Vyuo vikuu kuanza November

Vyuo vikuu kuanza November

Joined
Apr 30, 2013
Posts
93
Reaction score
19
SERIKALI imetoa waraka unaovielekeza vyuo vikuu vyote nchini, kuchelewa kuanza muhula wa masomo kwa mwezi mmoja, ili kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa waraka huo, badala ya kuanza Oktoba kama ilivyozoeleka, muhula kwa vyuo vikuu vyote katika mwaka huu, utaanza juma la kwanza la Novemba, baada ya kumalizika uchaguzi huo wa madiwani, wabunge na rais.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, alisema vyuo hivyo vitafunguliwa kati ya Novemba 4 na 5.
Hata hivyo alisema hatua hiyo haitokani na uchaguzi na kwamba inatokana na mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na serikali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.

"Fedha zinazohitajika kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi mwaka huu ni nyingi sana, zinafikia Sh250 bilioni ni pesa nyingi, kwa hiyo tunaandaa utaratibu mpya ambao tunatarajia utakuwa umekamilika ifikapo Novemba 3,"alisema Waziri.

Kawambwa alisema hata mwaka wa masomo uliopita, vyuo vikuu vilifunguliwa Oktoba 25 na kwamba kuwa tarehe hiyo haipishani sana na ya kufunguliwa kwa vyuo hivgo katika mwaka huu.

"Tatizo kila kitu kinachofanywa sasa na serikali kinahusishwa na uchaguzi kwa sababu tu tunaelekea kwenye uchaguzi lakini hili la kufunguliwa kwa vyuo Novemba, halina uhusiano kabisa na uchaguzi,"alisisitiza Kawambwa.

Waziri Kawambwa alisema utaratibu wa mpya wa utoaji wa mikopo ambao hakuwa tayari kuuweka wazi, utasaidia kuharakisha ulipwaji wa mikopo hiyo ili wanafunzi watakaporejea vyuoni, wakute mikopo hiyo ikiwa tayari.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Profesa Mayunga Nkunya, alithibitisha kupata taarifa kuhusu hatua hiyo.

Profesa Nkunya alisema, katika kipindi cha Oktoba, wanafunzi wengi watakuwa wakishughulia mikopo kutoka bodi ya mikopo na kwamba halitakuwa jambo zuri kazi hiyo isiingiliane na uchaguzi mkuu.

Chanzo: Varsity College Network
 
Duh, tumefanya kaz bure, tumehamasisha wanavyuo kujiandikisha bt hawatapiga kura.

Goli la mkono in the making
 
Raisi wa TAHLSO huwa anafanya kazi gani?
 
Mmmmmhh...
Nahisi kitu hapa!
Nahisi kama kuna kamchezo ka kisiasa hapa sikaelewielewi hapa!
 
Hata 2010 vyuo vilifunguliwa november wala sishangai maana dila ya tz chini ya ccm
 
Duh, tumefanya kaz bure, tumehamasisha wanavyuo kujiandikisha bt hawatapiga kura.

Goli la mkono in the making
Kwani huko watakakokuwa hawaruhusiwi kupiga kura?
 
Raisi wa TAHLSO huwa anafanya kazi gani?
Kumbe TAHLISO nanyi mna RAIS wa kuwafanyia kazi?. Alishindwa hata kufanya jitahada za kufuatilia boom la wanafunz Udom ambapo pia yeye ni RAIS wa Kitivo Cha Elimu hapa Udom mpaka yalipochukuliwa maamuzi ya kumpindua na kumsimika shujaa mtetez aliyoongoza maandamano haki ikapatikana huku jamaa akiwa kimya km kabanwa. mdomo.
 
SERIKALI imetoa waraka unaovielekeza vyuo vikuu vyote nchini, kuchelewa kuanza muhula wa masomo kwa mwezi mmoja, ili kupisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

................................

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, alisema vyuo hivyo vitafunguliwa kati ya Novemba 4 na 5.
Hata hivyo alisema hatua hiyo haitokani na uchaguzi na kwamba inatokana na mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na serikali katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.

..............

.......................

"Tatizo kila kitu kinachofanywa sasa na serikali kinahusishwa na uchaguzi kwa sababu tu tunaelekea kwenye uchaguzi lakini hili la kufunguliwa kwa vyuo Novemba, halina uhusiano kabisa na uchaguzi,"alisisitiza Kawambwa.

........................

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), Profesa Mayunga Nkunya, alithibitisha kupata taarifa kuhusu hatua hiyo.
Profesa Nkunya alisema, katika kipindi cha Oktoba, wanafunzi wengi watakuwa wakishughulia mikopo kutoka bodi ya mikopo na kwamba halitakuwa jambo zuri kazi hiyo isiingiliane na uchaguzi mkuu.

Hapo "bolded/red" pana "ukinzani"....! What a strange world we live in....!
 
duuh,cie ambao hatujaenda jkt ktaa kta2koma,yan daaaah!
 
Wengi watakosa mikopo,hivyo huenda wanaepuka wapinzani wasije wakaigeuza agenda ya kisiasa.Huenda wanataka iwe November ili uchaguzi uwe umeisha watu wakipiga kelele wakutane na washawasha.Ni hisia zangu tu!
 
2010 hiyo. Mwaka huo nilifanikiwa kumpigia kura rais tu, mbunge na diwan sikufanikiwa. Matokeo yenyewe ya rais hayahojiwi hata mahakamani, hivyo wanafunzi wataishia kumpigia huyo ambaye hata matokeo yakipinduliwa hayatabadilishwa
 
Hapo mjue hakuna mkopo serikali haina pesa au watakao pata wachache😎
 
Back
Top Bottom