Vyoo vya kulipia jijini vinakidhi mahitaji

Mozila

Senior Member
Mar 23, 2012
174
47
Hivi vyoo vya kulipia jijini dsm kweli vinakidhi mahitaji ya wakazi mil 4?
 
Uliza kwanza vyoo vya barabarani, ambavyo wasafiri wa mikoani kama vipo, baada ya Mwakyembe kupiga marufuku kunya msituni.
 
vitoke wapi?
posta mpya ushaona choo wewe? au utembee mpaka jirani na station kulikuwa na choo sijui bado kipo?
na hata vyoo vilivyopo vinanuka hatari....kuingia shurti ubane pua
 
Mi huwa natumia vya baa tu, nazuga kununua soda kisha naingia kwenye matundu yao naacha kitu. Vyoo vya mitaani noma! Waweza kukuta kibaka kajibanza ndani au ukaingia cha kike ukapishana na lidume huko.
 
Inabidi tukubali kuwa sisi watanzania kwenye issues za vyoo tupo nyuma sana. Dah!! yaani vyoo ukiingia tu unaweza kuwa kipofu!!
 
Heri nusu shari. Anayehoji kama vyoo vya kulipia vinakidhi au la anapaswa kuanza kuishi kwenye ukweli badala ya ndoto. Kama havifai nenda ambapo havipo. Tunapaswa kujivunia kidogo tulichowezesha. Nairobi hawakuwa na wazo la kuwa navyo. Walifikia mahali pa kuwa na the so called flying toilet. Baada ya kujifunza toka Dar angalau mji wao sasa unatamanika kama siyo kuishika.
 
boss are you serious? kutotembea ni shida
 
Back
Top Bottom