Vyeti vyenye Utata

Vyeti vyenye Utata

Chiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2008
Posts
4,151
Reaction score
5,025
mara ya kwanza nilipoliona tatizo hili, sikuliona kwa mapana sana kwakuwa nilikuwa naamini waliofanya hivyo toka mwanzo walijua risk wanayochukua na niliamini walijipanga jinsi ya kukabiliana nayo. kumbe sivyo hivyo ,binadamu husahau na ndivyo kilivyotokea kwa wengi na matokeo yake ni maumivu na machungu mazito sana kwao na hasa wakikabiliwa na mzigo na uchungu mzito kwa yaliyotokea.
binafsi nauona upungufu kwa pande zote tatu serikali ambaye ni mdau mkubwa, muhusika na jamii kwa jumla ambyo ndio tuliotengeneza machungu yaha kwa kuwaelekeza wenzetu kuwa inawezekana fanya hivi au vile.
kuna hasara kubwa sana kwa hawa watu kwa yale yaliyotokea kwao na kwa wale waliokuwa wanawaudumia pia. mfano kwa daktari bingwa aliyefuzu vizuri kozi yake ya udaktari na amekuwa akiwaudumia vizuri watu wake na akiaminika akiwa na vyeti halali vya udaktari ila hana cheti cha form four, kumtoa huyu katika huduma ni hasara kubwa kwa taifa.
naweza kueleza na kutoa mifano mingi lakini ifike wakati nini kifanyike:-
  • wale wenye taaluma wajitambue kuwa pamoja na mapungufu hayo wao wanauwezo na uzoefu mnzuri wa kufanya kazi hiyo na wajivunie kwa uwezo wao.
  • jamii itambue mchango waliotoa katika mafanikio yao kama wataalamu. inasikitisha unakutana na mtaalamu wa kilimo na mifugo wa kata ambaye amekuwa akiwasaidia kwa kiasi kikubwa wanajamii lakini leo tunamsomea na kumwona hafai tukisahau tulivyokuwa tukimwamsha ahudumie ng'ombe wako wakizaa.
  • serikali nafikiri bado inahitaji kuangalia upya ni kwa jinsi gani watu hawa wanaweza kutumika na sekta binafsi kwa kutoa vyeti vya kuwatambua kuwa ni watendaji wazuri ila hawakuweza kukidhi vigezo vya ajira serikalini.
  • mwisho jamii haitakiwi kuwadharau na kuwanyanyapaa kupita kiasi kwa zaidi ya ugonjwa usio na jina wala tiba kwa kuwa bado tunawahitaji kwa maendeleo yetu.
  • pia walioathilika wajikubali na wajipange na wapunguze maumivu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili. bado jamii inawahitaji na fursa bado zipo msiogope.
 
Huyo daktari aende Zambia, Botswana wanatafuta madaktari. Usipende kulalamika hata kama ni wewe. Funguka watu wakusaidie maisha yaende. Serikali ina wenyewe akina DAB
 
Tena ninyi madaktari ndio mmezidi umagumashi, kama ulikuwa una akili kwa nini usi re seat ili kupata cheti chako badala ya kwenda kutafuta index number za watu na kwenda kujichongea vyeti stationary bila hata mwenye cheti kujua, halafu unajitengenezea uhalali? There is no right out of an illegal act "Ex turpi causa non oritur actio" kwa kujiokoa jisalimishe na ukaanze shule upya maana akili yako itakuwa imekwisha amka. Uzuri fani ya udaktari kama unaipenda hata mzee anaweza ifanya na ile life sparm wanayoisema wazungu dhidi ya waafrika ni ya uongo kwani watu wanatusua hadi miaka 110
 
mara ya kwanza nilipoliona tatizo hili, sikuliona kwa mapana sana kwakuwa nilikuwa naamini waliofanya hivyo toka mwanzo walijua risk wanayochukua na niliamini walijipanga jinsi ya kukabiliana nayo. kumbe sivyo hivyo ,binadamu husahau na ndivyo kilivyotokea kwa wengi na matokeo yake ni maumivu na machungu mazito sana kwao na hasa wakikabiliwa na mzigo na uchungu mzito kwa yaliyotokea.
binafsi nauona upungufu kwa pande zote tatu serikali ambaye ni mdau mkubwa, muhusika na jamii kwa jumla ambyo ndio tuliotengeneza machungu yaha kwa kuwaelekeza wenzetu kuwa inawezekana fanya hivi au vile.
kuna hasara kubwa sana kwa hawa watu kwa yale yaliyotokea kwao na kwa wale waliokuwa wanawaudumia pia. mfano kwa daktari bingwa aliyefuzu vizuri kozi yake ya udaktari na amekuwa akiwaudumia vizuri watu wake na akiaminika akiwa na vyeti halali vya udaktari ila hana cheti cha form four, kumtoa huyu katika huduma ni hasara kubwa kwa taifa.
naweza kueleza na kutoa mifano mingi lakini ifike wakati nini kifanyike:-
  • wale wenye taaluma wajitambue kuwa pamoja na mapungufu hayo wao wanauwezo na uzoefu mnzuri wa kufanya kazi hiyo na wajivunie kwa uwezo wao.
  • jamii itambue mchango waliotoa katika mafanikio yao kama wataalamu. inasikitisha unakutana na mtaalamu wa kilimo na mifugo wa kata ambaye amekuwa akiwasaidia kwa kiasi kikubwa wanajamii lakini leo tunamsomea na kumwona hafai tukisahau tulivyokuwa tukimwamsha ahudumie ng'ombe wako wakizaa.
  • serikali nafikiri bado inahitaji kuangalia upya ni kwa jinsi gani watu hawa wanaweza kutumika na sekta binafsi kwa kutoa vyeti vya kuwatambua kuwa ni watendaji wazuri ila hawakuweza kukidhi vigezo vya ajira serikalini.
  • mwisho jamii haitakiwi kuwadharau na kuwanyanyapaa kupita kiasi kwa zaidi ya ugonjwa usio na jina wala tiba kwa kuwa bado tunawahitaji kwa maendeleo yetu.
  • pia walioathilika wajikubali na wajipange na wapunguze maumivu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili. bado jamii inawahitaji na fursa bado zipo msiogope.
Huo ni upande mmoja wa shilingi. Na je kwa upande wa walioumizwa na u fake wa waliodhaniwa kuwa wanataaluma halali kumbe sivyo na waliumiza watu unawazungumziaje?
 
hao ni feki kabisa na wanastahili walichovuna
kwangu nazungumzia wale waliokuwa waadilifu na wanavyeti vya taaluma halali na walienda darasani ila wanakosa chiti cha kidato cha nne.
 
Back
Top Bottom