getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,824
Wakuu habari za jumapili..
Awali ya yote napenda kuwapongeza wachezaji, kocha, benchi la ufundi uongozi mashabiki,wapenzi, wanachama wa Simba football club. Na Watanzania wote kwa ushindi wa Jana dhidi ya Algeria..
YES WE CAN..
masikitiko yangu ni kwa menejiment ya Uwanja wa Taifa ama Timu ya uendeshaji wa Uwanja vyoo vya uwanja wa Taifa ni aibu kubwa, kwa uzoefu tulio nao Waswahili hatuna utamaduni wa kuwa na nidhamu kwa maeneo ya vyooni. Ukiingia vyoo vya uwanja wa Taifa kuna Uchafu ulio kithiri mtu anaenda chooni anakunya anatwadha kwa chupa ya juice na kutupia chupa hiyo humo humo.
Mapendekezo yangu.!
Huduma ya vyoo uwanja wa Taifa ibinafsishwe na viwe vyoo vya kulipia hii itaongeza umakini wa usafi na kuhudumia vyoo,na kipato kwa TFF na serikali kwa ujumla kama uwanja unaingiza watu 60,000 na watu 10000 tu wakaenda chooni kila mtu akatoa tsh 100 au kwa huduma yoyote. Bila shaka kutakuwa na kama milioni 100.
Faida sio tu kipato kwa TFF, timu husika na serikali, pia hii itakuwa sehemu ya ajira kwa waliokosa ajira, jambo hili pia litatuhakikishia mazingira salama kwa sisi mashabiki wa soka na uhakika wa Afya zetu na kutuondelea fedheha hii.
Mwisho watakapo binafsisha huduma hii ya vyoo ni bora vikatengwa pia vyoo kwa ajili ya watoto ni aibu kwa mzazi kumpeleka mtoto wake chooni kwa haja ndogo au kubwa kisha akakutana na watu wazima wako uchi sio jambo jema.
Nawasilisha
Sent using Jamii Forums mobile app