Wa-Salaam Aleikum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa-Salaam Aleikum

Discussion in 'Utambulisho (Member Intro Forum)' started by Al-Watan, Apr 17, 2009.

 1. A

  Al-Watan JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 4,700
  Likes Received: 4,961
  Trophy Points: 280
  Wa-Salaam Aleikum sana, mabibi na mabwana
  Waungwana hata watwana, jamvini mnaofana
  Wembamba na wapana, wajuvi wa karakana
  Ndimi Al-Watan Nyeti, ziso vyeti
  Mtanzania burushi wa ki-sovieti
  Najitambulisha kwa beti, mnifungulie geti
  Nipate wasaa jamvi hili wakuketi
  Siku hizi mambo neti, kwa kasi kama ya jeti
  Tangu hisabati za seti, wazi wala haziteti
  Alif mpaka zeti, nzuri kama alizeti,

  N'shaperuzi makini na sasa nawaingia
  kabla miluzi ju-chini vina nitawaimbia
  Mpate kuburudika, mashairi yalopikwa
  Kama tunda hakika si la kupepe vundikwa
  Tarakimu na methali vionjo vya kupashana
  Midahalo maridhali yenda kwa kupatana
  Au kupingana hoja, pasipo tashtiti moja
  Na kurusha maambizo pasipo kungoja ngoja
  Ukakamavu kisoja, bila kuleta vihoja
  Kwa kasi isochoja, hatari kama Kamboja

  Hodi hodi wanabodi
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 17, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 70,466
  Likes Received: 28,339
  Trophy Points: 280
  Aleikum salaam....karibu mpaka ndani. Jisikie uko nyumbani....kaa usubiri futari...
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haya sheikh karibu yakhe
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 60,389
  Likes Received: 39,789
  Trophy Points: 280
  Aleykum Islamu :), karibu sana yakhe jamvini, jisikie uko nyumbani kabisa.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Apr 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Aleikum salamu, salam twaitikia
  Mgeni wetu Adhimu, leo umetufikia
  Ni Swahiba Akiramu, mbali ametokea
  karibu mgeni karibu, tuambie tusio yajua

  Kwa jina lake Rahimu, ndugu yetu karibia
  Ndani ya hii forumu, mengi twatarajia
  Nikadiri kukhitimu, hayo ulokusudia
  karibu mgeni karibu, tuambie tusio yajua

  Amekuja ana hamu, baada ya kutuangalia
  leo ametema sumu, ile ilomwingia
  Amekuja na Ilimu, ilimu tusio ijua
  karibu mgeni karibu, tuambie tusio yajua

  Karibu wetu mgeni, kwa hamu twakupokea
  Ajuaye ni manani, siri na yako nia
  Sisi zetu mboni, kilicho moyoni wakijua
  karibu mgeni karibu, tuambie tusio yajua

  Haya wana foramu , mgeni ashaingia
  Aje na yake hamu, twasubiri kwa nia
  Ulonayo muhimu, tupe tupate ridhia
  karibu mgeni karibu, tuambie tusio yajua
   
Loading...