vyuo vya ualimu

kim jung shik

Senior Member
Mar 26, 2014
129
23
jamani naomba kujuzwa qualifications zinazotakiwa ili kujiunga na mafunzo ya ualimu kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kwasababu kwenye tangazo wameandikwa mpaka waliopata division III So sijaelewa vizur naomba msaada wa kuelimishwa
 
Due to kawambwa juz wakimuhoj alsema kuwa kuanzia div one ya 7 mbaka dv 3 ya 31 watachagulwa kidato cha tano afu hao kuanzia 4 ya 32 n vyuo . more info moe.go.tz.
 
jamani naomba kujuzwa qualifications zinazotakiwa ili kujiunga na mafunzo ya ualimu kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kwasababu kwenye tangazo wameandikwa mpaka waliopata division III So sijaelewa vizur naomba msaada wa kuelimishwa

Maelezo hayo ni chini ni kwa grade A
 

Attachments

  • 1397818077757.jpg
    1397818077757.jpg
    80.4 KB · Views: 1,340
  • 1397818092925.jpg
    1397818092925.jpg
    84.6 KB · Views: 1,287
  • 1397818105103.jpg
    1397818105103.jpg
    35 KB · Views: 685
Nilivyoelewa mimi aliyepata div3 form(science) huyu yeye atasoma dip kwa miaka 3
 
kwani daraja la 3A na A pekeake tofauti nn mpka iwe hvo

maelezo kwa diploma haya hapa au kama hauoni vizuri hizo picha nenda website ya wizara ya elimu..
 

Attachments

  • 1397818597835.jpg
    1397818597835.jpg
    67.3 KB · Views: 691
  • 1397818615754.jpg
    1397818615754.jpg
    60.9 KB · Views: 603
  • 1397818627774.jpg
    1397818627774.jpg
    61.1 KB · Views: 514
  • 1397818645085.jpg
    1397818645085.jpg
    62.5 KB · Views: 478
  • 1397818656431.jpg
    1397818656431.jpg
    62 KB · Views: 440
  • 1397818667687.jpg
    1397818667687.jpg
    14.4 KB · Views: 383
Jf mods tufanyieni msaada tusome vizuri hili tangazo yani likuzwe kidogo.

Mods wapo likizo:


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Simu: 022-2110146/2110150/2, 211679, Faksi: 022-2113271,
Tovuti:United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015

UTANGULIZI

Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni wale wenye ufaulu mzuri katika mtihani ya kidato cha NNE. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa alama 26 au 27 (mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mwaka 2013) watadahiliwa katika programu ya mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.

Aidha, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya ualimu na kufaulu mafunzo yao watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za Serikali.

VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/15.

1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA 'A':
MUDA MIAKA 2
(i) Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, , Kitangali, Mandaka , Murutunguru , Ndala , na Tarime.
(ii) Cheti Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya Kabanga, Kinampanda, Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
(iii) Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala na Mtwara (U)

Mwombaji awe:
Mhitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye ufaulu wa kiwango kisichopungua Daraja la III katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.

MAFUNZO KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA
2: AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI:-

MUDA MWAKA 1

Mafunzo katika vyuo vya ualimu Bustani, Kinampanda, Mhonda, Mpuguso, Mtwara (U), Nachingwea, Singachini, Tandala, Katoke na Sumbawanga.


1. Mwombaji awe:
(i) Amehitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na awe amefaulu kwa kiwango kisichopungua Daraja la IV kwa alama 26 au 27 (kwa mtihani wa mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mtihani wa mwaka 2013) kwa mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
(ii) Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.

Tanbihi: Watakaofaulu mtihani wa mafunzo rekebishi wataendelea na
mwaka wa pili wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti Daraja A

3: ELIMU MAALUM: MIAKA 2 katika chuo cha Patandi:-
Mwombaji awe:
(i) Mwalimu wa Daraja 'A' mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
(ii) Mwenye ufaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha IV.

Tanbihi:
Walimu wanaofundisha Elimu Maalum hata kama hawana mafunzo maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho uambatishwe).


MAELEZO MUHIMU

(i) Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;

(ii) Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;

(iii) Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja 'A' kwenye 'Selforms' wakati wanamaliza Elimu ya Sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;

(iv) Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;

(v) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training), OWM-TAMISEMI (PMORALG | Prime Minister's Office - Regional Administration and Local Government) na NACTE (The National Council for Technical Education)


(vi) Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;

(vii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.


Namna ya kutuma maombi:


a) Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO (online application) kupitia tovuti zifuatazo: www.moe.go.tz AUThe National Council for Technical Education

2. Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000 itakayolipwa kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizaraUnited Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training na Baraza la Taifa la Elimu ya UfundiThe National Council for Technical Education

Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia M - PESA kama ifuatavyo:
1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3. Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4. Weka LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5. Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6. Weka Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7. Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8. Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.


AU

b) Barua kwa:

KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
 
nenda hapa www.moe.go.tz
utapata maelezo yote niliweka hapo juu kama kwako hayazomeki vizuri..Lakini unaeza kuyazoom ukasoma na kuelewa

Hapo yapo kwenye PDF na watumiaji wa simu wengi hawajuwi kusoma pdf kwenye simu zao na wakati mwingine maandishi ya pdf hayaonekani vizuri kwenye simu. Nime-convert hiyo pdf kwenda ms-word na nimewawekea hapo juu.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI


Simu:022-2110146/2110150/2/211679 Faksi:022-2113271,
Tovuti:United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training


TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015


UTANGULIZI

Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni wale wenye ufaulu mzuri katika mitihani ya kidato cha NNE na SITA. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa
Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu tu.

Aidha, kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati wa takribani walimu 26,000 kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo Sayansi na Hisabati ili kuziba pengo hili. Nia ya Serikali ni kuwavutia wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi na Hisabati. Kuanzia mwaka huu wa masomo 2014/15 wanafunzi watakaojiunga na fani ya Ualimu kwa masomo ya Sayansi na Hisabati watagharimiwa na Serikali kupitia mfumo wa ruzuku na mkopo. Wanafunzi watakaokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza watapatiwa Ruzuku na wale wenye Daraja la Pili na la Tatu watapewa mkopo ili kuwasaidia katika masomo yao. Watakaofaulu mafunzo ya ualimu katika masomo ya Sayansi/Hisabati watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za
serikali.


VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka 2014/15.

1: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA: MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA UFUNDI:

MUDA MIAKA 2.


(i) Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Kleruu na Monduli.

Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa 'Principal Pass' mbili katika Masomo ya Sayansi na Hisabati.


(ii) Ualimu wa ufundi katika chuo cha ualimu Kleruu Mwombaji awe amehitimu: a. Mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2004 na 2010 kutoka Vyuo vya Ufundi, Au b. Mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA Level 6 au sifa linganishi (equivalent qualification) kati ya mwaka 2007 na 2013 kutoka chuo chochote cha Ufundi kinachotambulika na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).


(iii) Ualimu wa Kilimo katika chuo cha ualimu Monduli Mwombaji awe amehitimu: Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu 'Principal Pass' mbili katika somo la 'Agricultural science' na 'Biology', 'Chemistry' au 'Food and Nutrition'.




2: MAFUNZO MAALUM YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA KWA KIDATO CHA NNE MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA ENGLISH: MUDA MIAKA 3

Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati na English katika vyuo vya Butimba, Morogoro, Korogwe, Songea na Mpwapwa

Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu, na Credit mbili (yaani A, B+, B au C) katika masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza.

3: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA:
MUDA MIAKA 2.
(i) Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu.


Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango cha 'Principal Pass' mbili


(ii) Biashara katika vyuo vya Shinyanga na Kasulu Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja


(iii) Sanaa za Ufundi, Sanaa za Maonyesho, Muziki na Michezo katika chuo cha Butimba. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja


Tanbihi: Masomo ya 'Economics', Basic Applied Mathematics', 'General
Studies' na 'Divinity' hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au kumdahili mwombaji.

4: MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI STASHAHADA ELIMU YA
MSINGI: MUDA MIAKA 3)

Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu

Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 wenye ufaulu wa Daraja la I Daraja la Tatu katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.

Tanbihi: Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya 'Mathematics', 'Biology', 'Physics', 'Chemistry', 'Agriculture', 'Food and Nutrition', 'English' na Kiswahili na wahitimu wenye mahitaji maalumu.



5. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA:- MUDA MIAKA 2

Ualimu wa masomo ya Sayansi katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpapwa, Tukuyu, Songea , Butimba, Kleruu na Monduli

Mwombaji awe amehitimu:
Mwalimu wa Daraja 'A' aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja katika Masomo ya Sayansi na Hisabati; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.



6: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA (SEKONDARI):-
MUDA MIAKA 2.

(i) Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa, Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu.

Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na mwenye ufaulu usiopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja
katika masomo ya 'Biology, 'Chemistry' na 'Food and Nutrition.

(ii) Ualimu wa masomo ya Biashara katika vyuo vya Shinyanga, Kasulu

Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja 'A' aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua 'Principal Pass" moja na 'Subsidiary' moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.

(iii) Ualimu wa masomo ya Elimu Maalumu katika chuo cha Patandi
Mwombaji awe:

Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi ya ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili, Au

Mwalimu wa Daraja 'A' aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua 'Principal Pass' moja na 'Subsidiary' moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.


Tanbihi: Walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum kama wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili, n.k. ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).



7: MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA ELIMU YA
MSINGI: MUDA MIAKA 2:

Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja 'A' mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.



MAELEZO MUHIMU



(i) Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya
Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;


(ii) Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile
anachokipendelea zaidi;


(iii) Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za
mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
(iv) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika
vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)




(v) Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo
na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;

(vi) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE:The National Council for Technical Education na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.




Namna ya kutuma maombi:

a) Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO (online application) kupitia tovuti zifuatazo:United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training AUThe National Council for Technical Education

Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000 itakayolipwa kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara www.moe.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi The National Council for Technical Education

Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia MPESA kama ifuatavyo:

1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3. Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4. Weka LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5. Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6. Weka Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7. Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8. Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.

AU

b) Barua kwa:


KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
 
ninachoona mimi hapa ni majanga kwa private colleges, kwani div3 wataishia form five au watachaguliwa na vyuo vyao vya ualimu!.
 
kwhyo hapo wanaoenda vyuo vya ualimu ni hao wenye four za 32 had 34 sasa hiyo bridging course ni yanini?
 
Duuh Hapa Kazi Ipo., Ina Maana Hakuna Cha Kudownload Fomu Na Kujaza Ukiwa Nayo Mkononi Kama Enz Zile Za Nyerere Sasa Iv Kila Kitu Ni Kwa Mtandao.? Na Hii Ya Barua Vp Ukishaiandka Unaweza Kuituma Kwa Njia Ya EMS (Posta) Kwenda Kwa Mkurugenzi.? @wadau
 
ya kama uko mbali makao makuu ya wizara ya elimu yaani dsm so tumia njia hi ya ems ni nzuri xna b'se inafika kwa muda mfupi thnx
 
Back
Top Bottom