Vyombo vya habari na ushabiki wa hatari

Vyombo vya habari na ushabiki wa hatari

Sikiliza Redio Imani na Uhuru kama umechoka kusikiliza Mawingu FM!
 
Vimeanza kuwa vyombo vya hatari,badala ya kuwa vyombo vya habari.
Kwa mfumo wa vyombo vya habari vya TZ, naweza kusema unaratibiwa na kuwekewa mikakati ya hali ya juu na CCM. Nitafafanua kama ifuatavyo. Tuna vyombo vya habari vya makundi mbalimbali hapa TZ. Tuna vyombo vya habari vya Umma vinavyoendeshwa kwa kodi zetu, vyombo hivyo ni kama vile TBC-TV, TBC Radio, magazeti ya Daily News na Habari leo.Vipo vyombo vinavyomilikiwa na vyama vya siasa,kama vile Radio Uhuru na gazeti la Uhuru,yanayomilikiwa na CCM, Vipo vyombo vinavyomilikiwa na taasisi za dini,kama vile radio Imaan, radio Tumaini nk. Pia vipo vyombo vya habari ambavyo vinapaswa kuwa huru, lakini kwa bahati mbaya sana, havipo huru! Katika hali halisi vyombo vingi vya habari vya Umma na vile vinavyojiita viko huru, vinafanya kazi kwa matakwa ya wanamagamba! Hivi ni nani asiyejua kuwa TBC na magazeti ya Daily news na Habari leo ingawa ni vyombo vya Umma vinavyoendeshwa kwa kodi ya wananchi, lakini kwa asilimia kama 99 vimeegemea upande wa CCM na wakati wote vinajitahidi kuvichafua vyama serious vya upinzani na kukifagilia kwa nguvu zote chama cha magamba??!! Hivi ni nani asiyejua kuwa kutokana na uswahiba wa Joseph Kusaga wa Clouds na JK, Clouds radio imekuwa mpiga debe mkuu wa CCM? Hivi ni nani asiyejua kuwa magazeti ya Mtanzania, Majira, Jamboleo na Tazama ingawa yanajiita ni magazeti huru,lakini wahariri wao hawako huru, kwa kuwa wameelekezwa na wamiliki wa vyombo hivyo kuwa wakiuke msingi mkubwa wa chombo chochote cha habari huru ambapo kinapaswa kubalance story na badala yake vyombo hivyo vimekuwa ni vya kuendesha propaganda kwa ajili ya kuinufaisha CCM kuvizidi hata vyombo vyao rasmi vya CCM, magazeti ya uhuru na radio yao ya uhuru? Kwa hiyo hivyo vyombo vya habari vinavyojiita viko huru, kama Clouds radio vinapaswa kuwa huru kiukweli, kinyume cha hapo, wananchi watavikimbia na vitakosa wasikilizaji!! Kwa hiyo ni hiari yao vyombo hivyo kurudi kwenye mstari na kutimiza majukumu yao kwa jinsi taaluma yao ya habari inavyotaka, ama sivyo ipo siku, watajikuta kwa mfano, hao Clouds radio, wanaobaki kuisikiliza radio hiyo wanakuwa wafanyakazi wenyewe na familia zao!!
 
Kibonde ni mganga njaa hana maadili ya utangazaji hata kidogo na mvivu wa kufikiri ndo maana yeye kila kitu ana kirusha hewani na kwa kuwa ni kilaza hajui athari zake kwa taifa. Kwa kweli kibonde ni janga la kitaifa
Mkuu,

It seems like umekariri maisha na wewe ndiye ambaye unashindwa kusoma alama za nyakati kwasababu kama ungekuwa unasoma alama za nyakati ungeelewa kwamba Kibonde na Clouds FM hawajaanza kulalamikiwa leo wala jana lakini hakuna mabadiliko yeyote sanasana wanazidisha. Kama ulimsikiliza jana kwenye kipindi cha Jahazi utaelewa ninachomaanisha ninapokwambia wanazidisha.

Soma alama za nyakati, hii njia ya kulalamika kwenye haya majukwaa imeshaFail.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom