Vyeti feki waombewa huruma serikalini

Vyeti feki waombewa huruma serikalini

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
Aidha TUCTA imesema inajua watu hao walifanya makosa, lakini serikali inapaswa kuwasaidia, ili kupunguza umaskini mbeleni kutokana na wengine umri wa kustaafu ulikuwa umekaribia.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Yahya Msigwa, katika warsha ya kupitia upya sera za UKIMWI na Afya kwa watumishi iliyowahusisha wataalamu kutoka vyama vya wafanyakazi.

Msigwa alisema kuwatoa katika ajira bila kuwapa chochote kunawafanya watumishi hao kuwa maskini ghafla, kwani maisha ya mtumishi ni mshahara wake na haki yake kazini.

Msigwa alisema TUCTA haina tatizo na uamuzi huo wa serikali, lakini watumishi wengine wana mikopo katika taasisi za fedha na benki.

"Kuwatoa ghafla watumishi hao hata benki zinaathirika kwani mikopo hairejeshwi, hivyo suala hilo liangaliwe upya kwa sababu hata benki zinaweza kufa kwa kutorejeshewa fedha zao,” alisema Msigwa.

Alisema ingawa ni makosa kisheria kwa mtumishi kuwa na cheti feki, lakini iangalie kwa jicho la karibu kuwa watumishi hao wana wategemezi ambao walikuwa wakitegemea mishahara ya ndugu zao.

“Sisi kama TUCTA hatuna ugomvi na serikali, lakini ombi letu serikali iangalie jinsi ya kuwasaidia watumishi hawa hata kuwalipa fedha kidogo kwani walikuwa watumishi wazuri tu, ukiacha kosa walilokutwa nalo,” alisema Msigwa.

Alisema tatizo siyo wao bali ni mfumo uliokuwapo wakati wakiingia katika ajira zao kipindi cha nyuma, jambo ambalo nalo linapaswa kuangaliwa, ili waweze kunufaika kidogo.

Aliwataka viongozi wanaoshughulikia matatizo ya wafanyakazi kutatua changamoto zao haraka katika kipindi kifupi, ili kundoa kero ya kusubiri kwa muda mrefu kutatuliwa matatizo yao.

Alisema kumekuwapo na matatizo mengi ya wafanyakazi ambayo huchukua muda mrefu kutatuliwa, jambo ambalo linawakatisha tamaa.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Getrude Sima, alisema wako pamoja na vyama vya wafanyakazi kuhakikisha sera wanayoipitisha inazingatiwa kwa weledi mkubwa na kuwataka washiriki katika upitiaji wa sera hizo kuzingatia jinsia
.

Chanzo: Nipashe
 
kwa kifupi hawa waliacishwa sio kwamba nchi ilikua inataka kuondoa vyeti feki, ni kwamba pesa ya mishahara ilikua hamna na njia pekee ya kupunguza gharama ilikua hiyo ya kupunguza watu kisa vyeti!!
 
serikali ilikuwa inapambana na vyeti feki au ni kubana matumizi tu.
 
Yaani TUCTA wanashindwa kujua adhma ya serikali mpaka sasa!!!
Vyeti feki ni sawa ni tunguli za mchawi, tunguli ni kama tu kinasaba cha uchawi ila uchawi halisi si vyeti feki.
TUCTA ni wanafiki tu, ni tawi la CCM makazini bila watumishi kujua.
Stahiki ngapi zimebanwa na serikali wamekaa kimyaaaaa.
 
Aidha TUCTA imesema inajua watu hao walifanya makosa, lakini serikali inapaswa kuwasaidia, ili kupunguza umaskini mbeleni kutokana na wengine umri wa kustaafu ulikuwa umekaribia.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Yahya Msigwa, katika warsha ya kupitia upya sera za UKIMWI na Afya kwa watumishi iliyowahusisha wataalamu kutoka vyama vya wafanyakazi.

Msigwa alisema kuwatoa katika ajira bila kuwapa chochote kunawafanya watumishi hao kuwa maskini ghafla, kwani maisha ya mtumishi ni mshahara wake na haki yake kazini.

Msigwa alisema TUCTA haina tatizo na uamuzi huo wa serikali, lakini watumishi wengine wana mikopo katika taasisi za fedha na benki.

"Kuwatoa ghafla watumishi hao hata benki zinaathirika kwani mikopo hairejeshwi, hivyo suala hilo liangaliwe upya kwa sababu hata benki zinaweza kufa kwa kutorejeshewa fedha zao,” alisema Msigwa.

Alisema ingawa ni makosa kisheria kwa mtumishi kuwa na cheti feki, lakini iangalie kwa jicho la karibu kuwa watumishi hao wana wategemezi ambao walikuwa wakitegemea mishahara ya ndugu zao.

“Sisi kama TUCTA hatuna ugomvi na serikali, lakini ombi letu serikali iangalie jinsi ya kuwasaidia watumishi hawa hata kuwalipa fedha kidogo kwani walikuwa watumishi wazuri tu, ukiacha kosa walilokutwa nalo,” alisema Msigwa.

Alisema tatizo siyo wao bali ni mfumo uliokuwapo wakati wakiingia katika ajira zao kipindi cha nyuma, jambo ambalo nalo linapaswa kuangaliwa, ili waweze kunufaika kidogo.

Aliwataka viongozi wanaoshughulikia matatizo ya wafanyakazi kutatua changamoto zao haraka katika kipindi kifupi, ili kundoa kero ya kusubiri kwa muda mrefu kutatuliwa matatizo yao.

Alisema kumekuwapo na matatizo mengi ya wafanyakazi ambayo huchukua muda mrefu kutatuliwa, jambo ambalo linawakatisha tamaa.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Getrude Sima, alisema wako pamoja na vyama vya wafanyakazi kuhakikisha sera wanayoipitisha inazingatiwa kwa weledi mkubwa na kuwataka washiriki katika upitiaji wa sera hizo kuzingatia jinsia
.

Chanzo: Nipashe
 
tucta kuwa mtetezi Mara hii itaweza?
Halafu wanachonishangaza ni kwamba wanasubiria kuongelea kwenye workshop sio kwamba wameomba appointment ya kuonana aidha na waziri wa kazi au hata JPM mwenyewe.
 
Yaani TUCTA wanashindwa kujua adhma ya serikali mpaka sasa!!!
Vyeti feki ni sawa ni tunguli za mchawi, tunguli ni kama tu kinasaba cha uchawi ila uchawi halisi si vyeti feki.
TUCTA ni wanafiki tu, ni tawi la CCM makazini bila watumishi kujua.
Stahiki ngapi zimebanwa na serikali wamekaa kimyaaaaa.
ukweli pasina shaka
 
Hata ajira mpya zilizotangazwa ni chache kuliko walioondolewa!, naanza kuamini kuwa lengo halikuwa vyeti, ni serekali haina mshiko hivyo inatafuta kiki zisizo na ulazima. Ikowapi sasa nyongeza ya mishahara kwa waliopo kazini? TUCTA hampo kwa kupigania haki za wafanyakazi. mbona kipindi cha utawala wa JK kulikuwa na maandamano kila kukicha hadi kwa madaktari? na walisikilizwa nyie hamna mbinu mbadala ili magu awasikilize kilio cha wafanyakazi?.
 
Kuna mambo mengine kwa akili hizihizi nyepesi nyepesi huwezi kufikiri ni nini ilikuwa mukhtadha wa kuwaondoa wafanyakazi wenye vyeti feki wakati wengine wapo kazini kwa miongo miwili na ushee hivi. Du inashangaza sana!
 
Vyama vyenyewe vya kutetea wafanyakazi vime paralyse . Vipo tu kisheria lakini kwa hili LA vyeti vilishindwa kujenga hoja kuwatetea wanachama wao. Labda kwa kuwa ni muajiri wao mkuu walishindwa watajengaje hoja kutetea? Kila mtu ikawa ni kujihami yeye mwenyewe asipoteze kazi
 
Aidha TUCTA imesema inajua watu hao walifanya makosa, lakini serikali inapaswa kuwasaidia, ili kupunguza umaskini mbeleni kutokana na wengine umri wa kustaafu ulikuwa umekaribia.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Yahya Msigwa, katika warsha ya kupitia upya sera za UKIMWI na Afya kwa watumishi iliyowahusisha wataalamu kutoka vyama vya wafanyakazi.

Msigwa alisema kuwatoa katika ajira bila kuwapa chochote kunawafanya watumishi hao kuwa maskini ghafla, kwani maisha ya mtumishi ni mshahara wake na haki yake kazini.

Msigwa alisema TUCTA haina tatizo na uamuzi huo wa serikali, lakini watumishi wengine wana mikopo katika taasisi za fedha na benki.

"Kuwatoa ghafla watumishi hao hata benki zinaathirika kwani mikopo hairejeshwi, hivyo suala hilo liangaliwe upya kwa sababu hata benki zinaweza kufa kwa kutorejeshewa fedha zao,” alisema Msigwa.

Alisema ingawa ni makosa kisheria kwa mtumishi kuwa na cheti feki, lakini iangalie kwa jicho la karibu kuwa watumishi hao wana wategemezi ambao walikuwa wakitegemea mishahara ya ndugu zao.

“Sisi kama TUCTA hatuna ugomvi na serikali, lakini ombi letu serikali iangalie jinsi ya kuwasaidia watumishi hawa hata kuwalipa fedha kidogo kwani walikuwa watumishi wazuri tu, ukiacha kosa walilokutwa nalo,” alisema Msigwa.

Alisema tatizo siyo wao bali ni mfumo uliokuwapo wakati wakiingia katika ajira zao kipindi cha nyuma, jambo ambalo nalo linapaswa kuangaliwa, ili waweze kunufaika kidogo.

Aliwataka viongozi wanaoshughulikia matatizo ya wafanyakazi kutatua changamoto zao haraka katika kipindi kifupi, ili kundoa kero ya kusubiri kwa muda mrefu kutatuliwa matatizo yao.

Alisema kumekuwapo na matatizo mengi ya wafanyakazi ambayo huchukua muda mrefu kutatuliwa, jambo ambalo linawakatisha tamaa.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Getrude Sima, alisema wako pamoja na vyama vya wafanyakazi kuhakikisha sera wanayoipitisha inazingatiwa kwa weledi mkubwa na kuwataka washiriki katika upitiaji wa sera hizo kuzingatia jinsia
.

Chanzo: Nipashe
Hivi Mgaya huu ndio mwisho wake wa kufikiri.Watu hawa wameiibia serikali kupitia kwenye ujira ambao hawakustahili.Isitoshe kwa kuwa hawana proper qualifications kwenye kazi ambazo walikuwa wanazifanya,ni lazima wameleta uharibifu kwenye system yetu kwa ujumla.As if that is not enough serikali iwalipe tena fedha!Eti tatizo ni mfumo,yaani mtu kafoji cheti huku akijua anafoji cheti, halafu mfumo ndio uwe tatizo.Mgaya naona anazeeka vibaya.
 
Leo TRA wamefanya usaili watu elfu 30000, nafasi zipo 400 tu, kwahiyo kuna watu wana vyeti halisi lakini hawana ajira,watu wanasotea magamba, eti jitu linaenda pale Buguruni linanunua cheti, kisa Mjomba bosi sehemu anapata ajira, huku wanaostahili wakisota kitaa...hii haikubaliki.
 
Back
Top Bottom