Vyuo vikuu Chadema waja na `washa taa mchana` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo vikuu Chadema waja na `washa taa mchana`

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kweleakwelea, Mar 23, 2011.

 1. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Vyuo vikuu Chadema waja na `washa taa mchana`
  Na Gideon Mwakanosya  22nd March 2011


  [​IMG]
  B-pepe  [​IMG]
  Chapa  [​IMG]
  Maoni
  [​IMG]
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  Vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamezindua kampeni waliyoipa jina la ‘washa taa mchana’, itakayoendeshwa nchi nzima, yenye lengo la kuleta ukombozi wa kifikra kwa wananchi.
  Akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jana mjini hapa, Mratibu wa kampeni hiyo mkoa wa Ruvuma, Likapo Bakari, alieleza kuwa taa hiyo itawashwa rasmi Machi 26 mwaka huu, ikiwa na lengo la kumulika na kuangaza katika kila mkoa nchini ili kuleta ukombozi kwa Watanzania
  Alisema kuwa, ukombozi huo utakuwa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa na kwamba itaanzia mkoa wa Ruvuma kwa kufanya mikutano mbalimbali ya hadhara katika kata zote za Manispaa ya Songea, kwa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wa eneo husika ili waweze kuzijua haki zao, kuzitetea na kuzidai.
  Aliongeza kusema kuwa, kupitia mikutano hiyo pia watahamasisha jamii namna ya kutumia vizuri rasilimali za taifa katika kujiendeleza na kujiongezea kipato na kuwaelimisha maana ya katiba ya nchi na umuhimu wa kudai katiba mpya.
  Akizindua kampeni hiyo, Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ruvuma, Joseph Fuime, alisema maendeleo yoyote hayawezi kufikiwa bila ya kuwepo kwa siasa safi, hivyo wameanzisha kampeni hiyo itakayoendeleza, kukuza na kukitangaza chama kila kona ya nchi na kufungua matawi mapya.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Well done wasomi wetu.......mna deni kubwa kwa taifa hili and this is atleast the least you can do.

  Never give up, the Dawn is so near
   
 3. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda sana! CCM wanasema tusubiri mpaka 2015 wakati kiza kitakapokuwa kimetanda ili wafunge magoli kiurahisi. Ila hii ya kuwasha taa mchana ni safi sana. Kama wachaga biashara asubuhi, jioni unahesabu faida.
  Go CDM go go go goooooo ...
   
 4. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Saaafi sana....
  Taifa hili halina mkombozi zaidi ya vijana wasomi....mapambano daima...na nguvu isambae hadi ngazi ya Masekondarini....ndio ukombozi utafikia mwisho...taifa ni la nguvu mpya na kizazi kipya...
  PAMOJA DAIMA....DAIMA TUNAWEZA...NA PAMOJA TUTAFIKA....WITH PEOPLE'S POWER...YES WE CAN!
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Thats perfect! Kazi ya vijana ni kukijenga chama. Tunamikakati ya kuhakikisha tunashinda ushindi wa kushtusha mwaka 2015. This is the right move to the right direction! Tuwaache wenzetu wakiendekeza majungu na kugombana wao kwa wao sisi tukijenga chama. Wakishtuka itakuwa jioni ishaingia! Tuwashe taa mchana ili tuwachunge wasichakachue tena kura zetu!
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Chadema wanahamasisha ukombozi wa kifikra. Pale ambapo wadau wanaamka kutaka kudai chao mnawatuliza. Yaani kama vile kumringishia mwanao pipi halafu humpi. Lazima atalia tu. Sasa kwa watu wazima hawa unadhani watachukua hatua gani?
   
 7. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kwa makakati hii siku moja mtachukua dola mtatuongoza kataifa, kwa sasa mnatuongoza kwenye halmashauri zetu. Focus sasa iwe mikoa ya nyanda za juu kusini. waachie akina lipumba wahangaike na wajahidina mpaka watakapopigwa mabomu.
   
 8. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Washa Taa Mchana


  Taa hii tunaiwasha itusaidie kuibua yaliyofichika,itusaidie kuhoji na itusaidie kukemea uchafu wa viongozi wasio waadilifu, Nchi yetu haitapotea...23-01-2011 Serengeti.
  [​IMG]
   
 9. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  chadema songea hiyo nzuri sana. na ndicho nafikiria cdm should be doing now, kueneza/ku inject fikra za mabadiliko kwa wananchi huko waliko vijijini, mashuleni, vyuoni na si kukalia inshu ya meya arusha na kutoa 21 days!. vjana songea na mwenyekiti wenu wa wilaya safiiiiiiiii sana!!!
   
 10. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Masikini CCM
   
 11. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Operesheni ''washa taa mchana'' ......ikiwa na lengo la kumulika na kuangaza katika kila mkoa nchini ili kuleta ukombozi kwa Watanzania......kwa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wa eneo husika ili waweze kuzijua haki zao, kuzitetea na kuzidai.

  Bonge la Operesheni. Limekuja Kwa kupindi sahihi, mahali sahihi na kwa watu sahihi. Na kama vipi hawa vijana wpitie na wilaya zilizo gizani sana hasa kule ambako wabunge majambazi ya CCM walipita bila kupingwa. Kule Igunga...etc.
   
 12. S

  SUWI JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa napita nikakutana na hii... Imebidi nisimame kutoa pongezi... Nimefurahia sana.... Wenye kuendekeza majungu na maneno ya taarabu watakoma wenyewe!!!! Songeni mbele na sisi tuko nyuma yenu.
   
Loading...