Vyuo Vikuu vingi Tanzania havina sifa- TCU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo Vikuu vingi Tanzania havina sifa- TCU

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Njowepo, Mar 11, 2012.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  [h=2][/h] Na Mwinyi Sadallah

  11th March 2012


  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TCU) imesema iwapo itasimamia ipasavyo sheria yake Vyuo Vikuu vya Tanzania vitalazimika kufungwa kutokana na kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri.
  Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Ithibati wa Tume hiyo, Dk Christine Hongoke, alipokuwa akizungumza na Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Makao Makuu ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam.
  Alisema kwamba TCU imebaini kuwa kuna upungufu mkubwa wa wahadhiri wenye sifa za kufundisha katika vyuo vikuu hapa nchini jambo ambalo ni kinyume na sheria.
  Alisema kwamba Vyuo Vikuu vya Tanzania vimekuwa vikinyang’anyana wahadhiri na kulazimika kuwatumia kwa zamu kufundisha wanafunzi kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
  Hata hivyo, alisema kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani imeanzisha utaratibu wa kusomesha wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya umma kwa kushirikiana na Shirika la DAAD la Ujerumani.
  Alisema kwamba Ujerumani imekuwa ikitoa nafasi za masomo (Skolashp) ngazi ya Shahada ya Uzamili mpango ambao ulianza utekelezaji wake mwaka 2009.
  Hata hivyo, alisema pamoja na Ujerumani kutoa hofa ya nafasi 20 za masomo ya ngazi ya shahada fursa hiyo haitumiwi ipasavyo kutokana Tanzania kushindwa kupeleka wanafunzi.
  Akitoa mfano, Dk. Hangoke alisema mwaka jana Tanzania ilipeleka watu sita kati ya nafasi 20 kutokana na wahadhiri kutojitokeza kuomba nafasi hizo.
  Dk Hangoke, alisema kwamba tangu kuanza mpango huo tayari wahadhiri 32 kutoka vyuo vikuu vya umma wamenufaika na mpango huo wa kusomeshwa nje ya nchi.
  Alisema kwamba tangu kuazishwa kwa TCU jumla ya vyuo vikuu 26 vimesajiliwa vikiwemo vyuo vikuu vishiriki Tanzania.

  MY TAKE
  Kama havina sifa na mkuu unaendelea kuwepo kwenye icho kiti huoni kuna haja ya wewe kujiuzulu bse unalea ubovu huo wa kuwa na uhaba wa wahadhili na no penalties
  Upande wa pili izo scolarships mngekuwa mnazitangaza kuna vijana wengi wako tayari kwenda kusoma tatizo mnakaa nazo kwenye mafile yenu mkingoja wanenu na ndugu zenu waende soma
   
 2. ma2mbo

  ma2mbo JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  kuna chuo kinaitwa Tanzania Institute of Project Management kipo kinondoni,kina wahadhiri wawili tu,ila kinatoa hadi masters na tcu wanaangalia tu.
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Rushwa, rushwa, rushwa!! If no rushwa, kwa nini uache maovu yatendeke?
   
 4. J

  John W. Mlacha Verified User

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  wanapewaga cha juu hawa nawajua
   
 5. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  imtu kinatoa hadi phd ila hakina teaching hospital, no lecturers, aafu tunasema tunataka kuingia kwenye jumuiya. Huku ni kudanganyana.
   
 6. kiagata

  kiagata Senior Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  sharti la kusajiri chuo lazima mambo kadha yafuatwe kama:- wahadhiri,vitabu,mazingira na nk.Sasa kama hayo mambo hakuna na mengineyo basihapo kuna tatizo labda rushwa au uzembe wa ufuatiliaji.Na kodi wanayolipa serikalini mmnachukua bure.Fungeni tuanze upya.
   
 7. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hii ndio Tanzania?????
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hakuna haja ya kuacha chuo ambacho hakikidhi matakwa ya watanzania.
  TUnahamishia UPE katika University level, na wakuu wanaangalia tu.
   
 9. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Shame on her face, saying that Tanzanians did not apply!
  She should inform us as well as to when and where it was advertised.
  This is shameful statement from the Director.
  Watanzania.... kila kitu kwetu ni kimyume kabisa.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna jamaa zangu kama watatu wanasaka PHD kwa udi na uvumba alafu huyu mtu mzima anasema PHD opportunities zinakuwa wasted.Next time zitupe umu JF uone kama kutakuwa nafasi itakayokuwa wasted!
  Ivi unajua tungekuwa serious iyo statement tayari uyo jamaa angekuwa kapigwa chini.
  Ila anajua serikali legelege haiwezi mpiga chini
   
Loading...