mhugo hantish
Senior Member
- Apr 21, 2015
- 137
- 36
Mpaka sasa ninavyoandika thread hii naugua kwa maumivu makali sana juu ya nchi yangu Tanzania.
Issue yenyewe ni hii hapa...
Mimi nimeoa Nina mke mmoja tangu mwaka 2016 mwezi wa 10. Tulipotakiwa kutunukiwa vyeti/shahada za ndoa takatifu Mchungaji alituambia kwamba tusubiri kidogo vyeti tumeshaagiza na vitafika soon ndani ya muda wa mwezi mmoja.
Ni kweli tulisubiri. Lakini hadi kufika tar 18/2/2017 nilipoenda tena kumwulizia mchungaji wetu atupatie vyeti vyetu akatuambia kwamba hadi sasa bado hawajapewa toka wizarani. Na kwenye stock zao kama ofisi ya mchungaji zimeisha. Hadi leo nimeuliza lakini majibu ni yale yale na zaidi sana hata mchungaji nae anashindwa kufaham ni nini kinazuia vyeti vya ndoa kutolewa.
Swali langu kwa wizara husika ni hili.. Kipi kimepelekea tukose vyeti hadi leo hii? Je, Kuna uhakiki wa ndoa hewa(feki)?, Je, hamdhani ya kwamba kwa kukosa kwetu vyeti tunashindwa kutambulika kisheria kwamba Sisi ni wanandoa halali?
Je, kwa kukosa kwetu vyeti/shahada hamdhani ya kwamba tunanyimwa haki stahili anazopaswa kupatiwa kama mwanandoa halali? Na hii inakuhusu hasa wafanya kazi.
Je, ni kipi kimechelewesha ama kimekwamisha kutoa vyeti ambacho hakikustahili kutolewa ufafanuzi kwa raia wema wa Tanzania?
Na Je, ni nini mtazamo wenu kwa hili jambo?
Kama wahusika wataliona, nitafurahi sana na zaidi. Maana mimi ni muathirika wa jambo hili na sina utatuzi kwenye hili maana sijapata taarifa yoyote toka wizarani zaidi ya HATUJUI/HATUFAHAMU.
Mwinjilist.