Vyumba chuo kikuu ni Wizi Mtupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyumba chuo kikuu ni Wizi Mtupu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by TwendeSasa, Jan 28, 2009.

 1. T

  TwendeSasa Senior Member

  #1
  Jan 28, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  vyumba katika hostel za chuo kikuu cha dsm zimekuwa kama biashara ya chuo kupata hela .. wanatoa faini ambayo haina msingi wowote

  Wale wanafunzi wakati wamefukuzwa waliondoka bila kurudisha funguo wanatakiwa kulipia siku zote ambazo walikuwa na ufunguo huo manyumbani kwao

  hali hiyo siyo ya kiutu kabisa na niunyanyasaji wa wazi ambao kama DARUSO ingekuwepo ingewatetea wanafunzi kwa hali na mali

  Kutokana na kutokuwepo kwa chombo chochote ambacho kinaweza kusikiliza matatizo ya wanafunzi basi wanalazimishwa kulipa na kama hutaki unaambia wafanya unalotaka

  Wakati wakufukuza kulikuwepo na harakaharaka sana nje kulikuwa na FFU na wakati huo umepewa mda wa masaa mawili sasa ungewezaje kurudisha funguo na uondoke so walio wahi walirudisha lakini wengi wao hawakuweza

  so Uongoz wa chuo ufikirie hili kiubinadamu na uwasaidie hao wanafunz waingie vyumbani mwao maana shule imeshaanza kubana ni wiki ya tisa inaingia

  Dhumuni la kuweka hapa hili tatizo ni kuwapa Ujumbe uongoz wa Chuo kwasababu hamna njia ingine ambayo ipo rahisi kuwafikia
   
 2. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  Mkataba kati ya Mwanafunzi na USAB(I think it still exist) uko vipi?

  Hapo ndipo pa Kuanzia kabla ya kulalamika kwanza
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hiki sasa ni chuo kikuu cha matatizo, linatoka hili, linakuja jingine...
   
 4. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  vumilieni yatapita!!!!!zusy mbunge viti maalum CHADEMA enzi zetu alifanya sana ufusadi katika masuala ya vyumba vya chuo na baadae USAB
   
 5. T

  TwendeSasa Senior Member

  #5
  Jan 28, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkataba unaruhusu kuvyunjwa wakati wowote kwa jinsi ninavyojua
   
 6. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama utaratibu upo basi ufuatwe.Nadhani kuna tatizo la kifikra..maadili na nidhamu kupungua kutokana na utandawazi.
   
 7. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  we nawe unaboa sasa.... kwani chuo kina wanafunzi wangapi?? inamaana hao wengine waorudisha funguo walipigwa na FFU au hawakuwaona hap FFU pale order ya kuondoka vyumbani ilipotolewa?? Ulishinidwa nini kurudi kesho yake au keshokutwa yake ukakabidhi funguo ya watu?? Uliondoka nayo ili iweje?? ulitegemea chuo walipotaka kukagua vyumba vyao wangefunguaje?? na kwa data nilizonazo mimi ni kwamba chuo iliwalazimu kubomoa milango yote ambayo wanafunzi waliondoka na funguo, na waliporudi kutaka kurejea vyumbani mwao walilazimika kulipia gharama ya kitasa ambacho ilibadilishwa si pesa ya siku zote ambazo umeondoka na key,, mambo mengine ni uchochezi usio na msingi.
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hivi ni wapi huku duniani unaendelea kushikilia nyumba alafu usilipe... wao ni wasomi walitakiwa kuelewa hilo... tutetee wazee sio watu werevu wanaoamua kufanya madudu wenyewe.
   
 9. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  poor estate management, you can't give students all copies of their rooms keys. According to USAB rules, rooms are co-own by USAB and student, that means warden can access students room at any time as necessary, students know this clearly.

  Warden anazocopy za funguo za vyumba vyote, don't kid me.
   
 10. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  nimeishi mlimani, nimeishi mabibo hostel, ninajua kuhusu vyumba vya hapo chuoni. Tena vyumba nilivyopitia funguo ninazo mpaka leo. Tulikuwa tunachongesha funguo pale Sinza Makaburini baada ya USAB kutupatia copy moja wakati room tupo 2 au zaidi. Masuala ya kubebana unayajua wewe?
   
 12. T

  Tango Member

  #12
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  nafikiri si vema kwa mwanafunzi kuondoka na funguo za chumba hata kama amekurupushwa kuondoka. Akae miezi mitatu au minne aje adai kuwa hakuna cha faini wakati hakurudisha funguo kama mkataba unavyosema. Hao wasomi wetu hapo mlimani sijui vipi wanataka kubembelezwa bembelezwa kwa mambo ambayo hayapo kabisa.
  Unajua mimi naishi hosteli hapa ughaibuni, kwanza ni kweli kuwa estates wanazo funguo za ziada lakini pia nimelipa desposit. Ufunguo ukipotea natakiwa kulipia Euros 30 haijalishi mara ngapi utapoteza. Ukitakakubadilisha room ni Euros 70 na ni mpaka kipatikane! Na kama sijarudisha funguo nikaondoka, kumeharibika kitu nimeacha Euros 150 deposit na watailamba. Hii ndio biashara inavyooenda. Sasa hao wanaolalamika kwa kwenda na funguo makwao kwa muda huo sioni cha kuwatetea. Kama ingekuwa biashara ya hao ndugu wangekubali? Pengine kuna watu walikuwa wanavitaka hivyo vyumba wakati ambao wanafunzi hawapo wanaingia gharama ya kwenda kupekua huku na kule bila sababu. Faini ni muhimu na hakuna wizi hapo.
   
Loading...