Vyuoni elimu chini - Class attendance big issue/sports

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,833
images
images
images
images
images
images

Wizara ya elimu ya juu haina budi kubuni kuiga mazuri toka nchi nyingine ili kuunda mfumo wa elimu ya juu kwa mfumo wa kuwaunda wanafunzi kitaaluma, kimaadili ili kujenga vema future yao. Kiwango cha wahitimu wengi vyuo vikuu ni cha chini sana hilo limekuja onekana tokana na SAUT kutangaza idadi kubwa ya mamia wa wanachuo ambao wamepigwa chini kutopata graduation sababu mojawapo ni academically issue.

Oral communication through English Language ambayo ni keyboard language for their studies, ukiongea nao kiingereza utaona wanavyojiuma ulimi, nashangaa how they communicate in their classes, groups and researches. Mabingwa sana wa kusahihisha spelling, lakini kwenye communication terrible, ambapo vyuoni
effective speaking ni moja ya kitu muhimu katika masomo, majadiliano na kujenga hali ya kujiamini kabla ya graduation. Hawa ndio tunaowatazamia kuwa viongozi na pengine kutuwakilisha katika mataifa ya nje kwa shughuli mbalimbali za kibishara na shughuli za serikali.

Nikianzia na mfumo wa elimu vyuo vikuu nchini ambao unajali zaidi mwanachuo amefanya assignments badala ya mahudhuria darasani ni dosari kubwa ambayo inaweza kusababisha mwanafunzi asipate elimu stahiki ila mradi amefanya class assignments kwamba ni kutoka kichwani mwake, au rafiki yake au pengine instructor what ever inamwathiri sana mwanachuo.

Kinachoshangaa wanachuo Tanzania utawaona siku za kawaida ambapo wanatakiwa wawepo madarasani utawaona wengi tu wakirandaranda mitaani, au maeneo ya chuoni wakati wenzao wako madarasani. Mfumo huu una kasoro kubwa kwa utoaji elimu bora, na pengine ndio moja ya chanzo cha kiwango cha elimu vyuo vikuu kuwa cha kujipakaa kwa nje na kuvaa majoho tu badala ya elimu hiyo inayotakiwa iwe soaked into their brain. You can find out that their brain folders are empty because they do not attend classes.

Marekani mfano mzuri wa utoaji elimu bora kwa mwanachuo
Nikichukulia nchi ya Marekani katika mfumo wake wa utoaji elimu kwa wanachuo, mfumo upo wa kuwabana sana wanachuo mahudhurio darasani licha ya academical results. Mfumo wa utoaji asilimia za credits zinategema:
Mahudhuriao darasani;
Mwanachuo anatakiwa asikose mahudhuria darasani, na ikitokea kwa ruhusa maalum kwa sababu maalumu darasa hilo anatakiwa awasiliane na instructor aweze kupanga muda kufanya full kufidia.
Kama mwanachuo atakosekana darasani siku tatu au nne atakuwa terminated katika kozi hiyo na hivyo kupata hasara ya tuition aliyolipia kwani hatarudishiwa zote ila makato ni makubwa kusajiliwa upya kwa gharama mpya katika semester inayofuata.
Assignments & Final exam:
Mfumo wao mwanachuo hata kama atafanya vizuri katika assignments/tests and final exam ambapo ni wastani wa 70% ya 100% ya all field hawezi kufaulu kwa sababu one third lazima itoke kwenye mahudhurio darasani (class attendance). Wastani wa kufaulu wa class attendance, assignments/tests and final exam ni above 75%, maana yake kati ya hayo matatu moja likikosekana au kutofikiwa wastani wa wakila aspect, utakuwa umeshindwa kiwango cha ufaulu chuoni, ingwa kiwango hupishana kidogo baina ya vyuo kadiri ya board of education ya chuo, lakini basically utaratibu ndio huo.

Lengo la body of education ni kuhakikisha wanachuo wanapata elimu kwa uhakika si kusoma tu kwa ajili ya kufaulu. Mwanafunzi anayekaa darasani, kumsikiliza instructor, kuuliza maswali na kujadiliana na wenzake uelewa wake ni mkubwa kuliko anayejisomea mwenyewe kwa sababu hana nafasi ya challenge ya anayosoma. Ndio maana vyuoni mafunzo ya vikundi yanatiliwa muhimu hata madarasani utaona instructors wanawagawa wanafunzi katika makundi ili kufanya baadhi ya assigments kivikundi.

images
images
images

Eneo mojawapo ambalo halijapewa uzito stahiki katika elimu nchini iwe shule za msingi, sekondari na vyuo ni sports education. Eneo hili lina nafasi kubwa sana katika social aspect licha ya kuwasaidia wanafunzi kisaikolojia na kielimu. Vyuo vingi nchini ni elimu darasani tu na baada ya hapo utaona wanachuo hawana cha kufanya zaidi wasichana kuanza kujiingiza kwenye uwanja wa kujigeuza bidhaa kwa wateja mitaani na maeneo ya stareh na vijana wengine kuwa katika makundia mbayo yanawafikisha kujifunza na kufanya yasiyotemewa. Vyuo vya majuu utaona wanachuo wengi wapatapo nafasi ni mazoezi yakufa ya viungo, kukimbia na kadhalika kujiweka sawa kimaungo na walio katika michezo ni sehemu ya mazoezi na wanapangiwa KM za kukimbia na huwa recorded mazoezi hayo kwenye credits za chuo.

Michezo husaida mengi kama baada ya uchovu wa kiakili ni refreshment, darasa hufanya watu wasiwe active katika miili yao, hivyo michezo huwasaidia kujengeka kimwili na kiakili. Michezo huwasaidia kujenga ubunifu, maana katika michezo licha ya mafunzo hutakiwa ubunifu wa papo kwa papo kutokana na ushindani mchezoni. Michezo vyuoni huibua vipaji vya mastaa mbalimbali wa michezo duniani, kwani wa vyuoni hufundishika vizuri zaidi na kuelewa maelekezo na vielelezo kuliko wa mitaani wasioelimika. Wanamiziki wengi wametokea vyuoni au wamekuza vipaji vyao vyuoni.

Niliposoma kuanzia shule za msingi hadi juu kipindi changu kulikuwa na msisimko wa michezo mashuleni isivyo kawaida. Hali hiyo imekufa ghafla na nilikuja kukumbushwa kitu hicho nilipokuwa chuoni Marekani kuona michezo mashuleni pengine hufunika hata ligi kubwa. Tunahitaji kurudi nyuma kujadili nini kimekwamisha hayo.

Kwa vyo vyote kuna mengi ambayo yanachangia kudorora kwa elimu vyuoni hata shule za awali.
 
tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
You have said it all. Our curriculum should be implemented as it is. Tatizo letu ni kwamba our teachers/tutors/lecturers are frustrated and therefore they don't care about what is taking place in their institutions. Mitaala yetu ni mizuri kwani inasisitiza masomo, shughuli mbalimbali za nje ya darasa nk. Tuboreshe mazingira ya taasisi zetu za elimu na tuwajali walimu wetu!
 
JAK

Member
Apr 23, 2012
92
20
Kuna kozi nyengine zinaitaji vitendo zaidi ya nadharia lakini hazitendewi haki katika ufundishaji hii inasababisha wahitimu wengi kushindwa kufanya kazi kwani nadharia ndo imekaa kichwani.
 
Fpam

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
290
114
mkuu umenena sana na ndio ukweli halisi, mm nipo south korea nasoma chuo flani hapa wao mfumo wao elimu wamekopi 100% toka USA na maprofesa karibuni wote wamesoma huko so kila ulichokisema ndicho kinachofanyika, issue hapa sio USA but mfumo, wakati tanzania chuo tulikuwakuwa tunasoma mtu anaweza asihudhurie darasana hata zaidi ya 60% per semister na akafaulu but hapa namna makasi zinavyogawanywa mtu kama huyo asingeendelea kuwepo chuoni, hapa kutoingia darasani ni kosa kubwa sana na lazima instructor atajua tu ana atakufuatilia hata iwe siku moja per semister, hebu jiulize huyu mwanafunzi haudhurii darasani na anafaulu kwa kukariri unategemea nini huko kazini?

extra activities tanzania niliishia kuziiona kwenye ratiba tu na miaka mingine hazipo kabisa hata kwenye ratiba hakuna mtu anayefutilia chuo kina mwalimu mmoja au wa wawili kwa michezo yote, lakini hapa kila mchezo unavifaa walimu na miundombinu na wapo very strict kufuatilia na wanatoa na marks mwisho wa semister hakuna mwanafunzi anayekosa
ni kweli nchi yetu haina uwezo huo but vp kuhusu hata vitu vidogo tu mpira wa miguuu, basket tenisi tunashindwa kusimamia?

mkuu hii maada tunaweza tukaiandikia hata paper ili kuipa nguvu zaidi
 
Hahaha, umeona ee! Kila kipindi wakati wa kuingia darasani instructor huwa na daftari yake ya mahudhurio ya wanchuo katika somo lake, hivyo anahakikisha attendance ya wanafunzi imefanyika kila aingiapo darasani, anayekosekana ajue moja kwani ni kosa kubwa kama ulivyosema. Bongo tambalare, jamaa wako mitaani na wengine kwenye kibuku they don't care.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,833
Tatizo kubwa vyuo vikuu havina walimu! Mark my words!

Sidhani kama ni hoja nzito, kwani tatizo kama hilo lipo vyuo vingi hata nchi zilizoendelea. Nilichoshuhudia nchi zilizoendelea wanafunzi wa garaduate wenye bongo zuri huajiriwa na vyuo hivyo kuwa part time instructors. Husaidia kupunguza tatizo la instructors na pia nafuu kwa chuo kwani hao ufundishaji wao ni sehemu ya gharama za ada chuoni, na wengi wanaosaidia hivyo ni wale ambao wanamatatizo ya kulipa karo lakini bongo lao zuri. Nchi kama Marekani wengi toka mataifa maskini ambao hukubwa na tatizo la karo ya chuo nafasi hizo ndizo zinazowaokoa hadi wanahitimu PHD.

Manmud

Member
Oct 27, 2012
67
8
Jaman kuhusu clas attendenc ni tatizo la chuo chenyewe kutokuweka sheria mahususi kuhusiana na ilo...ukiangalia vyuo kama st.joseph groups of institute wana sheria madhubuti na kali ktk suala ilo kwan ukiwa kama mwanafunz ktk vyuo vya lazima uattend chuo kila siku na tena unatakiwa mahudhurio yako yasishuke chini ya 75% wanakupa supplement kama adhabu ya utoro kwa kuzingatia ilo mwanafunz hana budi kwenda chuo na kuigia clas kwa kuogopa supplement...so ningeshauri vyuo vingine vingeiga sheria kama izo ili kupunguza wimbi la utoro vyuon
 
Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,645
4,482
Tatizo kubwa vyuo vikuu havina walimu! Mark my words!

tatizo ni nchi kukosa sera ya taifa. Haya mambo ya kutekeleza sera za magenge ya wahuni ndo matatizo yake. Wakiona watoto wao hawapati special schools wanasema tuzifute ile wapeleke watoto wao kirahisi, degree zao hazitambuliki na wana udsm wanaunda tcu ili kupitisha, watoto wao wanapata div 3 na 4 hawapati vyuo tcu inapewa kazi ya kupachika watoto wao udsm, muhas, sua etc na heslb ni genge la kuzuia vizazi vingine vya kina lisu,mdee, mnyika nk visiwepo. Wawepo walimu na wanasayansi wasiofanya praktical. Bila kuwa na sera ya taifa ambayo itatekelezwa na kunadiwa na yeyote hatufiki popote.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,833
Jaman kuhusu clas attendenc ni tatizo la chuo chenyewe kutokuweka sheria mahususi kuhusiana na ilo...ukiangalia vyuo kama st.joseph groups of institute wana sheria madhubuti na kali ktk suala ilo kwan ukiwa kama mwanafunz ktk vyuo vya lazima uattend chuo kila siku na tena unatakiwa mahudhurio yako yasishuke chini ya 75% wanakupa supplement kama adhabu ya utoro kwa kuzingatia ilo mwanafunz hana budi kwenda chuo na kuigia clas kwa kuogopa supplement...so ningeshauri vyuo vingine vingeiga sheria kama izo ili kupunguza wimbi la utoro vyuon
St. Joseph Groups of Institute ni chuo binafsi si cha serikali. Hali kadhalika chuo cha SAUT nilichokiandika hapo kwenye uzi huu ni chuo binafsi kinachomilikiwa na kanisa ndio maana wameanza kubana ubora wa wanafunzi badala ya kuwa na wahitimu waliojipakaa tu elimu na kujivika majoho bila kupata elimu stahiki.

Tatizo ni mfumo wa elimu nchini ambao utaratibu wa mfumo huo unaundwa na kuendeshwa na Wizara ya Elimu. Wizara ndiyo inayotoa utaratibu, mwongozo, sheria na maelekezo na ndio wenye kutoa mikopo kwa wanavyuo. Hapo St. Joseph wanafanya hivyo ni kwa sababu ni taasisi binafsi.

Wengi wa maprofesa wamesoma nje na kuona namna vyuo vya wenzetu wanavyofanya, nashangaa kwa nini wawapo katika jopo lao hawapeleki mapendekezo wizarani kufanya tathmini bora ya kuwa na mfumo unaoeleweka badala ya huu wa sasa ambao ni sawa forward anayepiga mpira bila kulenga goli, piga bora liende kukwepa fedheha na kubaki kubeba lawama.
 
sawa mkuu nimekuelewa....
 
UKI

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
692
170
mkuu nashukuru umelileta hili suala watu waelewe nahisi hata wahariri wavivu watachukua moja ya point kuweka kwenye magazeti. yao jamani mimi mtanzania tulizoea kusoma vyuo vya bongo huwezi amini niliamua kufanya transfer kwenda nje hukoooo nikajua elimu ni kama bongo sio siri sikuhudhuria class siku mbili mwisho wa mwezi nilikutana na bonge la email la warning na niandike maelezo sio chini ya 500 words kwanini sikuhudhuria class na wakasema tutakureport uhamiaji na utaondolewa hapa nchini mara moja huwezi amini nilifikiri utani kumbuka wenzetu ukiwa mwanafunzi unapewa electronic ID card ukiingia tu class unaweka ile ID kwenye checking point so inasoma umeeingia class na ukimaliza napo unatakiwa u checking out, wenzetu wako mbele kwa kumuandaa mwanafunzi halafu home huwa tunajiandaa kusoma kufanya mitihani tu ila ukweli final exam sio kigezo tosha cha kumpima mwanafunzi, assignment, presentation za wenzetu zinavyosimamiwa tafikiri unaenda kuomba kazi za mkurugenzi mkuu wa tanesco au BOT kumbe ni mwanafunzi tu unakuta malecturer wengine kibao wako kwenye class wanawasikiliza na mbaya ukutue unafanya presentation ya moja ya company ambayo iko hapo nchini (mfano share value, au strategic analysis ya hiyo co, etc) huwa wanakuja hadi wawakilishi wao waone kama kwenye umefanya research ya ukweli au lah , jamani watu wawe wanajikongoje waende hata kusoma nje waone watu walivyo serious na elimu zao.
 
ndupa

JF-Expert Member
Jan 25, 2008
4,403
131
mada nzuri....kwa kweli kwa hapa bongo bado tuko nyuma...bila kujali ni chuo kikubwa au kidogo,kinachojulikana au hakijulikani!!! inashangaza sana mtu unaingia masomo ya uhandisi au udaktari unakuta vifaa havipoau vipo lakini havifanyi kazi!! sasa hapa tunatarajia nini?? uelewa?? au kujisifu ooohh nimesoma udom,udsm sijui nini!!! mi nadhani nchi yetu hasa viongozi akili zao zimepungukiwa akili!!! wao kila siku wanajitahidi kuingiza siasa kwenye elimu....kila siku wannajisifu wanaboresha elimu kwa kujenga majengo tuuu akatiwalimu na miundo mingine ni zero!!! kwa mtindo huu hakika hatutafika mahali zaidi ya kujisifia tuu na kwa kupewa ka degree ka kubebwa na kuhonga ch***p!!! wataalamu wanatoka vyuoni lichwani hakuna kitu unakuta mtu ni mhandisi lakini ni ma theory tu yamejaa kichwani...sasa hali hii inashangaza na sijui tunaenda wapi....ma proffesor wanaacha kazi zao na kujiingiza kwenye siasa,alafu kila siku tunalalamika wahadhiri hasa wa science vyuoni ni wachache!!! inasikitisha ila ndo tz bwana...mungu ibariki tanzania,mungu laani mafisadi!!!! nawasilisha....
 
samilakadunda

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
1,780
349
Tatizo kubwa vyuo vikuu havina walimu! Mark my words!

Daah hapo umenigusa! Tuna mwalimu wetu wa geography hufundisha part time kutoka udsm, ukweli hatuwezi fika anakuja darasani mara 4 kwa mwezi hana course out line, yeye akiingia na powerpoint yake ni kuponyeza tu,na hataki kuulizwa maswali! Tumechokaa!
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,833
mkuu nashukuru umelileta hili suala watu waelewe nahisi hata wahariri wavivu watachukua moja ya point kuweka kwenye magazeti. yao jamani mimi mtanzania tulizoea kusoma vyuo vya bongo huwezi amini niliamua kufanya transfer kwenda nje hukoooo nikajua elimu ni kama bongo sio siri sikuhudhuria class siku mbili mwisho wa mwezi nilikutana na bonge la email la warning na niandike maelezo sio chini ya 500 words kwanini sikuhudhuria class na wakasema tutakureport uhamiaji na utaondolewa hapa nchini mara moja huwezi amini nilifikiri utani kumbuka wenzetu ukiwa mwanafunzi unapewa electronic ID card ukiingia tu class unaweka ile ID kwenye checking point so inasoma umeeingia class na ukimaliza napo unatakiwa u checking out, wenzetu wako mbele kwa kumuandaa mwanafunzi halafu home huwa tunajiandaa kusoma kufanya mitihani tu ila ukweli final exam sio kigezo tosha cha kumpima mwanafunzi, assignment, presentation za wenzetu zinavyosimamiwa tafikiri unaenda kuomba kazi za mkurugenzi mkuu wa tanesco au BOT kumbe ni mwanafunzi tu unakuta malecturer wengine kibao wako kwenye class wanawasikiliza na mbaya ukutue unafanya presentation ya moja ya company ambayo iko hapo nchini (mfano share value, au strategic analysis ya hiyo co, etc) huwa wanakuja hadi wawakilishi wao waone kama kwenye umefanya research ya ukweli au lah , jamani watu wawe wanajikongoje waende hata kusoma nje waone watu walivyo serious na elimu zao.

Hiyo ndiyo hali ya elimu kwa wenzetu wambao wanahakikisha unapohitimu unakuwa mhitimu kweli na umeiva vilivyo. Mwanachuo upo chuoni kwa ajili hiyo na mwanachuo anatakiwa atumie muda wake huo kwa ajili hiyo na chuo kihakikishe uwajibikaji wa mwachuo ipasavyo katika utaratibu wao kuhakikisha umepata elimu uliyotarajiwa, la sivyo kusajili tu chuoni si kupata elimu ya chuo, maana baadhi yetu tuna mazoea ya kusema nimekuwa mwanachuo wa chuo fulani.
 
Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,236
530
Kwa wale waliobahatika kusoma barua ya A K Opicho kwenye The East African la 1-7 Dec, watakubaliana na mleta uzi -- something's very wrong with the whole education system. The rotten-ness and lack of scholaristicism does not start at university (though it ought be more pronounced at this level), but is down rooted from the early stages of education system.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom