Vyeti vya elimu havina thamani kama unavyodhani: Mawazo ya mwajiri

Vizuri

Mwalimu umesema afundishe tuition, hoja yako ni kukusanya na kazi zako.

Sijaelewa mwalimu haikusanye darasa lake la tuition na wanafunzi wake waingie kwenye Email au Bahasha.

Eliza sio blaa blaa
Tengeneza hata lesson plan;
notes za somo lako
Tengeneza hata online tutorials ( hii inaweza kua audio au short video ukielezea topic)

Tumia ubunifu wako kuonyesha mwajili kwamba we ni zaidi ya cheti
 
Ok

nimemuuliza jamaa, mjibie rafaiki yangu ni MWALIM yeye aambatanishe nini??
Kuna mifano nimeitoa katika maelezo yangu hapo juu, hapo nimetumia career ya engineering lakini hiyo mifano inaweza kuwa applicable katika cares zingine.

Kitu cha msingi ni awe na uwezo wa kuonyesha kwanini nafasi ile apewe yeye na siyo mwingine ilihali wote wana degree za ualimu na ufaulu mzuri kama wake?

Kipi kinamtofautisha na waalimu wengine? Ana nini ambacho waalimu wengine hawana? Maana kama ni vyeti na matokeo mazuri wengi wanazo.
 
Tengeneza hata lesson plan;
notes za somo lako
Tengeneza hata online tutorials ( hii inaweza kua audio au short video ukielezea topic)

Tumia ubunifu wako kuonyesha mwajili kwamba we ni zaidi ya cheti
Mfano ulio hai kabisa huu. Asante mkuu.
 
Recruitment ina procedures zake, huwezi ku skipe au ku ignore hatua unapofanya staffing, lazima uweke vigezo na sifa unavyotaka wewe kama muajiri na tunapo ongelea sifa vyeti ni kitu cha muhimu sana huwezi kubeza pamoja na uzoefu kwa baadhi ya post. So vijana watengeneze vyeti vizuri wawe smart kichwani kama kwenye vyeti.

Waajiri wote wangekuwa kama wewe unawaza kuibiwa, kukimbiwa hiyo experience vijana watatoa wapi?
Sikatai uwepo wa procedures: kwa nguvu zote fuata procedure pale unapopaswa kufuata procedures.

Lakini mwisho wa siku angalia sehemu gani unapoweza kuwa mbunifu na kuonyesha experience yako.

Mi nimetoa kama tip on how to stand out hasa hasa ukiwa unaomba competitive jobs...
 
Ungechukua la saba wenye experience na kazi, kwanini uwasumbue watu na degree zao?

Hivi wee unazani hizo degree hutolewa/huchukuliwa kama kugawa karanga?

Hivi wee unajua msoto wa Elim kweli?

Hivi ukiambiwa ulipe mshahara halali wa degree utaweza?

We uskariri maisha experience ni kitu rahisi sana kuipata hata ndani ya siku tatu mtu akiwa tayari kazini

Kama la saba amekuwa na uwezo wa kuwa na experience, we huoni huyu mwenye degree (fast learner) bado anauwezo wa kupata hiyo experience ndani ya ajira/kazi, mara 10 zaid ya huyo wa la saba.

Kwanza huu utaratibu wa experience haukuwepo, miaka ya juz kati hapa mkihitimu mnafwatwa chuoni mkaanze kazi moja kwa moja na mnalipwa kwa kiwango stahiki cha level ya degree.
Point sio kwamba sizingatii elimu, lakini mwisho wa siku yule anayeonesha uwezo wa kazi anakuwa mwepesi kuajili dhidi ya yule mwenye cheti tu.

Degree mi naifahamu ni ngumu kupata, lakini mwisho wa siku: watu 40+ wana vyeti

Watu watano wana kazi zinazoonesha uwezo wa kazi, style yao ya kazi, mapungufu yao, na makamiliko yao: yani wanauwezo wa kuanza mda huo huo.

We ungemuajili nani?
 
Kwa hiyo uliwaamini hao wachache kwa kuwa waliandika kwenye CV. Maajabu hayataisha duniani. Kumbe kuandika tu, very simple! Mimi nitaendelea kumuamini mwenye vyeti vilivyothibitishwa na taasisi au mamlaka ninayoiamini. Mwenye vyeti vizuri ana akili kichwani, maana yake atakuwa fast learner wa kazi zake.

Kufanya kazi kwa uzoefu (mazoea) hakuwezi kuleta ubunifu mpya maana mtu hana akili hiyo ya darasani, yeye anachojua ni hicho tu, nje ya box hana uwezo wa kuleta ubunifu mpya.

Kwa ufupi mimi ni muumini wa vyeti vya darasani (vilivyohakikiwa kuwa ni original from a respective institution), mwenye vyeti vizuri anaweza akatumia mwezi mmoja kujifunza kazi, lakini mwenye uzoefu tu bila akili atatumia miaka mitatu kupata cheti, can you see the difference?
We ndo Tatizo, hata ujasoma og post lakini ulishawahi commenting.

Mi sijasema experience ya CV!!!

Mi nasema evidence ya uwezo wa kazi.

Sample ya kazi yako kwa mfano.

Unalalamika kuhusu kufanya kazi kwa mazoea, lakini jibu lako linaonesha unajibu kwa mazoea.
 
Wewe umechanganyikiwa kweli na mwehu.

Kwenye tangazo la kazi lolote lazima liweke vitu ambavyo muombaji anatakiwa kuambatanisha.

Kwa mfano, tangazo likieleza kuwa unatakiwa uambatanishe cheti cha form four na cha kuzaliwa, basi unapaswa kuambatanisha vyeti hivyo viwili. Ukiambatanisha zaidi labda cheti cha diploma au degree basi utakuwa ume-over qualify hivyo unakosa kazi, ukiambatanisha pungufu ya ulivyoambiwa pia umekosa kazi.

Mtu anaomba kazi kwa kufuata vigezo vya kwenye tangazo sio maneno yako ya kipuuzi. Hujui hata abc za kusaili watu kwenye kazi -

Hujui hata Recruitment Procedures​

HILI NDO TATIZO KUBWA SANA KWA WAAJILIWA WA TANZANIA: MAZOEA

Yani wanafikili kila kitu kinafanana, hawana uwezo wa kutoka nje ya box.

Kwa hiyo kila mtu anayetaka huduma flani anapaswa kuangalia vyeti vya form4

Nikitaka mtu wa kunisaidia mambo ya IT niangalie vyeti vya form4 vya kazi gani?!!!

Nikitaka mtu kunisaidia maswala ya kurekebisha website au project yangu niangalie cheti cha darasa la saba cha nini?!!!

ACHA MAZOEA, KUWA CREATIVE
 
Ungechukua la saba wenye experience na kazi, kwanini uwasumbue watu na degree zao?

Hivi wee unazani hizo degree hutolewa/huchukuliwa kama kugawa karanga?

Hivi wee unajua msoto wa Elim kweli?

Hivi ukiambiwa ulipe mshahara halali wa degree utaweza?

We uskariri maisha experience ni kitu rahisi sana kuipata hata ndani ya siku tatu mtu akiwa tayari kazini

Kama la saba amekuwa na uwezo wa kuwa na experience, we huoni huyu mwenye degree (fast learner) bado anauwezo wa kupata hiyo experience ndani ya ajira/kazi, mara 10 zaid ya huyo wa la saba.

Kwanza huu utaratibu wa experience haukuwepo, miaka ya juz kati hapa mkihitimu mnafwatwa chuoni mkaanze kazi moja kwa moja na mnalipwa kwa kiwango stahiki cha level ya degree.
Huyu jamaa hawezi kulipa kutokana na cheti amezoea vibarua wasio na vyeti ndivyo nilivyomwelewa
 
Experience utaipata wapi ndo kwanza unatokea chuoni ?!. Hizi ni lugha za kichoyo

Odhis *
Hapa ndo ndugu yangu unapaswa kuwa creative: sio lazima uajiliwe

Kwenye IT kwamfano, kuna vijana wanafanta project zao wenyewe.

Point ni kufanya kitu kinachoweza kuonesha uwezo, sio experience ya CV tu
 
Tengeneza hata lesson plan;
notes za somo lako
Tengeneza hata online tutorials ( hii inaweza kua audio au short video ukielezea topic)

Tumia ubunifu wako kuonyesha mwajili kwamba we ni zaidi ya cheti
Unamaanisha ni-Submitt na Lesson plan, Notes na Flash iliyokuwa na Video yangu ndani nikifundisha.
 
HILI NDO TATIZO KUBWA SANA KWA WAAJILIWA WA TANZANIA: MAZOEA

Yani wanafikili kila kitu kinafanana, hawana uwezo wa kutoka nje ya box.

Kwa hiyo kila mtu anayetaka huduma flani anapaswa kuangalia vyeti vya form4

Nikitaka mtu wa kunisaidia mambo ya IT niangalie vyeti vya form4 vya kazi gani?!!!

Nikitaka mtu kunisaidia maswala ya kurekebisha website au project yangu niangalie cheti cha darasa la saba cha nini?!!!

ACHA MAZOEA, KUWA CREATIVE

Naongea na mwehu au na mwendawazimu?

Nimeshakuambia mtu anatuma viambatanisho kulingana na tangazo linavyohitaji, kama tangazo linasema ambatanisha hiki na hiki basi unapaswa kufuata maelekezo.

Kweli waalimu wanakazi sana hasa kufundisha kiazi kama wewe
 
Mtu kama anataka kukupa kazi anakupa tuu acheni visingizio vya experience hizi ni dalili za kichoyo na kazi za masimango.
 
Pokea ushauri utafakari uufanyie kazi.

Unaweza kufundisha tuition ukawa na data base ya uliowafundisha na jinsi walivyofaulu katika ulichokuwa unafundisha.Unaweza kuwa na report personal ikihitajika unaotoa.

Nimejaribu kumuelewa mtoa mada
Vizuri

Mwalimu umesema afundishe tuition, hoja yako ni kukusanya na kazi zako.

Sijaelewa mwalimu haikusanye darasa lake la tuition na wanafunzi wake waingie kwenye Email au Bahasha.

Eliza sio blaa blaa
 
Unamaanisha ni-Submitt na Lesson plan, Notes na Flash iliyokuwa na Video yangu ndani nikifundisha.
Ndugu, mi sisemi nenda serikalini na u-submit hivyo vitu.

Point yangu ni kwamba, unapo-omba kazi; hasa hasa online, onesha jinsi gani unaweza kuchangia kwenye hiyo organisation.

Kama we ni mwalimu, waweza onesha uwezo wako kwa kutumia njia bunifu. Ubunifu mi juu yako, lakini point ni ile ile, stand out.

Hii ni haswaa kwa mashirika madogo binafsi yanayotafuta mtu wa kuongeza thamani kwenye film zao.

Upungukuwi chochote.
 
Mtu kama anataka kukupa kazi anakupa tuu acheni visingizio vya experience hizi ni dalili za kichoyo na kazi za masimango.
Mkuu kuna kitu wengi wanaamini hasa katika suala la kupata ajira.

Hicho kitu ni CONNECTION.

Tatizo wengi hawajui connection inaanza na yeye mwenyewe kutokana na kile alichonacho.

Unaweza tuma taarifa zako ila kutokana na ushindani kuwa mkubwa ukakosa nafasi katik kampuni A, lakini kama una sifa za ziada ambazo kweli zinadhiirisha utofauti wako siyo ajabu muajiri wa kampuni A akakuunganisha na kampuni B ambayo anajuana nao na anaona wewe utawafaa.

Hiyo ndiyo connection ya kweli ukiachana na ya undugu kubebana.

Unataka connection, jitengeneze wewe kwanza na hizo connection zitakufuata.

Tofauti na hayo mkuu, kumbuka watu wapo serious na maisha, habari ya kuajiriwa kisa utu halafu uaribu kazi za watu hakuna anayevumilia karne hii.

Kila mwanadamu ni selfish, hata huyo anaye kuajiri siyo kwamba anakupenda, hapana. Ni kwamba anaona kupitia wewe mambo yake yataenda vizuri, na ukumbuke siku mambo yasipoenda vizuri mda wowote unafukuzwa analetwa mwingine mwenye uwezo zaidi yako ili mambo ya boss yaende vizuri.

Life is not fair, na lazima ujifunze kuishi nayo hivyohivyo.
 
Mtu akishahitimu degree yake tayari ana experience ya kutosha kwenye eneo alilosomea, ndo maana dakatari akihitimu leo kesho tu yupo tayari kutibu wagonjwa. Labda unaongelea experience ya uongozi au kwenye taaluma fulani iwapo wanahitaji mtu wa ku cover a senior position.
Natamani waisikie waajiri hii.
 
Natamani waisikie waajiri hii
Mkuu kinachowekwa sawa hapa ni hiki hapa.

Una bulb mbili, zote lengo ni kutoa mwanga.

Ila bulb ya kwanza inaweza waka na kutoa mwanga kama ilivyo kawaida.

Na bulb ya pili inatoa mwanga ila ina uwezo wa kuji-adjust kiwango cha mwanga kutegemeana na uhitaji wako muda wowote.

Thamani za bulb zote ni moja.

Utachukua bulb gani kati ya ya kwanza na ya pili?
 
Ya pili coz ni more advanced Ina cha ziada kuliko bulb ya kwanza.
 
Ya pili coz ni more advanced Ina cha ziada kuliko bulb ya kwanza.
Uko sahihi mkuu. Wahitimu wote wana experience pale wanapomaliza elimu ya juu, ila waajiri wanaangalia nani mwenye cha ziada katika career yake tofauti na wengine, maan huyo ataleta manufaa na kunufaisha zaidi kampuni.

Hawawezi kuambia ukweli huo, kwamba tumekuacha wewe na kumchukua huyu kwasababu wewe huna hiki na huyu anacho hiki na hiki na kile, ndiyo maana wengi wamemtafsiri mtoa mada tofauti, ila mtoa mada yeye kama muajiri katoa ule ukweli ili wengine kujifunza na kujiongeza.
 
Back
Top Bottom