Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Kwa muda sasa, kumekuwepo kelele nyingi za Wadau wa Elimu nchini juu ya kuzorota kwa Mfumo wa Elimu wa Tanzania lakini kelele hizi zimesikika sana hasa katika Awamu ya V ya Rais John Pombe Magufuli. Kwa haraka haraka, unaweza ukaingia kwenye mkumbo wa kudhani, Sera za sasa za Serikali ya Awamu ya Tano, ndizo zimeifikisha hapa elimu ya Tanzania. Wengi wamekuwa wakiinyoshea Sera ya Elimu Msingi Bila Malipo kuwa, ndio chanzo cha kuporomoka kwa elimu ya Tanzania.
Hata hivyo, mi naona kelele zimekuwa nyingi baada ya Serikali kuboresha kwa kiwango kikubwa shule zake, ikiwemo kuondoa karo na hivyo kuvutia wazazi wengi kuhamishia watoto wao katika shule za umma kutoka shule binafsi na hivyo kuathiri sana sekta binafsi hasa katika kipindi hiki cha kupaka vyuma grisi. Je, kushuka kwa elimu kuhusishwe na Rais John Pombe Magufuli, ama a Magufuli ndiye anayeitoa shimoni na hivyo kuwawafumbua macho Watanzania, juu ya jinsi elimu yetu ilikuwa imeshadharaulika?
Jibu: Kwa kawaida, Mfumo wa Elimu kwa dunia nzima, umetengenezwa katika umbo la Pyramid kuanzia chini hadi juu Killeen, ambapo wanafunzi huanza wakiwa wengi na kadri madarasa yanavyopanda ndivyo pia idadi ya wanafunzi hushuka. Hivyo, wanafunzi wa shule za msingi huwa wengi kuliko wale wa shule za sekondari, kama ambavyo nao ni wengi kuliko wa vyuo vikuu.
Hata hivyo, kwa Tanzania, kuna sehemu kama Nchi tuliamua kujichanganya wenyewe na kuiacha hiyo kanuni kwa kuendekeza kupanua magoli na hivyo kuruhusu wenye ufaulu mdogo kuchaguliwa kwenda chuo kikuu. Tumeruhusu kuwepo kwa utitiri wa Vyuo Vikuu vya Private vinavyodahili wanafunzi waliopata hadi Principals za D. Hao watu wakimaliza Vyuo, ndio huwa wa kwanza kupata kazi kwani huwa tayari kuhonga wakijua hawakuwa na sifa kama za wenzao. Hali hiyo huwaacha vipanga wakirandaranda mitaani bila ajira.
Mfano: Kwa mwaka 2018, Tanzania ina wanafunzi wanaotarajiwa kufanya Mtihani wa STD IV - 1,609,000; Mtihani wa Std. VII - 965,000; Mtihani wa Kidato II - 547,000; Form IV - 440,000; na Form VI - 80,000 (wameshafanya).
Ajabu ni kuwa, mwaka 2014, jumla ya Watahiniwa 196,805 (68%) walifaulu Mtihani wa Kidato cha IV, kati ya Watahiniwa 235,227 waliofanya Mtihani huo. Hata hivyo, ni Watahiniwa 73,832 pekee, sawa na asilimia 30% ndio waliopata madaraja ya: distinction, merit na credit.
Wanafunzi hao 73,800 ni miongoni mwa Wahitimu 75,116 waliofanya Mtihani wa Kidato cha VI mwaka 2017, ambapo wanafunzi 58,556 sawa na asilimia 93%, walifaulu Mtihani huo.
Kama asilimia 93% wanafaulu Mtihani, kuna haja gani ya Mtihani huo? Na in fact, hao ni waliopata I - III lakini ukijumlisha na wale waliopata ushindi wa Division IV (huwa wanaenda vyuo vya diploma), utakuta possibly asilimia 99% ya Watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha VI, hufaulu.
So, huo ni Mtihani? Je, hatujicheleweshi tu sisi wenyewe bila kujua? Chanzo cha kupunguza point za kujiunga na chuo ni nini? Mlitaka wote waende Chuo Kikuu?
Mchawi amejificha hapo. Vyuo vikuu vilitaka hela za mikopo na zikawa tayari kudahili wanafunzi wenye makisi za chini. Haiwezekani wanafunzi wanaotoka stage moja ya kielimu kwenda nyingine wawe wengi (40,000 wa Mwaka wa Kwanza watakaopata mkopo - 2018) kuliko ambao hawakuchaguliwa kwenda Vyuo vikuu (58,000 - 40,000 = 18,000) Chukua tena hao 18,000 utoe wanachuo ambao hawakuomba/Hawatapata mkopo, utapata ambao hawakwenda Chuo Kikuu.
Hiyo inamaanisha wanaoingia kusoma kazi za utaalamu wa kati (diploma) ni around 10,000 pekee. Hapa ndipo kuna tatizo.