Vyombo vya habari msitumike kukandamiza wananchi

mlemwa

Member
Jan 8, 2016
8
0
Naandika haya kwa masikitiko makubwa baada ya kushuhudia upotoshaji mkubwa wa habari zinazochukuliwa na vyombo vya habari kwa kuwapendelea wawekezaji wa mgodi wa TANZANITE ONE.

Ulipotokea mgomo mnamo February mosi 2016 waandishi wa habari walipka habari hata kufikia kuweka kwenye taarifa ya habari documentary isiyokuwa sahihi ikimuonesha marehem akifungua geti. Hii inasikitisha wapendwa

Kuna habari pia chini ya kapeti kuwa kesho kuna wahariri Fulani wameandaliwa kwenda kuisafisha kampuni kwa kuandika mazuri yake huku hali halisi haiko ivo. Ikumbukwe kampuni hii iko kwenye mgogoro na wafanyakazi wapatao 201 na ni juzi Tu kumetokea ajali ya wachimbaji kuangukiwa na mgodi.

Serikali kuweni macho na takukuru fanyeni kazi ipasavyo tunaweza pata majipu mapya
 
Wawekezaji wamelata wahariri kutoka Dar na wanaingia hapo mgodini kesho jumatatu 14 march kwa lengo la kuzuia habari za uovu wa Tanzaniteone,kwa nini siku zote tangu wapewe mgodi hawajawahi kuwaleta?Lengo lao ni kuuuwa habari za uovu wa Tanzanite one maana mhariri ndiye mwenye maamuzi ya kusema habari hii itoke au isitoke.kweli nchi yetu imefikia hapa?au ni kwa kuwa watu hawa wana hela sasa wanazitumia vibaya?lakini naamini hata kama watawachukua wahariri si wote watakuja kufanya huo ujinga na kwa hakika tutawarusha hewani soon wakija tumechoka na ubabaishaji wa wazawa hawa.kweli mvunja nchi ni mwananchi.
 
Back
Top Bottom