VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA TUNAHITAJI UKWELI.

Ceas

Senior Member
Joined
May 5, 2019
Posts
193
Reaction score
204
Tulishuhudia Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasa vyombo vya habari havikujishughulisha na kutuambia ukweli juu ya nani anahusika. Leo Mdude Nyangali baada ya kutojulikana kwa siku kadhaa amepatikana akiwa amedhoofu ikiwa vyombo vya ulinzi na usalama havitajishughulisha na kutuletea Watanzania ukweli kuhusu nani yuko nyuma ya hili, Tutawashuku moja kwa moja kuwa nyinyi ndio wahusika wa hayo.
 
Na wamemuacha tu kwa sababu ya kelele nyingi za watu. Otherwise wangemla kichwa. Wapi Mawazo, wapi Ben
 
Pole sana Mdude Nyangali
 
Asiyeumba haumbui, Tanzania ni nchi yetu, na inasemekana ni nchi ya amani, ila mi sijawahi kuelewa hiyo tafsiri ya neno "Amani" naielewa tu kwa mujibu wa biblia, Gal 5:22 Hasa nikihusisha maisha ya kika mtu bibafsi
 
Yanayofanyika sasa ni yale yaliyokatazwa Gal 5:15
 
Lissu toka anasema hatataja watesi wake mpaka Leo ni hola ngoja labda huyu atasema
Kunde Ekeke vp tena ndg kipigo kimekuelemea nn? kama Lisu alisema hatataja watesi wake unataka awataje wakati unasema alisema hatawataja?
 
NINACHOTAKA KUJILAZIMISHA NI KUAMINI SABABU ZA KISIASA NDIO ZILIZO MPONZA NA SHUGHULI ZAKE ZINGINE ZA KIBIASHARA ILA NAFSI INASITA. TUWE MAKINI NA NYENDO WAZIFANYAZO WATU NJE NA MAISHA YA KISIASA
MUNGU AMPONYE NDUGU YANGU
 
Jamaa kapigika wakuu na wasi wasi hatofungua mdomo kusema yaliyomsibu. Na kama hawajamhasi basi lazima watakuwa wamemfanyia ukatili wa kijinsia. Hapo inahitaji ujasiri mkubwa kuuambia umma yaliyokupata.
 
NINACHOTAKA KUJILAZIMISHA NI KUAMINI SABABU ZA KISIASA NDIO ZILIZO MPONZA NA SHUGHULI ZAKE ZINGINE ZA KIBIASHARA ILA NAFSI INASITA. TUWE MAKINI NA NYENDO WAZIFANYAZO WATU NJE NA MAISHA YA KISIASA
MUNGU AMPONYE NDUGU YANGU
Amina
 
Kwa ninavyoona mimi, ifike wakati sasa wanaokumbana na matukio kama haya waseme ukweli. Wautangazie ulimwengu kile wanachokutana nacho huko wanakopelekwa. Pia watuambie ni nani hasa yupo nyuma ya hili. Wao ndio wanaojua ukweli wote. Amazing! Roma hajasema, Lisu hajawataja japo anapiga kelele kuwa anawafahamu, Mo hajasema. Labda huyu atasema. ila kuna mambo ya kikatili sana hapa nchini. Natamani mmoja aanike ukweli aliye jasiri sana juu ya udhalimu na ushetani huu NA KUWATAJA WALIO NYUMA YA HILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…