Vyeti vya darasa la saba havipo tena

Vyeti vya darasa la saba havipo tena

Hivi vyeti vya shule ya msingi vya mwaka 2007 vilishatoka?
 
Naomba kuuluza hivi hicho cheti huwa kinauliziwa kwenye ajira au kujiunga na elimu ya sekondari au elimu ya juu?
Mimi sikijui kinafananaje na sijapata kuombwa hicho cheti popote pale.
Wakati mwingine umuhimu wake unaweza kujitokeza katika mazingira usiyoyatarajia. Mfano mbeleni mtu akiibuka na kudai wewe ni wale akina Bashite wakati sivyo kama una cheti cha darasa la saba chenye jina lako si utakata mzizi wa fitina kwa kukionyesha?
 
Darasa la 7 vyeti vinatolewa vizuri tu
Mimi changu ninacho, nilimaliza 2009

Mfano ukienda immigration unaulizwa kama una cheti cha la 7? Incase hauna vya sekondari (ukihitaji passport)
 
Hapana mkuu, kinatengenezwa na kutolewa na Baraza LA mtihani LA taifa, kina sahihi prof. Msonde mtendaji mkuu was baraza LA mtihani LA taifa NECTA na siyo NACTE
 
Wakati mwingine umuhimu wake unaweza kujitokeza katika mazingira usiyoyatarajia. Mfano mbeleni mtu akiibuka na kudai wewe ni wale akina Bashite wakati sivyo kama una cheti cha darasa la saba chenye jina lako si utakata mzizi wa fitina kwa kukionyesha?
Cheti cha darasa la saba hakiwezi kuwa ni uthibitisho wa uraia sheria zetu, kama cheti cha kuzaliwa tu kimeandikwa huu sio uthibitisho wa urai!

Mtoto wa raia wa kigeni anaweza kuzaliwa na kusoma Tanzania lakini akakosa sifa za kuwa raia.
 
Cheti cha darasa la saba hakiwezi kuwa ni uthibitisho wa uraia sheria zetu, kama cheti cha kuzaliwa tu kimeandikwa huu sio uthibitisho wa uraia!

Mtoto wa raia wa kigeni anaweza kuzaliwa na kusoma Tanzania lakini akakosa sifa za kuwa raia.
Hebu tukumbushane mkuu. Suala la Bashite lilihusu uraia?
 
Habari za leo wakuu

Kuna mama mmoja analalamika anafuatilia cheti cha mwanae cha darasa la saba aliyemaliza shule ya msingi inayoitwa Magoza Dar-es-salaam mwaka 2014. Hajapata ushirikiano halmashauri kitengo cha elimu ya msingi, wanamwambia sio jukumu lake kuulizia awaachie walimu.

Walimu wa shule husika wanadai serikali imesitisha kutengeneza vyeti darasa la saba, hivyo hawana vyeti hivyo tangu wahitimu wa 2014.

Je, ni kweli? Naombeni majibu mliopo jikoni

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mama moja bila shaka ni wewe mwenyewe
 
Ndio hivyo mkuu, tofauti na wakati tunasoma sisi, binti yangu kahitimu darasa la saba mwaka 2019, na tulitangaziwa michango yote mpaka gharama za kutengeneza vyeti. na usipotoa mwanao hapati cheti mpaka ulipe
Hizo ni kama Leaving Certificate tu.
 
Kwenye usaili wa majeshini hiko cheti huuliziwa kwa msailiwa.(hasa JKT)

Vyeti vya waliomaliza la saba 2017,18 vipo ila 19 na 16,15 nadhani na 14 bado havijatoka.(kwa mujibu wa Mwl.Mkuu wa shule moja ya msingi Wilaya ya Ilala)

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili linawezekana ikawa kweli. Ina maana kuna miaka Serikali ilisitisha kutengeneza vyeti darasa la saba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Darasa la 7 vyeti vinatolewa vizuri tu
Mimi changu ninacho, nilimaliza 2009

Mfano ukienda immigration unaulizwa kama una cheti cha la 7? Incase hauna vya sekondari (ukihitaji passport)
Je umejaribu kuulizia kwa mwaka 2014,2015,2016 Kama waliohitimu wamepata vyeti? Kama kuna mtu unamfahamu jaribu kumuuliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom