Vyeti vyasaidia watu kupata mkopo CRDB

Jean piaget

Senior Member
Mar 15, 2014
143
0
Hii tarifa ya kuweka vyeti vya shule/chuo dhamana ili upate mkopo CRDB mimi naona haiko sawa kabisa, kwa sababu unapokopa lazima urudishe mkopo uliokopa,
Je endapo utashindwa kurudisha mkopo kwa sababu mbalimbal bank itafanyia nini vyeti vya mhusika?

Pia mhusika atashindwa kuomba kazi yeyote endapo biashara yake itagoma.
Je kwa upande wa bank haioni kwamba haitofaidika na chochote na wale watakaoshindwa kurudisha mkopo? Maana lengo la bank ni kupata RIBA zaidi, je hivyo vyeti vitatoaje riba maana hawawez kuviuza kama ilivo kwenye nyumba, kiwanja au mali zingine.

NB: great thinkers naomba tujadili hili
 

BRAVO 2 ZERO

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,031
2,000
Basi ilitakiwa ulete habari kamili ili tuweze kujadili kwani kujadili habari isiyokuwa na uhakika ni sawa na kupoteza nguvu na mda
 

Jean piaget

Senior Member
Mar 15, 2014
143
0
Basi ilitakiwa ulete habari kamili ili tuweze kujadili kwani kujadili habari isiyokuwa na uhakika ni sawa na kupoteza nguvu na mda


Tambua hata tetesi inaweza badilika na kuwa factual information, mtu hadi kwenda bank kufatilia mkopo naamini hakukurupuka lazima alipata taarifa,
 

BRAVO 2 ZERO

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,031
2,000
Lete data kwanza ndipo tujadili

Kweli kabisa,jamaa kadai kuwa kunajamaa yake kaenda lakini hajamjulisha kilichotokea huko sasa si ni bora angemuuliza kwanza ndio arudi na Maelezo kamili ili tujadili haya maswala ya kujadili tetesi mhhh.
 

CHIKITITA

JF-Expert Member
May 1, 2013
446
195
Huu mkopo haumuhusu kila muhitimu, ila kwa wale ambao watataka kujiajili katika sector ya kilimo. unapewa mkopo chini ya uangalizi wao kupitia taasis furani kutoka Dernmark i think, unarejesha mkopo mara tu baada ya mavuno. Huu mkopo upo siku nyingi CRDB wakulima wasio na dhamana wamefaidika nao na pia riba ni ndogo. Tembelea Tawi la CRDB kwa maelezo zaidi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom