Vyuo vikuu kama shule za kata



Kumbe ni tatizo lako la u coservative. teh teh teh, Sio tatizo la UDOM. Kuna senteso umesema yani inazifanya hoja zako zote kua zero.
 


Nimekuelewa ila wanafunzi wa UDSM pamoja na kuchaguliwa na marks za juu ni vihiyo kuliko maelezo. Kwa nini usinunue vitabu vyako. Baada ya kugraduate utaacha kabisa kujisomea? Kitu kingine asilimia kubwa ya wanafunzi wa mlimani ni wavivu katika suala zima la matumizi ya internet! Nawajua wengi lakini sitaki kugeneralize maana wazuri wa computer pia wapo! Sitaki kuisifia SUA kwa vile nimesoma pale lakini ina wanafunzi bora zaidi hata mkikutana kazini. Conflict of interest declared lakini haikuathiri ukweli wenyewe!
 

Naomba niadike chini ya maelezo yako. Naamini umeandika ukweli kwamba wewe ni mmoja wa wanafunzi wa UDOM. Namaanisha una taarifa rasmi za nini kinatokea hapo UDOM.

Binafsi nina maelezo ya nini kinachoendelea hapo UDOM kwa maelezo ya wanataaluma ninaofahamiana nao.

Ni sifa kubwa kwa serikali kuanzisha chuo kikubwa kwa kiwango hicho na kuondoa ukiritimba wa elimu ya chuo kikuu. Lakini ni aibu kubwa kwa serikali kuanzisha Chuo kwa mtindo uliotumika. Hii ni miaka 50 baada ya nchi kupata uhuru, hatuna sababu ya kujiuliza UD ilianzaje. The past has gone! Baada ya miaka yote hii hatuwezi kuanzisha chuo utadhani U-profesa ni jambo geni nchi hii.

Tatizo kubwa la UDOM ambalo nimelisikia kila wakati ni ubovu wa Utawala. Utawala uliopo waonekana ni wa kisiasa badala ya uwezo wao. Kwa ufupi mwanafunzi uko sahihi kusema kuna mambo ya kisiasa badala ya taaluma. Ni chuo pekee ambacho kila wakati utasikia wakuu wakisifiwa kwa kazi nzuri. Kazi nzuri inayotajwa ni ujenzi wa 'majengo ya kisasa.'

Taarifa nilizonazo pia kila mwalimu mzuri aliyeshawishiwa kuhamia UDOM ameishia kukimbia na kurudi alikotoka. Yaonyesha kunyanyasa ni sehemu ya sifa za watawala wa UDOM. Sasa ukiona mtawala wa Chuo kikuu (UNiversity) ananyanyasa wanataaluma kwa mtindo tunaousikia, hapo kuna tatizo la msingi ambalo serikali iliyo makini ilistahili kuliangalia. Ukimya wa serikali umesababisha watu kuhisi suala la kidini pia kutumika kwa nguvu sana. Samahani sana lakini nilisikia pia kwamba baadhi ya wanafunzi wanapewa admission na baadhi ya staff wanaajiliwa kwa sababu tu ni wa dini fulani. Nahisi makamu mkuu wa chuo anafahamu malalamiko hayo maana kuna wakati alijitokeza redioni kukanusha kuwepo kwa tatizo hilo.

Sasa tena unasema kuna vyeti vya CCM. Maana inaonekana degree za UDOM ni za utiifu kwa CCM! Naanza kuwa na wasi wasi kwamba watakaopewa vyeti mwaka huu kwa mara ya kwanza, huenda wataajiliwa kwa lazima ya CCM. Tusubiri maana hayo yalikuwa yakitokea kule USSR, ile miaka ya zamani.

Tukubali kwamba UDOM bado hakijawa Chuo kikuu (University) ya kukimbilia kwa yeyote anayehitaji elimu ya kweli. Pamoja na kilio cha wengi juu ya kushuka kwa viwango vya elimu na hadi vyuo vikuu, lakini nahisi UDOM kuna matatizo ya ziada ambayo yanaonekana hayatatatuliwa hivi karibuni.
 
Eliakeem ni kweli Roma haikujengwa kwa siku moja na kama warumi wangekuwa ni mtazamo kama huu basi hiyo Roma isingejengwa kabisa. Wadau tuliongelea suala la wabunge vilaza, lakini wengi walikuwa mitazamo hafifu, fikiria Mr Ngonyanyi Stephen Ngonyani yupo bungeni kuchangia bajeti ya wizara ya sayansi na teknolojia kweli mbunge huyu atakuwa na wamazo kuchangia kuboresha elimu ya juu wakati yeye ni kilaza? Umenukuu Mwl. Nyerere sawa kabisa kwani huo ndio umasikini unaoikabili CCM. CCM imejigamba sana kwa kufanikisha sera wamekitumia UDOM kama moja ya mafanikio yake kwenye sekta ya elimu lakini wamesahau kuwa chuo si majengo pekee yake huwezi kujigamba kuwa una chuo kikuu wakati huna walimu na zana kufundishia, jamani tupo karne ya 21.
 
Acheni watu wasome, hayo ndo maendeleo yenyewe. Nyie mnataka mwe na chuo kimoja kama cha enzi zile??

Acheni hizo, na uhakika mtu aliyefika chuo kikuu hata kama kipo chini ya mwembe ana uelewa mkubwa wa kupambanua mambo kuliko yule wa LY.
Wewe kwa nini ulikimbilia nje ya nchi kutafuta hiyo elimu badala ya kuitafuta hapa udanganyikani? Acha kupotosha watu hapa. Angalau wacha wengine wachangie si watu wa aina yako!
 
Kutoka kwa wachangiaji kuna hoja mbili pingamizi
1. Tuwe na vyuo watu waende chuo bila kujali kiwango cha elimu
2. Tunahitaji wasomi wa vyuo vikuu wapikwe waive.

Kwa kweli hoja namba moja ni kuogopwa kama ukoma. Yaani tudilute elimu ili tuwe na numbers?

Mlimani ya miaka ya sabini ilikuwa kitovu cha elimu, watu wanasoma na kuelimika. Msomi kama ku-challenge na kuelezea your side of teh story huwezi ni kufanya ni upuuzi mtupu.

Nasubiri nione hizo voda faster za UDOM

Wake up guys!
 

hio ndugu yangu sio zamani tu mpaka saivi my self nipo russia sitishi but thr are some fellow tanzanians ... Taking engineering and medicine in short warusi wanawakubali and sio warusi pekee hata wanafunzi wa nchi nyengine wanatukubali,,,,,
 
Acha u conservative, Nafkiri wewe ni mmoja kati ya wale watu ,Wanaofikiri mtu aliyemaliza UDSM ndio msomi, waliobaki wote ni FEKI.:becky:
 
Mkuu,
Mie nakusupport hundrend percent...hii elimu sijui itatupeleka wapi..mfano mwingine ni pale Mzumbe kampasi ya Dar ...wanachukua wanafunzi wengi ili mradi madarasa yajae...kuna kila aina ya wanafunzi wengine hta hizo degree zao au advance zao hazieleweki ili mradi tu wapate wanafunzi..hamna restriction kwamba ni GPA ngapi uweze kuingia kwa ajili ya Masters ni km zombazomba tu unakuta mtu na GPA ya 2..halafu nanaingia pale na masters yap one yeat the tayariii Du yaani ni hatari...
Lingine ni jinsi wanafunzi wanavyodesa material za wenzao na kukopy material...ktk mitihani unakuta mtu ni secretary wenu mko nae masters...sasa hapo sijui inakuwaje bosi na secretary ngoma droo..
Jambo lingine hizo masters za kuunga unga za walimu wetu pia zinafanya product za undergraduate students kuwa bomu ukimwita kwenye interview..graduate majibu yake ukimuuliza swali km tell about yourself au what is your streaght unaweza kutoa machozi ni aibu..inabidi Elimu yetu ya Vyuo vikuu ziboreshwe ili product ziwe compettive...
 

JK ni graduate wa UDSM wa 1970s lakini mbona hawezi hata kupambanua mambo?
 

Nimependa upembuzi wako. Kwani definition ya Chuo Kikuu ni ipi? Ni majengo Mazuri? Je Ni ni itofauti kati ka chuo kikuu na Shule za sekondari?
Hayo ndo ya msingi hapa. Tanzania ndiyo tuna uhaba wa watalaam katioka nyanja mbalimbali Lakini si kigezo cha kufanya mass production ya wasomi! Mimi ningefurahi kama Wangeruhusu ama Ku import Maprofesa na madakatari wa nje kuziba pengo badal ya kuwatumia Ma TA kUFUNDISHA!! Na hii imetiwa chumvi na vyuo binafsi huko ndo kumeoza. Kuna jamaa ambaye sidhani hana hata degree. Na ni senior Lecturer katika one of the chho kikuu binafsi na anaotoa wanafunzi wenye shada First class GPA 4.9! na makampuni yanapotoa nafasi katika young graduates wanaangalia GPA sasa 4.9 Utashindana naye nawe Upper ama lower seconda ulioipta ya mbinde? Sijui Hili Bomu lakini litatulipukia. One sign ni kuwa kazi nyingi za maana nje nchi tutasikia hadithi, na utandawazi huu ukitangaza nafasi za kazi mtanzania hatiii mguuu!! akiitwa interview madudu!! TUNAJIKAANGA KWA MAFUTA YETU WENYEWE!:confused2:
 
Taifa kuelemika ni jambo la msingi,na hupatikana kutokea vyuo vikuu,hivyo ongezeko la wanaohitaji elimu,kunahitaji ongezeko la vyuo vikuu vipya au upanuzi wa vyuo vilivyopo bila kuadhili ubora na viwango vya elimu husika.Lakini elimu ya vyuo vikuu ni endelevu haianzii chuo kikuu inatokea elimu za msingi,sekondari n.k.Walimu wakutosha wenye sifa zinazokidhi mafunzo ni nguzo mmoja wapo.Vitendea kazi vya kutosha kwa kumuwezesha mwalimu na mwanafunzi kufikia malengo.Mishahara,posho,malazi,usafiri na vivutio mbali mbali kuvutia mwalimu,bila vivutio mwalimu mahili anatafuta green pasture.Usishangee kuona walimu mahili wamekimbilia kwenye siasa kwani siasa inalipa,na kazi ya ualimu ni ngumu kweli.Kwa ujumla elimu inahitaji nia na mtaji mkubwa wa kuiboreshesha toka chekechea hadi vyuo vikuu,vinginevyo tutakuwa na wahitimu wengi wasiokidhi matakwa ya sasa.Kupanga ni kuchagua elimu bora au bora elimu?
 


Mkuu uko sawa kabisa hapo, ila sasa hilo je, serikali ipo tayari kulitekeleza? ni kweli kwa chuo kikuu sio majengo mazuri lakini ukumbuke kuwa majengo ni sehemu muhimu ya chuo ili kuwe na mazingira mazuri ya kutoa hiyo elimu bora. SAsa tusipokuwa na majengo yanayokidhi mahitaji, tutarudi kule kule kama UDSM ambapo wanafunzi wengine wananing'inia nje ili kumsikiliza mwalimu!
 

Mkuu nadhani hakuna aliyesema hapa kwamba watu waende tu chuo kikuu bila kujali kiwango cha elimu...hiyo itakuwa uendawazimu!

Knachozungumzwa hapa ni kwamba tusibeze juhudi ambazo zimefanyika hadi sasa katika kuboresha na kuongeza nafasi za wanafunzi watanzania kupata elimu ya chuo kikuu ambayo kwa wengine bado inaonekana ni anasa na ukiritimba flani hivi!
 
Hivi chuo ni maprofesa tu?
Masters za ungaunga zikoje hizo?
Ni chuo gani duniani ambacho mtu mwenye master hafundishi chuo kikuu?
Elimu ya chuo kikuu inafanana na ya kata kivipi?
Vifaa gani hakuna katika vyuo vikuu?
Main topic ya thread yako ni nini?
Hakuna kitu hapo!
 
Ndio maana unafeli wewe.
 

Sio kweli kwamba wanafunzi wote wanaweza kujinunulia vitabu ilhali ni ghali chukulia mfano wa kitabu kimoja cha akaunting kinaweza kukonsume meal yako ya mwezi,achilia mbali matumizi ya internet.mi naona kuwa bado ubora wa vyuo vikuu hapa nchini vinapishana japo kuna vingine vinakuja juu kwa kasi naona wadau mmekomalia only udsm, na sua na udom.kuna vingine tembeeni muone na qualities zao
 
Kumbe ni tatizo lako la u coservative. teh teh teh, Sio tatizo la UDOM. Kuna senteso umesema yani inazifanya hoja zako zote kua zero.

Mkuu,
Sijui ni kwa nini unakuwa hivyo. Kwa nini unapingana na kila mtu anayekosoa serikali au institution ya serikali?

Siyo vizuri kuwa na majibu ya kudumu kwa kila swali. Jaribu kuangalia aina ya challenge. Siyo siri kwamba serikali zetu hizi hazifanyi kazi vyema na ndiyo maana hatuelekei tunakotaka.

Sasa Mkuu kwako wewe, unaonyesha kana kwamba serikali hii ni safi, ni perfect, ni supper kuliko tunavyoiona. Ni kweli hiyo mkuu?

Zipo njia za kutimiza wajibu wa kumtetea mtu au kitu kama sehemu ya kazi yako na kuwaonyesha watu kwamba uko reasonable, uko fair. Siyo hivyo mkuu.
 
Kuanzisha na kufungua utitiri wa vyuo is ok as long as the quality of education ktk hivyo vyuo iwe ya kueleweka. Ni bora kungekuwa na Accreditation Board ambayo ita-monitor mwenendo na ubora wa elimu ktk hivyo vyuo under very strict guidelines kama ilivyo huku ughaibuni.
Kuna faida gani ya kuendelea kufungua universities nyingi hapo nchini and then kila siku nikisoma magazeti ya huko nyumbani nasikia most employers wanapendelea kuajiri overseas-trained graduates? Sasa hao wanaoenda hivyo vyuo vya hapo nyumbani kama hawatakiwi na hao waajiri then what's the point ya kufungua utitiri wa vyuo vikuu? Naona ni kupotezeana muda tu. Correct me if I'm wrong!
Ni bora kuwa na universities chache kuliko kuwa na nyingi ambazo ni bogus kama ilivyo Nigeria! Tutakuwa kama mapopo sasa na kuishia kwenye scams!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…