Wa Kenya wana msimamo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa Kenya wana msimamo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gaza, Mar 21, 2012.

 1. G

  Gaza Senior Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 103
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Boder ya Namanga leo shuguli zime dorora haswa upande wa TRA na KRA ,KRA ni kama TRA wote ndio wana kusanya mapato Kenya na Tz , KRA wame ongeza viwango vya ushuru zaidi ya mara dufu kiasi kwamba wafanya biashara wanao peleka bidhaa Kenya wame shindwa kulipia hali hii ime sababisha wafanya kazi wa clearing agency upande wa Kenya kugoma hivyo hakuna kinacho ingia wala kutoka kenya ,kuna magari yamesheheni viazi kutoka nyombe na Maua kutoka AR na bidhaa nyingine nyingi kukwama ku ingia Kenya tayari kwa kuuzwa.
   
 2. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna mahala Kikwete aliulizwa kama tuko tayari kwa Shirikisho la Afrika Mashariki, nakumbuka alisema "hakuna lisilowezekana" Ukiangalia kwa upande wa Kenya wanasiasa wao wanashughulika sana na hili shirikisho, hapa kwetu zaidi ya Mnyika sijawahi kumsikia mtu mwingine ndani ya mizingo yetu ya duru za siasa akilizungumzia kwa maslahi ya Tanzania!!
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu huo msimamo wa nini tena si tunatakiwa tuhuishe viwango vya kodi kwenye nchi zetu za EA? Ina maana walikubaliana kuongeza ushuru mara dufu kwa pande zote mbili lakini TZ hatukuongeza?

  Maua kama hajatunzwa vyema yatanyauka!

  Hivi soko la pamoja lina maana gani? Mimi nadhani ni kwamba bidhaa toka Tanzania kwenda Kenya ni sawa na bidhaa toka DSM kwenda Morogoro, sasa ushuru wa nini tena? Au hatujasaini itifaki ya soko la pamoja = free movement of goods and services?
  Nadhani Wakenya wana chokochoko. Halafu wanatupuuza sana wao wanachotaka ni ardhi ya Tanzania tu hawana lingine. Kuna jamaa yangu wa kutoka huko Kenya eti anataka nimfanyie mpango apate ardhi Morogoro ili alime WALI!!
   
Loading...