
Nimejaribu kusoma post yako kwa makini sana ila sijakuelewa kabisa unachotaka kumaanisha

Nadhani Mkuu uwezo anataka usema bila kumung'unya sababu ya machungu haya nani anayasababisha na tufanye nini ili tubadili mwelekeo wetu?

Mimi nadhani umelaumu sana siasa lakini siasa ndiyo ustaarabu wa kujitawala duniani kote, hii ndiyo mwendo wa dunia nzima. Hatutaweza kufuta siasa na kupata namna nyingine bora zaidi ya namna ya kujitawala Cha msingi ni wanasiasa gani wanawatawala ndicho kinacho determine mstakabali wa nchi yenu. Na je wananchi mna nguvu na uhuru gani juu ya watawala wenu?

Mimi ninaona tayari tumeanza kwenda kwenye right track, maana elimu ya siasa inayotolewa na wapinzani imeanza kuwaamsha watu na kuanza kutambua mamlaka na nguvu wanayotakiwa kuwa nayo juu ya watawala wao. Bado tunatatizo la umasiki na elimu duni Kule vijijini ambavyo ni mtaji mkubwa kwa watawala wanaotumia rushwa na ulaghai kubaki madarakani.

Ni kweli umasikini vijijini umekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa nchi yetu lakini kibaya zaidi ni kukosa elimu ambayo huwafanya watu kuwa masikini jeuri.
Nchi kama kenya wanao umasikini kama sisi lakini wenzetu wamewasomesha hawa watu masikini ndiyo maana wanajeuri na hakuna mtawala anayeweza kuwarubuni kwa ulaghayi wa rushwa na uongo.

Ni heri kuwa masikini kuliko kukosa elimu maana huu ndo mtaji wa watawala wabovu duniani kote.

Tunahitaji watu wetu wawe na elimu ili wawe masikini jeuri ambao hawatakubali kudanganywa na mtawala ambaye ameshindwa kutatua shida zao za kimaisha.

Hatutakaa tujikomboe, mpaka pale watanzania watafikia kiwango cha kuwa masikini jeuri who can not take nosense za majukwaani ambazo ni propaganda tupu kisa watu wamebebwa kwenye malori na kugawiwa chumvi na Kanga.


kazi kubwa iliyoko mbele ya wananchi si kuwaondoa madarakani watawala ili wengine nao wajaribu, bali ni KUREJESHA NGUVU na MAMLAKA kwao ili waweze kuamua nani awaongoze na kwa namna gani na wawe na uwezo wa kumwajibisha wakati wowote wasiporidhika na mwenendo wa uongozi wake.

Ili kuufikia uhuru na mamlaka haya ni lazima kuwe na mabadiliko makubwa maana walioko kwenye uongozi leo hawaamini juu ya jambo hili wao wanadhani ingefaa tuendelee na system hii ya sasa maana ndo waliyoizoea na rahisi kwao.

We need a system that can be controlled by wananchi, but not a system that controls wananchi!
 
Ngonini
Nakubali kuwa tunahitaji mfumo mpya wa kujitawala, kujiongoza na kusimamia. Mamboyetu, lkn unajua fika Kama hujui uendako huwezi kupotea, thus why tumebaki na party politics badala civil politics, personalised leadership badala ya principles, na criticism badala ya patriotism, hawa unaosema "vyama vya upinzani"ni nani hawa? Cdm? Nccr? Tlp? Cuf? Unaweza kutamka kwa ujari, nafsi, akili na uso Wako vikakiri kweli kuwa tunavyama vya upinzani? Au ndani ya makundi Haya ya "vyama vya upinzani kuna wapinzani" ?
Ni nyimbo tuuuu....toka 2007nchi imesimama, imeporwa Zaidi, hawa wapo wanashibishwa na kodi ya sisi masikini? Au cku Dar ikiwaka MOTO, magari kuchomwa ovyo, na mjini kuwa giza ndo utajua kumbe mpinzani wa kweli c zito,mbowe, slaa, sita, wewe, ila ni sisi watu duni? Kwani nani mpinzani kati ya mpemba aliepigwa risasi2001 na lipumba+maalim sef?
Upinzani wa jukwaani c lolote, tunayoyataka Leo yanawezekana tu hata ccm ikiwepo, na pia yanaweza yasiwe pamoja na upinzani uujuao kushika nchi, nini mwelekeo wA NCHI yetu?
 
Inasikitisha sana kuona taifa limekuwa lakisiasa, kila mtu si mtoto,mwanamke,mwanamume,Dr,shekhe,kasisi,nk wote siasa tu! Tumeacha mambo muhimu ya kitaifa tunajadili watu na viatu!
Tena siasa zenyewe za nani katoga sikio, nani kamwoa nani, na nani mtoto wa nani?
 
Back
Top Bottom