Wa-Tz tunaangamia, tunauliwa soon

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Nashangaa namna siasa za majitaka zilivyoshamiri, magazeti na wanaoitwa waandishi tegemezi nao hawana tofauti, magazeti yamejaa taarifa ambazo hazina msaada wowote kwa watanzania, hatusikii juu ya Mafuta yetu, juu ya dhahabu yetu, juu ya ardhi yetu, juu ya kilimo chetu, juu ya afya zetu, juu ya utamaduni wetu, juu ya tunu za taifa, juu ya mustakabali wa taifa na utaifa wetu.
Heshma yetu imepotea mbele ya walimwengu, utu na nafasi yetu yimedharaulika, wengine wanatuamulia mambo yetu, kenya imetutawala, imetuzuia kujenga barabara serengeti, tumefyata mkia, wazalendo mkowapi?wapiganaji mkowapi? Wenye nchi mkowapi? Arumeru ni kitu kidogo sana ndani nchi, mama zetu, baba zetu, dada zetu, kaka zetu, wadogo zetu vijijin wanaliA hawana afya, magonjwa, njaa umasikini vimewazonga, tunafanya nini mijini? ni hili la pamela lowasa, Sioi sumari, na nassari? Kweli wandugu?
Nashindwa kuelewa, nchi imebaki na wasira tu? Nape? Ndo policymakers wetu? Mwigulu? Slaa? Zitto? Kweli jamani?
Wazee wa upanga pamoja na makumbusho mmebaki na uniform tu za kukatia tepe? Nawaona wakikata nyasi pale lugaro barracks wamechoka? Toeni ushauri walau? Jamii inasema shule yenu ndogo, kweli?
Bongo imebaki na mwanahabari mmoja tu- ulimwengu jenerali khalfan
 
Uko sawa mkuu, tumepoteza uelekeo. Nani wa kuturudisha kwenye mstari?
 
Angel
Eleza mapungufu ya ujumbe, baby wa flora huenda by 29yrs nchi ataikuta majivu
 
Nashangaa namna siasa za majitaka zilivyoshamiri, magazeti na wanaoitwa waandishi tegemezi nao hawana tofauti, magazeti yamejaa taarifa ambazo hazina msaada wowote kwa watanzania, hatusikii juu ya Mafuta yetu, juu ya dhahabu yetu, juu ya ardhi yetu, juu ya kilimo chetu, juu ya afya zetu, juu ya utamaduni wetu, juu ya tunu za taifa, juu ya mustakabali wa taifa na utaifa wetu.
Heshma yetu imepotea mbele ya walimwengu, utu na nafasi yetu yimedharaulika, wengine wanatuamulia mambo yetu, kenya imetutawala, imetuzuia kujenga barabara serengeti, tumefyata mkia, wazalendo mkowapi?wapiganaji mkowapi? Wenye nchi mkowapi? Arumeru ni kitu kidogo sana ndani nchi, mama zetu, baba zetu, dada zetu, kaka zetu, wadogo zetu vijijin wanaliA hawana afya, magonjwa, njaa umasikini vimewazonga, tunafanya nini mijini? ni hili la pamela lowasa, Sioi sumari, na nassari? Kweli wandugu?
Nashindwa kuelewa, nchi imebaki na wasira tu? Nape? Ndo policymakers wetu? Mwigulu? Slaa? Zitto? Kweli jamani?
Wazee wa upanga pamoja na makumbusho mmebaki na uniform tu za kukatia tepe? Nawaona wakikata nyasi pale lugaro barracks wamechoka? Toeni ushauri walau? Jamii inasema shule yenu ndogo, kweli?
Bongo imebaki na mwanahabari mmoja tu- ulimwengu jenerali khalfan
Kwani wewe huwa unasoma magazeti gani?
 
Japo uchungu umejitokeza sana lakini kwa bahati mbaya sana, pengine bila hata ya wewe mwenyewe (MajiyaMtungi) kulitambua hadi hapa, ujumbe wenyewe uliokusudiwa utangulie mbele ya uchungu wote huo mwenyewe umerudi nao tumboni.

Sana sana hapo juu watu tunaoja tu ka-kasha la maneno matupu tu yasiobeba maji hata tone. Mkuu hebu teremka tena uwanjani ukasaidia kuoanisha uchungu wote huo ili upate kuendana bega kwa bega na ujumbe mama basi.
 
Tofauti na jf, uchungu wk umewahi kuutoa hadharani wakakusikia? Namaanisha majukwaa kibao yanatoa nafasi watu kutoa kilio chao, humu ni sawa na kilio cha samaki,
 
Mimi mpaka kuna wakati huwa nawatamani wa-CHINA na siasa zao za kijamaa!Huwezi mkuta mwananchi anapoteza muda na siasa kila mtu yupo busy kujitafutia riziki,na mambo kwao tambarare kabisaa!!
 
wanaweza tuchinjia baharini, kama waliweza kwa baba wa taifa. Wajinga sana hawa
 
Inasikitisha sana kuona taifa limekuwa lakisiasa, kila mtu si mtoto,mwanamke,mwanamume,Dr,shekhe,kasisi,nk wote siasa tu! Tumeacha mambo muhimu ya kitaifa tunajadili watu na viatu!
 
Back
Top Bottom